AG Werema ataweza?

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,083
5,066
Wandugu,
nilikuwa nafuatilia mswaada wa madini ukijadiliwa na naona AG alishindwa kudhibiti ghadhabu na Mzee wa vijisenti alimfunika kabisa.
Ataweza kustahimili vishindo vya kina Slaa na wabunge wanaosoma nyaraka vizuri?Tujadili.
 
akaanza kulialia ''kazi hii ngumu sana'. Spika akaanza kumbembeleza kuwa kutunga sheria ni kazi ya kisiasa(nadhani aliamua kumturn down pale AG aliposema kwamba yeye ni professional'
 
Nashindwa kuelewa ni kwanini Chenge anatoa sana ushirikiano this tym. Lakini jana Mhe Sita aliwaonyesha kuwa serikali na bunge vyote vipo kwa ajili ya watz.

Najiuliza pale kulikuwa na uprofessional gani mpaka akawa vile. Ila alimalizwa haswa.
 
Amechangia nini huyo mzee wa vujisenti mbona aliharibu sana alipokuwa AG?

uko sahihi , mzee wa vijisenti aliharibu mambo mengi katika nafasi ya AG.
Chenge alikua shupavu katika kupambana uso kwa uso na wabunge machachari , iwe kwa hoja ama kwa namna yoyote.
Chenge anajua mambo mengi sana, kifupi anaweledi wa kutosha katika taaluma yake, lakini hakuwa mwadilifu, aliyokua anayafanya alikua anafanya makusudi kwa malengo ya kujinufaiusha yeye na genge lake.
Werema hamfikii Chenge hata kidogo linapokuja swala lakujenga hoja za kushawishi ndani ya bunge.
kielelezo ni jana, WEREMA NI KAMA MWANYIKA TU.
 
Amechangia nini huyo mzee wa vujisenti mbona aliharibu sana alipokuwa AG?

Mzee wa vijisenti ni mwerevu sana ukilinganisha na vingozi wengine ila tu ametumia werevu wake vibaya alipokuwa AG.
Uelewa na werevu wake umefanya viongozi wengine wamuogope. Ukisikiliza maongezi yake utabaini ni muelewa anayejiamini tofauti na wengine wengi.

AG wa sasa amekalia uprofessional wa kukariri zaidi kuliko common sense!

Tunachotakiwa kuelewa ni kwamba pamoja na elimu zetu za madarasani, kuna factors za asili zinazochangia performance ya mtu katika posts alipo. Kwa mfano watu wenye Phd wanashindwa na watu wenye Diploma ya kawaida tu.
 
Jana AG alikuwa mdogo kama pritoni ndo madhara ya kupeana peana madaraka.
Alihisi lile koti zito kama kabeba masarafu mifukoni, Bravo Cheyo aliweza kumbana kisawa sawa.
 
I was impressed by Chenge! The guy is good na spika knows the potentiality of Chenge ndo mana alimtumia sana! Werema nae tumpe mda! probably atakuwa safi! Kwa ujumla debate ya jana ilikuwa safi sana hasa pale 6 anapokuwa upande watz wenzake. I like that
 
I was impressed by Chenge! The guy is good na spika knows the potentiality of Chenge ndo mana alimtumia sana! Werema nae tumpe mda! probably atakuwa safi! Kwa ujumla debate ya jana ilikuwa safi sana hasa pale 6 anapokuwa upande watz wenzake. I like that

Chenge ni mzuri kwa mediocre wa third country kama Tanzania!
I wonder watu kama Chenge,Mramba,Mkono ,Karamagi,Rostam,Lowassa bado wanaserve bunge la Tanzania.

SHAME ON US
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom