Agano la damu katika mapenzi lina madhara gani?

Agano la damu katika mapenzi lina madhara gani?

chabby chubby

Member
Joined
Aug 7, 2015
Posts
11
Reaction score
4
Habari Jf,

Hapo katikati niliwahi kupost maswahibu yangu na mpenzi wangu wa zamani. Kuna kitu kinanitatiza sn naombeni mawazo yenu though i might sound weird.. Ni hivi wkt tupo kwenye mahaba motomoto na mpenzi wangu wa zamani tuliwahi kufanya kiapo cha damu.

Tulijikata vidole tukagusanisha damu huku tukisema maneno tukiachana tuharibikiwe and tusipate wapenzi wakudumu khaa! Najiona mjinga sn now je kuna madhara yoyote katika hilo au ni just imani za kijinga tu and if ni tatizo nifanyaje kuliondoa?

Wakati mwingine hua tunafanya mambo ya ajabu sana tunapokua tumekufa tumeoza.
 
Pole sana. Hapo mlichoahid ndicho kitakachokuwa vinginevyo mkae pamoja mtakiane heri upya la sivyo kweli hamtapata hata kama mtapata bado ndoa zenu zitakuwa za shida yaani shida kweli na inaweza ikatafuna had vizaz vyenu vya 3. Wezenu huwa hawali kiapo kwenye mapenz maana mapenz ni sawa na uhai wakat wowote yaweza kufa na kuzikwa licha kupendana tena zaid ya sana.
nitarud nikusumulie yangu juu ya kiapo na mapenz kw ujumla nikirud baadae
 
Ukiamini yatakukuta kweli nakushauri chukulia poa haya mambo ukiyatolea macho nayo yatakutolea pia.
 
Jiandae kwa uliyonaongea.... Au
Katubu Mkuu Mungu wetu ni warehema na anasamehe...
 
Hamna lolote hapo wewe endelea na maisha yako "as if nothing happened". Mbona hata kiapo cha mahakama kinavunjwa "with no consequences"? Watawala wanakiuka kiapo na wanaendelea kuneemeka. Labda kama mgehusisha ushirikina kwenye viapo vyenu hapo ingekuwa ishu si unajua kinachowapata wale wanaokiuka masharti ya waganga wa kienyeji? "Just go on leave those powerless utterances behind your back".
 
Agano lisipoondolewa hugeuka kuwa kifungo cha milele. Wakati mnaunganisha damu zenu, mliongea kwa kumaanisha na mlikuwa na imani kuwa itakuwa kama mlivyosema. Kwa maneno yenu mliumba kitu (kwenye ulimwengu wa roho) kwamba mkiachana tu, hakuna atakayepata mpenzi wa kudumu na ndivyo itakavyokuwa sawasawa na mlivyojinenea.

Ulikuwa unajua unachokifanya ndo maana hata sasa hivi unakuwa na wasiwasi kwamba itakuwa sawa na kiapo chenu. Kwa hiyo usipotafuta solution utaendelea kuishi kwa wasiwasi na hutokuwa na mahusiano ya kudumu as you promised each other. Ni afadhali usiweke agano/ nadhiri kuliko kushindwa kuiondoa. Cha msingi msali kwa imani zenu na mtoe sadaka ya kuvunja agano lenu
 
usicheze na kitu kinachoitwa kiapo.kuna ndugu zangu wamekula kiapo kwa kutumia quran.walikuwa wanagombana na kupigana lakini walikuwa wanarudiana.kile kiapo kinawarudisha
 
Habari Jf,

Hapo katikati niliwahi kupost maswahibu yangu na mpenzi wangu wa zamani. Kuna kitu kinanitatiza sn naombeni mawazo yenu though i might sound weird.. Ni hivi wkt tupo kwenye mahaba motomoto na mpenzi wangu wa zamani tuliwahi kufanya kiapo cha damu.

Tulijikata vidole tukagusanisha damu huku tukisema maneno tukiachana tuharibikiwe and tusipate wapenzi wakudumu khaa! Najiona mjinga sn now je kuna madhara yoyote katika hilo au ni just imani za kijinga tu and if ni tatizo nifanyaje kuliondoa?

Msinitukane please wakati mwingine hua tunafanya mambo ya ajabu sana tunapokua tumekufa tumeoza.

Hiyo ni hatari sana. Mlichofanya kwenye ulimwengu wa roho kina madhara makubwa sana. Mmeunganishwa nafsi milele na milele. Hata ikotekea mmoja wenu labda akaoa, au kuolewa na mtu mwingine, atakuwa na wakati mgumu sana kwenye ndoa. Vilevile mtu unakuwa kwenye kifungo cha milele, yaweza kutokea usioe au kuolewa kabisa na kupata matatizo mengi Vilevile ni rahisNa ikitokea mmoja amefariki, nafsi yake itaendelea kutesekea milele.

Watu huvamia na majini, na kujikuta kwenye vifungo milele. Hatupaswi kufanya agano la damu. Damu ya YESU ndio agano tosha na hamna zaidi ya hapo. Nakushauri umpokee YESU kuwa Bwana na mokozi wa maisha yako kwanza, halafu waone watumishi wa Mungu waeleze nia yako ya kuvunja hilo agano la damu, uliliofanya. Ubarikiwe.
 
Habari Jf,

Hapo katikati niliwahi kupost maswahibu yangu na mpenzi wangu wa zamani. Kuna kitu kinanitatiza sn naombeni mawazo yenu though i might sound weird.. Ni hivi wkt tupo kwenye mahaba motomoto na mpenzi wangu wa zamani tuliwahi kufanya kiapo cha damu.

Tulijikata vidole tukagusanisha damu huku tukisema maneno tukiachana tuharibikiwe and tusipate wapenzi wakudumu khaa! Najiona mjinga sn now je kuna madhara yoyote katika hilo au ni just imani za kijinga tu and if ni tatizo nifanyaje kuliondoa?

Msinitukane please wakati mwingine hua tunafanya mambo ya ajabu sana tunapokua tumekufa tumeoza.

Ndugu hapa umefanya agano.hili jambo si la kufanyia mzaha.unacho takiwa ni kuongozwa sala ya toba na kumpokea Yesu kuwa bwana na mokozi wako.pili ni busara kuongea na huyo rafiki yako na kuvunja hilo Agano.tafadhali usifanye mzaha juu la hili swala maana unaweza kurudi hapa kama utalichukulia kimzaha mzaha.Nakutakia kila la kheri ndugu.
 
Pole sana. Hapo mlichoahid ndicho kitakachokuwa vinginevyo mkae pamoja mtakiane heri upya la sivyo kweli hamtapata hata kama mtapata bado ndoa zenu zitakuwa za shida yaani shida kweli na inaweza ikatafuna had vizaz vyenu vya 3. Wezenu huwa hawali kiapo kwenye mapenz maana mapenz ni sawa na uhai wakat wowote yaweza kufa na kuzikwa licha kupendana tena zaid ya sana.
nitarud nikusumulie yangu juu ya kiapo na mapenz kw ujumla nikirud baadae
usiache kurudi kusumilia nahitaji sn kusikia
 
Asanteni sn kwa mawazo yenu hasa ushauri wa kiimani mlionipa. Nitatubu na kuongea na wachungaji wanisaidie. Mbarikiwe sn
 
  • Thanks
Reactions: ram
Back
Top Bottom