Afya sambamba na uchumi

Sweveboy_tz

New Member
Jul 14, 2021
2
4
20210714_135210.jpg


Afya sambamba na uchumi

Changamoto kubwa sana inayotukabiri sisi wa Tanzania pamoja na mataifa mengine yanayoendelea ,ni kwamba tunashindwa kutambua ni jinsi gani afya za wananchi zinaathiri moja kwa moja Uchumi wa Taifa.

Iwapo wananchi watakuwa na afya njema basi hata kasi ya kupanda kwa uchumi itakuwa juu. Hivyo Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuhakikisha Sekta ya afya inaboreshwa kwa hali na Mali katika jamii Yoyote yenye kutaka maendeleo,ususani maendeleo ya kiuchumi .tukiangalia mataifa yaliyo endelea kama USA watu wamekuwa na Life expectancy (muda wa kuishi) kubwa kuliko mataifa yanayo endelea mfano marekani life expectancy ni miaka 77.8 tofauti na Tanzania ambayo life expentancy ni miaka 65.02 .ni vema kila taifa kutambua kwamba .watu ndio nguvu kazi ya taifa. Watu wakiwa na afya bora basi ni rahisi kwa taifa kuendelea. Kwani uchumi unaenda sambamba na nguvu kazi.

Je ni kwa vipi Serikali inaweza kuboresha sekta ya afya? Kitu cha kwanza ni kuthamini vitu vya ndani, hapa inapaswa kuangalia sana sekta ya madawa .nchi nyingi zinazoendelea zimekuwa zikitegemea madawa kutoka nje ya Nchi jambo ambalo ,limekuwa likikandamiza uchumi wa mataifa mengi na kupelekea madeni katika Nchi. Kutokana na dawa hizo .Ambazo kwa upande wa pili mitishamba na wadudu Mbali Mbali ambao wapo ndani ya Nchi yetu wanaweza kuzalisha dawa hizo. Mfano asali ,aloevera na mdalasini

Tiba asilia inatumiwa na wananchi wengi. Takribani asilimia sitini ya wananchi huanza kutumia tiba asilia wanapopatwa na maradhi kabla ya kwenda vituo vya kutolea huduma za afya. Aidha, hivi karibuni tiba mbadala imepata umaarufu miongoni mwa wananchi kutokana na uimarikaji wake duniani.

Kadhalika, wagonjwa hutoka hospitalini na kwenda kutafuta tiba asilia au kutumia aina zote za tiba kwa pamoja. Vilele, takwimu zinaonyesha kwamba bado kuna wanawake wajawazito wanaojifungulia nyumbani kwa kusaidiwa na wakunga wa jadi. Pamoja na huduma hizi kutumiwa na wananchi wengi, uratibu wa uendeshaji wake unahitaji kuimarishwa.na serikali ya Tanzania Kuendeleza, kuratibu na kuboresha utoaji wa huduma za tiba asilia, mbadala
20210714_135304.jpg

ASALI ITOKANAYO NA NYUKI

20210714_135322.jpg

Aloe vera
20210714_135246.jpg

Mdalasini

Mimea iliyo orodheshwa katika picha hapo ni miongoni mwa mimea michache inayotibu magonjwa Mbalimbali.ya binadamu .iwapo serikali itaweka nguvu kubwa kuwasaidia wavumbuzi wa dawa .waliomo ndani ya Nchi yetu kwa njia Yoyote ile ikiwemo fedha pamoja na mazingira wezeshi katika utengenezaji wa dawa ,basi watapelekea maendeleo makubwa katika Nchi. Pia itaongeza kipato katika Nchi iwapo dawa hizo pia zitauzwa nnje ya nchi.pia itawawezesha watanzania wengi kupata madawa Mbali Mbali yatakayo kubolesha afya zao kwa bei ndogo kabisa jambo litakalo punguza vifo visivyo vya lazima nchini.

Pia serikali inatakiwa kuendelea na zoezi la kutoa elimu kwa wananchi kwa njia tofauti tofauti.jambo litakalo wapelekea wananchi kujilinda na magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika .kwa njia Mbalimbali ikiwemo njia salama za maisha kuepuka matumizi mabaya ya vyakula, vilevi kama sigala pamoja na pombe kali .pia hata vinjwaji vya viwandani ambavyo vimekuwa vikipelekea watu kusumbuliwa na maradhi ya figo .elimu kwa watanzania wote itapunguza pia kazi ya watu kupata magonjwa .jambo ambalo litawafanya watu wote kufanya kazi na kupelekea uchumi kukua.

