Afya ya Dr. Ulimboka Yaimarika, Kutua Nchini August

Afya ya Dr. Ulimboka Yaimarika, Kutua Nchini August

Asante mkuu kwa taarifa.
Je Dr. Uli anafahamu kuwa mmoja wa waliomteka ameshatubu kwa Gwajima/Kova?
Je, Dr. Uli anafahamu kwamba alitekwa na kichaa?


Huu ni Ushindi mwingine katika demokrasia ya nchi yetu!!
 
Tetesi kwamba hali ya afya ya mpambanaji Komredi ulimboka na taarifa za kurejea mwezi ujao August, ni ishara kwamba watanzania wapo mbioni kuvunja rekodi ya mapokezi uwanja wa ndege. taarifa za chini ya kapeti ni kwamba wanaharakati na wadau mbalimbali wamepania kutumia nafasi hii kuwasilisha ujumbe wa ushindi wa nguvu ya umma dhidi ya utawala wa mabavu na udhalilishaji. katika historia ya nchi hii, binadamu anayeongoza kwa kupata mapokezi makubwa ni Pope John Paul II, Nelson Mandela, Mwisho Mwampamba na sasa itakuwa zamu ya Dr. Ulimboka kuvunja rekodi.
Watanzania tunamwombea apone haraka na tunamsubiri kwa hamu tumpe mapokezi ya kihistoria kwa maandamano.

Solidarity 4eva, Ushindi dhidi ya utawala wa kiimla na mabavu!
 
natamani ningekuwa dar siku hiyo.tunamtakia mapokezi mema dr.hofu yangu ni chama cha mabwepande kisije kikafanya hujuma zaidi kabla hata hajatua bongo.
 
Policcm hawatoruhusu!!! Wanasema serikali itatukanwa sana na wasio na nidhamu.
 
Tunaliongelea kama jambo la kawaida lakini sio jambo dogo hata kidogo Ulimboka kurudi mzima wa afya na kusema wazi kilichofanyika, tukae tukijua wazi kwamba hiyo itakuwa a huge step back kwa serikali hii ya kifedhuli. Hawataikubali hii hali kirahisi na ni rahisi sana serikali kuamua lolote ( liwalo na liwe ) ilimradi Dr. Ulimboka asipate uwezo wa kusema wazi kilichotokea. Binafsi namuombea Mungu Dr. Ulimboka arudi salama na kusema kila kitu kilichotokea maana Mungu ana uwezo wa kufanya hilo litokee, hata hivyo pamoja na kuombea hilo ni muhimu kuwa na mikakati mikali sana ya kuhakikisha Dr. Ulimboka yuko salama. Ijulikane wazi kwamba kitendo cha Dr. Ulimboka kurudi na kutaka kusema ukweli ni vita ya moja kwa moja itakayowaaibisha watawala na kuthibitisha uovu mwingi ambao serikali hii ya kifedhuli imekuwa ikijaribu kuiaminisha jamii kwamba ni uovu wa kufikirika ama kwa sehemu kubwa uovu wa kusingiziwa. Mwisho naamini hata kama Dr. Ulimboka hatarudi, ama kama atarudi ikashindikana kusema kilichotokea.., sisi tunaelewa wazi kilichotokea na hili nalo limeongeza kasi na chachu ya ukombozi wa nchi hii. Tunamuombea sana Dr. Ulimboka kokote aliko na tunawaombea sana Madaktari wote waendelee kuwa chachu ya ukombozi wa Taifa hili, siku zote nuru hushinda giza.., itafika mahala harakati zitaizidi nguvu serikali yetu ya kifedhuli na watasalimu amri aidha kwa kupenda ama kwa kutokupenda.
 
Najuwa wewe ni mtani wangu,
la sivyo ningekujibu.

Asante mkuu kwa taarifa.
Je Dr. Uli anafahamu kuwa mmoja wa waliomteka ameshatubu kwa Gwajima/Kova?
Je, Dr. Uli anafahamu kwamba alitekwa na kichaa?
 
km nitakua nje ya dar,nitahakikisha narudi fasta ........alluta continua
 
Get well soon Dr. Ulimboka

Hii habri iatawafanya ACP, Msangi, Abeid, Kova, Jack Zoka, IGP Said Mwema(SIC!), Liwalo na liwe na wapaganji wa Magogoni washindwe kupata usingizi, Itabidi wameze pilton kwa sana.

Nami nashauri Dr. Ulimboka afanye series of interview kabla ya kurejea nchini na kuziweka kwenye ytube. Hii itasaidia kuondoa motive ya kumdhuru because the truth will be out.
 
Daktari wetu mpendwa Mungu akubariki upone haraka , mimi nadhani hata usipokuja kutueleza tunajua kilichojiri , Haya majitu ni mauaji hiyo si siri tena , usalama wa Taifa ni wauaji ukae utambue hilo kwa hiyo katafute hifadhi pahala salama muda si mrefu utawala wa kishetani utaisha ndipo urudi home , la sivyo wanaosema aliyekujeruhi ni kichaa, bado kuna vicha wengi watatumwa wakumalize. Haraka ya nini kurudi kwenye nchi ya laana
 
Mungu ni mkubwa, aliyehusika natamani naye ang'olewe meno bila Ganzi:israel:

Una Huruma sana wewe...mimi natamani ang'olewe kichwa, na moyo bila ganzi, nimechagua viwili hivyo kwa sababu kwake mtu huyo havina kazi, wala havina maana kuwa navyo.
 
Una Huruma sana wewe...mimi natamani ang'olewe kichwa, na moyo bila ganzi, nimechagua viwili hivyo kwa sababu kwake mtu huyo havina kazi, wala havina maana kuwa navyo.

Kuna taarifa kwamba watu wa Usalama wa Taifa wamemwita Mengi kwamba asirushe hotuba ya Ulimboka siku akirejea maana inajenga chuki zisizo na maana TBC wao hilo wanalifahamu mda mrefu hawatarusha
 
Wakati watanzania wanaombea Dr Uli apone haraka arudi kujenga taifa kuna ambao wanatamani hata agongwe na gari ili mradi asirudi bongo. Hawa ni Kova, Hemed Msangi, Said Mwema, Jack Zoka na jamaa wa baraza la waislam la bahakita

They are all pitiful little demons; dr. Ulli may come to pass on as we all will anyway! but he has made his mark and with his passing he shall have left a legacy one can be proud of, He endured pain and suffering NOT for personal gain but so fellow Tanzanians could get better medical services, Every revolution demands sacrifices; be it scientific, social, industrial and what have you! Ulli you bore the brunt of that sacrifice! We are proud of you Dr. Ulli; your blood will go a long way to nourish the momentum of agitation for a better Tanzania.
 
Aibu yao aibu yetu...tukisema vilaza ndio wako kwenye usukani tena hawajui wanalofanya tutakuwa tumekosea?
 
Back
Top Bottom