Virutubisho muhimu kwa ukuaji Bora wa Ubongo wa Mtoto

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Tangu kutungwa kwa ujauzito hadi kuzaliwa, mwili wa mtoto huhitaji kuwezeshwa kwa virutubisho muhimu ili ukuaji bora wa afya ya mwili na akili uweze kufanikiwa.

Kwa mujibu wa tafiti, Ubongo wa mtoto hufikia 80% ya uzito wa ubongo wa mtu mzima akiwa na umri wa miaka 2 pekee. Hii inamaanisha kuwa msingi mwema wa makuzi ya kiakili, pamoja na mambo mengine hutegemea aina ya lishe anayopatiwa mtoto.

Vyakula hivi vinaweza kutoa mchango mkubwa katika kuboresha makuzi ya ubongo wa mtoto;
  • Samaki na vyakula vingine vya baharini, huwa na asidi ya mafuta ya Omega 3, zinc na Madini joto ambayo huboresha afya ya ubongo.
  • Mboga za majani, huwa na viondoa sumu, asidi ya foliki pamoja na Vitamini E. Ni virutubisho muhimu katika kuulinda ubongo.
  • Matunda hasa machungwa, huwa na kampaundi za hesperidin na narirutin zilizothibitishwa na tafiti za afya kuwa na uwezo wa kuongeza msukumo wa damu kwenye ubongo na kuboresha utambuzi wa mambo.
  • Vyakula jamii ya Karanga, huwa na Zinc, Vitamini E, asidi ya foliki na protini. Vyote hufaa katika ukuaji na utendaji kazi wa Ubongo.
Katika mpangilio wa mlo unaompatia mwanao kila siku, hakikisha unazingatia kuongeza baadhi ya virutubisho hivi ili umsaidie akue akiwa na afya bora ya mwili na akili.

Chanzo: Healthline
 
Mada kama hizi hazipati watu wengi.

Kwa sababu hatuwekei umuhimu haya mambo.

Na kutowekea umuhimu mambo haya kunaigharimu sana jamii yetu.

Ndiyo maana unakuta jitu lina Ph.D ya kemia lakini ni mtu mzima ovyo.

Kumbe utotoni lilikosa virutubisho muhimu vya kukuza ubongo vizuri.
 
Aiseee!!!
 
Tangu kutungwa kwa ujauzito hadi kuzaliwa, mwili wa mtoto huhitaji kuwezeshwa kwa virutubisho muhimu ili ukuaji bora wa afya ya mwili na akili uweze kufanikiwa.

Kwa mujibu wa tafiti, Ubongo wa mtoto hufikia 80% ya uzito wa ubongo wa mtu mzima akiwa na umri wa miaka 2 pekee. Hii inamaanisha kuwa msingi mwema wa makuzi ya kiakili, pamoja na mambo mengine hutegemea aina ya lishe anayopatiwa mtoto.

Vyakula hivi vinaweza kutoa mchango mkubwa katika kuboresha makuzi ya ubongo wa mtoto;
  • Samaki na vyakula vingine vya baharini, huwa na asidi ya mafuta ya Omega 3, zinc na Madini joto ambayo huboresha afya ya ubongo.
  • Mboga za majani, huwa na viondoa sumu, asidi ya foliki pamoja na Vitamini E. Ni virutubisho muhimu katika kuulinda ubongo.
  • Matunda hasa machungwa, huwa na kampaundi za hesperidin na narirutin zilizothibitishwa na tafiti za afya kuwa na uwezo wa kuongeza msukumo wa damu kwenye ubongo na kuboresha utambuzi wa mambo.
  • Vyakula jamii ya Karanga, huwa na Zinc, Vitamini E, asidi ya foliki na protini. Vyote hufaa katika ukuaji na utendaji kazi wa Ubongo.
Katika mpangilio wa mlo unaompatia mwanao kila siku, hakikisha unazingatia kuongeza baadhi ya virutubisho hivi ili umsaidie akue akiwa na afya bora ya mwili na akili.

Chanzo: Healthline
Umeongelea kwa watoto je kwa watu wazima inakuwajee
 
Back
Top Bottom