Ifahamike kuwa watu wakiishi katika hali ya usalama .ususani katika afya zao basi kutakuwa na nguvu kazi ya kutosha kukuza uchumi wa taifa .msingi wa kila kitu ni afya .tukiangalia mataifa mengi ya dunia yakiathirika kwenye afya kwa wananchi wake basi hata hali yake ya uchumi pia huzolota.mfano janga la COVID 19 limepelekea mataifa mengi kupoteza nguvu kazi (watu) jambo ambalo limepelekea mataifa hayo kuanguka kiuchumi kwa kasi .huo ni mfano tu ambao unaonesha ni kwa jinsi gani afya inaweza kuathiri uchumi . Taifa lolote lenye hali nzuri ya kiuchumi basi ni taifa imara sana katika sekta ya afya.

Basi serikali ya Tanzania inatakiwa pia kuhakikisha upatikanaji wa madawa ambayo hayapatikani ndani ya Nchi yetu .pamoja na vifaa tiba vinapatikana kwa urahisi zaidi katika Nchi yetu .hii itawezekana kama wataalamu wa dawa pia watatengenezewa mazingira bora ya kuuza dawa mfano pharmacy

20210714_135232.jpg


Hivyo ni vema sana serikali yetu kutambua kuwa mabadiliko makubwa sana yakifanywa katika sekta ya afya.basi hii itapelekea Athari njema sana katika uchumi wa taifa letu.hivyo basi wananchi pia tunapaswa kuhakikisha pia tunashirikiana bega kwa bega na serikali yetu kukuza sekta ya afya .kwa njia tofauti tofauti ikiwemo kutunza afya zetu .kwakuzingatia taratibu zilizowekwa na taasisi yetu ya afya.pia kuhakisha tunalipa kodi serikalini.

Pia serikali inatakiwa Kuongeza bajeti ya sekta ya afya kila mwaka, ili kukidhi mahitaji muhimu ya afya kwa wananchi wake. Ili, nyongeza hiyo Iweze kukidhi mahitaji halisi ya kutolea huduma za afya, kwa sababu ya kuongezeka kwa gharama za kukinga na kutibu magonjwa mbalimbali kutokana na mabadiliko ya teknolojia na mfumuko wa bei.

Vilevile, kuna uhaba mkubwa wa vitendea kazi na vile vilivyopo, vingi ni chakavu, havina matengenezo na vimepitwa na teknolojia ya kisasa.

Pia Serikali inatakiwa kuongeza viwango vya ubora katika utoaji wa huduma za afya. Hata hivyo, huduma za afya hapa nchini hazijafikia viwango vinavyotakiwa. Aidha,kuna upungufu wa wataalam katika ngazi zote, uchakavu wa majengo,upungufu wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendea kazi. Vilevile, mazingira ya kufanyia kazi.

Pia serikali inatakiwa kupinga ongezeko la biashara huria na utandawazi ambalo linachochea kuwepo kwa bidhaa nyingi za vyakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi nchini.

Hali hii ni changamoto kwa Serikali katika kulinda afya za watumiaji dhidi ya madhara yatokanayo na matumizi ya bidhaa hizo. Aidha, uwepo wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba bandia na visivyofikia viwango vilivyowekwa vya ubora na usalama ni changamoto nyingine inayohitaji mfumo thabiti wa udhibiti. Kwa kutambua hali hiyo, Serikali ilianzisha Mamlaka ya Chakula na Dawa kwa Sheria namba 1 ya mwaka 2003.

Lakini Bado nguvu kubwa inahitajika kupinga vitu hivyo Na hizi ni njia za moja kwa moja Ambazo kama serikali ikizingatia itapelekea mabadiliko makubwa sana kiuchumi katika taifa letu la Tanzania,

1) Kupunguza magonjwa na vifo, ili kuongeza umri wa kuishi wa watanzania wote kwa kutoa huduma bora za afya, pamoja na kuzingatia mahitaji ya makundi maalum, hususan; watoto wachanga na walio chini ya umri wa miaka mitano, watoto walio katika umri wa kuanza shule na walio shuleni, vijana, watu wenye ulemavu, wanawake walio katika umri wa uzazi na wazee.

(2) Kuhakikisha kuwa huduma za afya ya msingi zinapatikana na kutolewa na mfumo madhubuti na kushirikisha jamii, kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo.

(3) Kukinga na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na yale yasiyo ya kuambukiza, hususan; Virusi vya UKIMWI na UKIMWI, Malaria, Kifua Kikuu, magonjwa yatokanayo na lishe duni, afya ya mazingira, na sehemu za kazini na usimamizi wa kemikali.

(4) Kuhamasisha wananchi kuhusu maradhi yanayoweza kuzuilika, ili waweze kuyatambua na kutafuta mbinu za kuyadhibiti.

(5) Kumuelimisha kila mwananchi, aelewe kuwa anawajibika moja kwa na afya yake

Pia miongoni mwa faida kuu Ambazo taifa letu linaweza kupata kutokana na afya bora kwa kila mwananchi ni kukukua kwa uchumi.hivyo maendeleo ya kiuchumi yamebebwa na afya za wananchi.
 
Back
Top Bottom