Afya ya Rais Robert Mugabe(92) yazidi kuzorota

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,825
Reaction score
26,228
robert-mugabe-634235.jpg

Raisi Robert Mugabe wa Zimbabwe leo aliamuru ndege iliyokuwa ikimpeleka nchini Indonesia siku ya Ijumaa igeuzie Dubai na kurudi Harare mara moja.

Mzee Jongwe ambae ana umri wa miaka 92 ndiye raisi mzee kuliko maraisi wote wa barani Afrika, alikuwa akielekea nchini Singapore ambako mara nyingi huwa anakwenda kwa ajili ya kupata matibabu.

Raisi Mugabe aliondoka mapema nchini Swaziland siku ya jumanne na kuacha kikao cha SADC kikiendelea ambapo alianza safari yake ya barani Asia lakini ndege yake ikasimama kwa muda mjini Harare kabla ya kuruka kuelekea mjini Dubai nchini Saudi Arabia.

Maofisa wa raisi Mugabe wamekuwa wagumu kutoa sababu za kiongozi huyo kughairi safari yake ya Asia na kusimama mjini Dubai na baadae leo asubuhi kurudi mjini Harare.

Msemaji wa raisi bwana George Charamba alikanusha madai ya vyombo vya habari kwamba kiongozi huyo ana hali mbaya na kudai kwamba ikiwa hivyo serikali ingesema lakini hizo ni safari ambazo yeye raisi Mugabe alizipanga hapo kabla.

Baada ya kurejea jumamosi asubuhi mzee Jongwe aliwatania waandishi wa habari waliokuwa wakimsubiri kwa hamu kwa kuwaambia kwa kiingereza kwamba, "Yes, I was dead, its true I was dead. I resurrected as I always do. Once I get into my country I real", alisema mzee Jongwe mbele ya waandishi wa habari.

Kiongozi huyo alisema alikwenda Dubai kwa masuala ya kifamilia na alikwenda kumwona mmoja wa watoto wake ambae anamhofia, alisema bila kufafanua zaidi.

Raisi Mugabe hivi sasa serikali yake anayoiongoza inakabiliwa na upinzani wa wananchi ambao wamechoshwa na hali mbaya ya uchumi wa nchi hiyo na vitendo vya rushwa na ufisadi ambavyo vimekithiri katika kila idara ya serikali.

Kumekuwepo na maandamano ambayo yamepangwa na umoja wa vyama vya upinzani nchini humo na polisi walizuia maandamano siku ya Alhamisi iliyopita kwa wiki mbili.

Raisi Robert Mugabe ameitawala Zimbabwe tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1980 na wazimbawe hawajawahi kumwona raisi mwingine zaidi ya Mugabe ambae amepanga kugombea kiti hicho tena katika uchaguzi wa raisi mwaka 2018.

Mke wa raisi Mugabe Grace Mugabe amesema muwe wake ataongoza nchi hiyo kutokea kaburini.

Akihutubia mkutano wa hadhara leo jioni ambao uliandaliwa na umoja wa vijana wa ZANU-PF, raisi Mugabe amesisitiza kuwa serikali yake haitavumilia maandamano yanayofanywa na vyama vya siasa na kwamba chini ya utawala wake jambo hilo halitafanikiwa.

Mzee Mugabe aliendelea kuvituhumu baadhi ya vyombo vya nchi za magharibi na khasa Marekani kwamba ndivyo vilivyo nyuma ya maandamano na migomo mbalimbali nchini humo na kudai kuwa wanatumia pesa kuvirubuni vyama hivyo ili kuleta mitafaruku nchini humo na kuzorotesha hali ya kisiasa na kiuchumi kupitia vikwazo kadhaa vya kiuchumi.

Zimbabwe imekuwa katika matatizo ya kiuchumi kwa miongo kadhaa na pia kuwa nchi yenye asilimia 90 ya watu waso na ajira.

