Afungiwa nyumbani kwa miaka 30

Afungiwa nyumbani kwa miaka 30

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Polisi nchini Ujerumani wanawachunguza mume na mke ambao wanadaiwa kumfungia mwanao wa kiume ndani ya nyumba kwa miaka 30, katika jimbo la Bavaria

Mwanamme huyo wa miaka 43 hajawahi kuonekana hadharani tangu kuacha shule akiwa na miaka 13. Polisi wamesema japo mwanamme huyo yuko shwari kiafya, hata hivyo ameonekana kuwa na mfadhaiko.

Hata hivyo wamesema hawatawasilisha mashtaka yeyote. Polisi walijulishwa kuhusu tukio hilo na jirani ya mtu huyo ambapo walimchukua kutoka nyumba alikoishi na kumpeleka hospitalini.

Hata hivyo walikabiliwa na wakati mgumu kumshawishi bwana yule kupelekwa hospitailini. Mamake amesema mwanawe huyo hakufungiwa na kwamba ni yeye binafsi aliyekataa kwenda shule na kuamua kusalia ndani ya nyumba kwa miaka 30.

Maafisa wa hospitali alikolazwa wanajaribu kumfanyia uchunguzi wa kiakili. Wengi wanahoji kuhusu jinsi mtu huyo aliepuka ushawishi wa mitandao, ujana, huduma za kijamii na zile za kiafya bila kujulikana.

Chanzo: BBC
 
Polisi nchini Ujerumani wanawachunguza mume na mke ambao wanadaiwa kumfungia mwanao wa kiume ndani ya nyumba kwa miaka 30, katika jimbo la Bavaria

...
Samahani; nje ya mada: Kiswahili kimekosa kabisa neno sahihi. Mwanao (wewe); mwanawe (yeye); mwanangu (mimi); mwanenu (ninyi); mwanetu (sisi); ....? (wao). Niliposoma hapo kidogo nilishtuka kusikia "mwanangu" amefungiwa huko Ujerumani ...
 
Ha! Huyo jamaa alikuwa hana minyege

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ha! Huyo jamaa alikuwa hana minyege

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
[emoji28] [emoji28] [emoji28] bila shaka alianza kujipigia puli akidhani atakuwa wa kwanza kugundua huo mchezo.
 
Back
Top Bottom