Boramaisha
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 820
- 18
Ndugu zanguni mambo ya kuhamasisha wananchi si magumu kama tunavyoyafikiria. Wananchi wanaelewa kinachoendelea hata wale ambao tunadhani wako vijijini na hawajui kitu. Tukumbuke kwamba Uhuru wa nchi yetu ulipatikana kwa hamasa tena ya viongozi ambao walikuwa hawana elimu yoyote ya juu ukiacha wachache na wananchi ambao walikuwa hawana elimu yoyote. Lakini elimu ya kuzaliwa ya kujue tofauti kati ya JEMA na BAYA ndiyo iliyosaidia kuelewa ubaya wa Serikali ya kikoloni na uzuri wa kuwa na Uhuru na kujitawala wenyewe. Kama iliwezekana wakati huo kwa nini isiwezekane sasa kuwaelimisha wananchi juu ya ubaya na mabaya yanayoendelea nchini chini ya utawala wa CCM?
Hata hivyo, kama ilivyokuwa huko nyuma tayari hata sasa wananchi wameashaelewa tofauti ya "JEMA na BAYA" na wameanza kujichukulia wenyewe maamuzi ya nini cha kufanya pale wanapoona wanabugudhiwa ama kutaka kupokwa haki kazi. Kuna mifano hai:
"WAKAZI wa Kijiji cha Kagongwa, Kata ya Isagehe wilayani hapa, wamechachamaa na kumshinikiza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige aondoke na askari polisi wa kituo kidogo cha Kagongwa kutokana na askari hao kujihusisha na vitendo vya rushwa na ulevi uliokithiri.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki, baada ya wakazi wa kijiji hicho, kuuzuia msafara wa Waziri Maige ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Msalala, alipokuwa akifanya ziara jimboni humo."
Na nje ya DSM nako
"Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala limetumia risasi za moto kuwatawanya wananchi wa eneo la Kigezi Chini, Buyuni katika Kata ya Chanika, baada ya wananchi hao kuzuia gari la polisi wakipinga zoezi la kubomolewa nyumba zao.
Hata hivyo, juhudi za polisi kuwatawanya wananchi hao ziligonga mwamba baada ya wananchi hao kuamua kulizingira gari lao kwa kuchimba mashimo mbele na nyuma huku baadhi yao wakijiamini kwa kuwasogelea vifua mbele na kuwaamuru polisi hao wafanye watakalo ikiwemo kuwapiga risasi ili wafe.
Baada ya wananchi hao kuchachamaa, polisi waliamua kuingia ndani na kujificha.
Hatua ya wananchi hao kufanya hivyo ilikuja baada ya askari hao kufika katika eneo hilo wakiwa na mfanyabiashara aitwaye Abdul Badi, ambaye aliongozana na kikosi cha watu kutoka kampuni moja ya udalali (jina tunalihifadhi) kwa lengo la kuvunja nyumba za wakazi hao kwa madai kuwa eneo hilo ni mali yake.
Katika tukio hilo, mfanyabiashara huyo alilazimika kujificha ndani ya kiti cha gari aina ya DCM walilofika nalo katika eneo hilo baada ya wananchi hao kutaka kumvamia bila kujali kuwa kulikuwa na polisi wenye silaha za moto.
Hali hiyo iliwalazimu polisi hao kuomba msaada kutoka kituoni ambapo baada ya muda mfupi mkuu wa kituo cha Ukonga Stakishari walikotokea askari hao alifika katika eneo la tukio akiwa na diwani wa kata hiyo, Angelina Malembeka, kuweka mambo sawa...."