Afya na ukuaji wa mtoto genius

Tzania

Member
Jul 23, 2019
31
12
Wakuu nahitaji kulisha ubongo wa kabinti kangu ambako kana takribani miaka mitano ila nahitaji kawe genius school na nyumbani pia.

Hebu nipeni muongozo kwa wataalamu wa haya mambo vyakula gani ambavyo vinamjenga kiakili mtoto na shule ipi bora ambayo itamjenga huyu binti katika misingi ya lugha tatu English, French na Kireno au Kispain na Kiarabu.

Karibuni kwa mawazo na ideas zenu wakuu.
 
Mpeleke shule nzuri mkuu, hutajuta. Pia hili wazo ulitakiwa ulifikirie wakati mama yake ni mjamzito. Masharti yanaanziaga huko. Hayo mawazo mnayo wote wazazi wawili au ni lako. Kama ni la kwako tu ni ngumu kufanikiwa pia.

Wakati Samsoni yule mwenye nguvu anatabiriwa kuzaliwa ,mama yake aliambiwa hivi
Waamuzi13:3 Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume.

4 Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi
 
Dawa nzuri ni kumkeep busy kujifunza yale unayoyataka(kupitia shule nzuri na malezi ya nyumbani).

Ubongo wa mtoto ni kama computer au smart phone, ufanyaji wake kazi unategemea sana installation apps, ukichelewa tu kumuwekea proper apps, basi atajiwekea za kwake au atawekewa na ulimwengu, hivyo apps zako zitagonga mwamba.

Angalizo muhimu.
- Hakikisha mtoto anakuwa na afya njema ya kimwili(Hardware) ili hayo maarifa(software) zipate mahali pa kukaa.

- Muweke mbali kabisa na utamaduni wa kupendelea kuangalia Video/Tv, kucheza game ama kuwa mshabiki wa miziki ya kizazi kipya, badala yake mjengee utamaduni wa kusoma vitabu. ('Genius' wote ni wapenzi wakubwa wa kusoma vitabu)
 
Hiv nini maana ya genius? Isiwe tunajadili jambo tofauti na dhana yake. Majibu initakayopata ndio yatanipa mwongozo wa kuchangia.
 
Back
Top Bottom