Serikali ya Zimbabwe kwa sasa haina hata uwezo wa kulipa mishahara watumishi wake wakiwemo polisi, na hata benki karibu zote nchini humo zinakabiliwa na uhaba wa fedha.

Ndani ya chama tawala tayari kuna mgawanyiko ambapo kuna kambi mbili zinazopimana ubavu kati ya kambi ya Emmerson Mnangagwa ambae ni makamu wa raisi na kambi ya Grace Mugabe mke wa raisi Mugabe.

Leo jioni mjini Harare kumekuwa na utulivu huku wananchi wakitafakari na kusikilizia habari yoyote ile inayosomwa katika redio na televisheni nchini humo na hali ya usalama ipo kama kawaida huku askari kanzu wa CID na wale wa ujasusi wa CIO wakiwa kama kawaida yao wamechanganyika na wananchi wakipiga story za hapa na pale na pia kushiriki maandamano.

Chanzo cha habari: vyombo mbalimbali vya habari duniani.

Nakumbuka wimbo wa Mlimani Park Orchestra na sauti ya mwimbaji Hassan Rehani Bichuka akisema , "Sura ya Zimbabwe inajionyesha Siasa za Mugabe zinazidi kung'ara"

Lakini hadi sasa Zimbambwe ina shida na Mugabe siasa zake zimeshindwa.

Je ikiwa Mugabe anaaga dunia ZANU-PF itaweza kuhimili nguvu ya wapinzani nchini humo au itatawala kwa nguvu?

Je kwa Mugabe kujitangaza kuwania tena uraisi mwaka 2018 anataka kumwachia kiti hicho mke wake au bwana Mnangagwa?

Je wapinzani wana nafasi yoyote ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2018?
 
Mkuu, Kichwa cha Habari na content haviendani. By the way, nimemwona Rais Mugabe kwenye TV na anaonekana mwenye Afya Kabisa. Long live Jongwe, Long live Mugabe.
 
Sawa, kwa hiyo wewe ndiyo ukaamua kuweka katika tafsiri ya kiswahili?

Dah! unahamu, mimi nilikuwa Mbabane na nilimwona Mugabe kwenye mkutano.

Ghafla akiwa mkutanoni akachomoka na kupanda ndege akiacha mkutano wa SADC ukiendelea, ikawa inasemwa mkulu alikuwa akiwahi Singapore, baadae nilipofuatilia hizi media reports nikaunganisha dots na ndio mzee umepata hiyo habari.
 
Hapo nimekuelewa mkuu.

Mzee Jongwe anajitahidi lakini anazidi kuishiwa nguvu, anajikakamua sana, ndio ukomredi huo.

Huyu ndie komredi khasa alibakia Afrika lakini hatoacha historia nzuri kwa watu wake.
 
Ndiyo, lakini hotuba zake zilizojaa ukweli zitakuja kufanyika darasa kwa vizazi vinavyokuja.

Kweli kabisa hii ndiyo historia halisi ya Africa's economic struggle before and after independence - case study Zimbabwe.

Walimu wa historia Afrika wana mchango mkubwa kwenye hii.
 
robert-mugabe-634235.jpg

Raisi Robert Mugabe wa Zimbabwe leo aliamuru ndege iliyokuwa ikimpeleka nchini Indonesia siku ya Ijumaa igeuzie Dubai na kurudi Harare mara moja.

Mzee Jongwe ambae ana umri wa miaka 92 ndiye raisi mzee kuliko maraisi wote wa barani Afrika, alikuwa akielekea nchini Singapore ambako mara nyingi huwa anakwenda kwa ajili ya kupata matibabu.

Raisi Mugabe aliondoka mapema nchini Swaziland siku ya jumanne na kuacha kikao cha SADC kikiendelea ambapo alianza safari yake ya barani Asia lakini ndege yake ikasimama kwa muda mjini Harare kabla ya kuruka kuelekea mjini Dubai nchini Saudi Arabia.

