Fahamu Umuhimu wa Madini Joto kwa Mama na Mtoto

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
VYAKULA VYA MADINI (CHUMA)IRON KWA WATOTO

Vyakula vyenye madini ya iron ni muhimu sana kwa ukuaji wa mtoto. Vyakula vya madini ya iron husaidia mtoto asipatwe na anemia.vyakula vya madini ya iron husaidia pia ukuaji wa ubongo wa mtoto, hivyo humfanya mtoto awe na kumbukumbu nzuri. Mtoto pia anahitaji vyakula vya iron ili aweze kujifunza vitu vipya kama kuongea na kutembea. Ni muhimu mtoto akapata vyakula vya madini chuma kila siku.

Dalili ya mtoto mwenye ukosefu wa madini chuma.

Kukosa hamu ya kula,ngozi inakosa nuru, uzito kupungua au kutoongezeka.

VYAKULA VYA MADINI YA IRON(CHUMA)

Maziwa ya mama
Samaki
Viazi vitamu
Dark Green Vegetables (Brocoli, Spinach, Green Bean)
Kuku
Nyama
Kiini cha Yai
Njegere
Maini
Green beans.
Parachichi

Mama Mzazi mlezi epuka kumpa mtoto chai au maziwa ys ngombe kwa kiwango kikubwa kwani vitu hivyo vinasababisha upungufu wa madini ya chuma mwilini. Mtoto kuanzia mwaka apewe maziwa ya ngombe vikombe 2 kwa siku. Epuka kumpa maziwa ya ngombe kwa kiwango kikubwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom