Afya ndio mtaji Mkuu

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Afya nzuri ni Mtu kuwa sawa kiuchumi, Kisiasa, Kijamii, Kiroho pasipo kuwa na Magonjwa yoyote yale yanayomsumbua. Katika Maisha ya Kila siku ya mwanadamu Afya ndio Mtaji wa kwanza halafu mengine yanafwata.

Bila Afya nzuri hakuna uzalishaji wowote ule, bila afya nzuri Uchumi unadorora Mwl Nyerere aliwahi Kusema Ujinga Umaskini & Maradhi ni Vitu vya Kuvikataa kwa hali yoyote ile. Wananchi wanahitaji Kupata Huduma bora za Afya kutoka kwenye Serikali zao tena kwa Gharama nafuu Tujiulize JE, SERIKALI YETU KWA HAPA IMETIMIZA WAJIBU WAKE? Kwa mlengo wangu Ni YES ya asilimia 77% na tutafika.

Mabadiliko ya Mfumo wa Maisha yamechangia sana Kuibuka kwa maradhi mengi Kisukari, Shinikizo la damu, Kiharusi, Malaria, Uti, Magonjwa ya Zinaa (Kisonono, Kaswende, Hiv/aids) etc. Pia watu kutokua na Tabia za kuangalia afya zao mara kwa mara,Watu Kupuuzia Shauri za watalaamu pamoja na Uharibifu wa Mazingira.

Kuuguza ni Gharama kwa nchi za wenzetu hakuna maradhi wanaogopa kama Kiharusi/Stroke hapa mgonjwa anaweza kukaa hata Miaka zaidi ya Kumi akiwa kitandani ni lazima familia kujipanga na ni Ugonjwa unaozuirika kwa kufwata kanuni za Kiafya.

Hivyo basi pamoja na ubize wa Maisha tusisahau kuwekeza katika afya zetu kwa kuchukua tahadhari muhimu.
 
Karibu sana Kiongozi nafikiri Kupima pressure hospitali Nyingi ni Bure unaweza toka hata misele ukapitia ukamwomba Mtaalamu akupime ni dakika 5 tu.

Tuwe na Tabia pia ya kupima Sukari mara kwa mara ni Kipimo cha dk 2 tu hata buku 5 haizidi.
 
Karibu sana Kiongozi..nafikiri Kupima pressure hospitali Nyingi ni Bure unaweza toka hata misele ukapitia ukamwomba Mtaalamu akupime ni dakika 5 tu.
Tuwe na Tabia pia ya kupima Sukari mara kwa mara ni Kipimo cha dk 2 tu hata buku 5 haizidi.
Kweli mkuu
 
Back
Top Bottom