Maofisa wa raisi Mugabe wamekuwa wagumu kutoa sababu za kiongozi huyo kughairi safari yake ya Asia na kusimama mjini Dubai na baadae leo asubuhi kurudi mjini Harare.

Msemaji wa raisi bwana George Charamba alikanusha madai ya vyombo vya habari kwamba kiongozi huyo ana hali mbaya na kudai kwamba ikiwa hivyo serikali ingesema lakini hizo ni safari ambazo yeye raisi Mugabe alizipanga hapo kabla.

Baada ya kurejea jumamosi asubuhi mzee Jongwe aliwatania waandishi wa habari waliokuwa wakimsubiri kwa hamu kwa kuwaambia kwa kiingereza kwamba, "Yes, I was dead, its true I was dead. I resurrected as I always do. Once I get into my country I real", alisema mzee Jongwe mbele ya waandishi wa habari.

Kiongozi huyo alisema alikwenda Dubai kwa masuala ya kifamilia na alikwenda kumwona mmoja wa watoto wake ambae anamhofia, alisema bila kufafanua zaidi.

Raisi Mugabe hivi sasa serikali yake anayoiongoza inakabiliwa na upinzani wa wananchi ambao wamechoshwa na hali mbaya ya uchumi wa nchi hiyo na vitendo vya rushwa na ufisadi ambavyo vimekithiri katika kila idara ya serikali.

Kumekuwepo na maandamano ambayo yamepangwa na umoja wa vyama vya upinzani nchini humo na polisi walizuia maandamano siku ya Alhamisi iliyopita kwa wiki mbili.

Raisi Robert Mugabe ameitawala Zimbabwe tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1980 na wazimbawe hawajawahi kumwona raisi mwingine zaidi ya Mugabe ambae amepanga kugombea kiti hicho tena katika uchaguzi wa raisi mwaka 2018.

Mke wa raisi Mugabe Grace Mugabe amesema muwe wake ataongoza nchi hiyo kutokea kaburini.

Akihutubia mkutano wa hadhara leo jioni ambao uliandaliwa na umoja wa vijana wa ZANU-PF, raisi Mugabe amesisitiza kuwa serikali yake haitavumilia maandamano yanayofanywa na vyama vya siasa na kwamba chini ya utawala wake jambo hilo halitafanikiwa.

Mzee Mugabe aliendelea kuvituhumu baadhi ya vyombo vya nchi za magharibi na khasa Marekani kwamba ndivyo vilivyo nyuma ya maandamano na migomo mbalimbali nchini humo na kudai kuwa wanatumia pesa kuvirubuni vyama hivyo ili kuleta mitafaruku nchini humo na kuzorotesha hali ya kisiasa na kiuchumi kupitia vikwazo kadhaa vya kiuchumi.

Zimbabwe imekuwa katika matatizo ya kiuchumi kwa miongo kadhaa na pia kuwa nchi yenye asilimia 90 ya watu waso na ajira.

Serikali ya Zimbabwe kwa sasa haina hata uwezo wa kulipa mishahara watumishi wake wakiwemo polisi, na hata benki karibu zote nchini humo zinakabiliwa na uhaba wa fedha.

Ndani ya chama tawala tayari kuna mgawanyiko ambapo kuna kambi mbili zinazopimana ubavu kati ya kambi ya Emmerson Mnangagwa ambae ni makamu wa raisi na kambi ya Grace Mugabe mke wa raisi Mugabe.

Leo jioni mjini Harare kumekuwa na utulivu huku wananchi wakitafakari na kusikilizia habari yoyote ile inayosomwa katika redio na televisheni nchini humo na hali ya usalama ipo kama kawaida huku askari kanzu wa CID na wale wa ujasusi wa CIO wakiwa kama kawaida yao wamechanganyika na wananchi wakipiga story za hapa na pale na pia kushiriki maandamano.

Chanzo cha habari: vyombo mbalimbali vya habari duniani.

Nakumbuka wimbo wa Mlimani Park Orchestra na sauti ya mwimbaji Hassan Rehani Bichuka akisema , "Sura ya Zimbabwe inajionyesha Siasa za Mugabe zinazidi kung'ara"

Lakini hadi sasa Zimbambwe ina shida na Mugabe siasa zake zimeshindwa.

Je ikiwa Mugabe anaaga dunia ZANU-PF itaweza kuhimili nguvu ya wapinzani nchini humo au itatawala kwa nguvu?

Je kwa Mugabe kujitangaza kuwanai tena uraisi mwaka 2018 anataka kumwachia kiti hicho mke wake au bwana Mnangagwa?

Je wapinzani wana nafasi yoyote ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2018?

!
!
kwa umri kama huu maradhi sio habari. Apumzike tu mzee
 
Hii ni habari kwa kuwa wale wote wanaohisi wamenyanyaswa na mzee Mugabe hawaeshi wakifuatilia kila upepo uvumao.

Wewe fikiria watu pale Harare kuona ndege na raisi iliyokuwa ikielekea Jakarta mara imekuwa diverted na kwenda Dubai halafu mara imetua Harare walishangaa sana hasa waongoza ndege.
 
kwa umri wa huyu bwana nadhani mtoto wake wa kwanza anatakiwa awe amestaafu pia.
 
Mtoto wake wa kwanza kwa mke wa kwanza (alifariki mwaka 1992) ambae ni marehemu leo angekuwa na umri wa miaka 53.

Watoto wa mke wa sasa aliowapa na mama Grace bado wadogo kisiasa, wa kwanza anaitwa Bona Mugabe- Chikore ana miaka 24

upload_2016-9-4_0-42-41.png

Bona akiwa na baba yake Robert na mama Grace Mugabe

Halafu kuna wavulana wawili Robert Peter Mugabe Junior na Chatunga Bellarmine Mugabe

robert-mugabe-junior.jpg

Junior akiwa na baba yake

chatunga.jpg

Chatunga ana miaka 19 ndie mtundu na msumbufu na amefanana khasa na baba yake.

Kwa taarifa za mpaka mwaka huu kuhusu utajiri wa Mugabe zinasema ana utajiri wa kiasi cha Dola za kimarekani milioni 10 ambazo zipo benki moja ya nje.
 
Mzee Jongwe anajitahidi lakini anazidi kuishiwa nguvu, anajikakamua sana, ndio ukomredi huo.

Huyu ndie komredi khasa alibakia Afrika lakini hatoacha historia nzuri kwa watu wake.
Anafahamu umri wa dunia huyu kiongozi? Anafahamu kwamba yeye hawezi kufikisha 105 au 110?
Anajitesa bure tu, awaachie wengine wafanye wanachotaka kufanya.
Amefanya kile alichotaka kufanya au anataka yale ya Rais wa Uzbekistani? Umauti umkute akiwe Rais wa kulazimisha?
Dunia hii ina vituko kweli.
 
Kumbe anahela nyingi hivyo?Unaweza kutupa source??

Mwanae Bona alikuwa akisoma Uingereza akilipiwa shule maalum sikumbuki figure ya ile shule maana ni pesa nyingi tu.

Huyu Robert Junior ambae baba yake ndio alikwenda Dubai kumjulia hali anasoma American University in Dubai AUD na ni chuo khasa, na mzee jongwe analipia.

Na huyu wa mwisho Chatunga ambae ni mtundu sana anasoma chuo cha private kipo Harare chaitwa St Georges College.

Hivyo hii inaweza kukupa mwanga khasa kuhusu hawa wanaolipiwa huko nje maana ni dola tu.
 
"Kwa taarifa za mpaka mwaka huu kuhusu utajiri wa Mugabe zinasema ana utajiri wa kiasi cha Dola za kimarekani milioni 10 ambazo zipo benki moja ya nje."

Million 10 tu wakati ameshikilia Zimbabwe for 36yrs?...Mh!

Labuda.
 
Jamaa ni mzalendo sana, nakuunga mkono!
 
Back
Top Bottom