Afukuzwa uanachama kwa kutetea ukoloni

Afukuzwa uanachama kwa kutetea ukoloni

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Chama kikuu cha upinzani cha Afrika Kusini, Democratic Alliance, kimesimamisha uanachama wa kiongozi wake wa zamani, Helen Zille, kwa sababu ya tweet aliyoandika, ambapo alisema, siyo ukoloni wote mbaya.

Kiongozi wa sasa wa chama, Mmusi Maimane, alisema hata hivyo, Bibi Zille atabaki na wadhifa wake, kuwa waziri kiongozi wa Jimbo la Cape Magharibi.

Chama cha Democratic Alliance kimeshinikizwa Bibi Zille achukuliwe hatua tangu tweet zake kuzusha utatanishi awali mwaka huu.

Mwandishi wa BBC anasema, chama cha Democratic Allience, kinajaribu sana kuondosha wazi, kwamba kwa jumla, kinawakilisha masilahi ya wazungu wa Afrika Kusini.

_96331541_zille1.png
 
Adabu anazo na akili nyingi sana... ukweli always huuma nini hapo alichokwepesha? enzi za wakoloni nchi zilikuwa safi kabisa... even Tanzania.. tizama now uchafu mtupu na kodi zinakusanywa na kuliwa tu barabara mbovu zinamahandaki yake ajabu sana... taa za barabarani ni issue... kodi ni za mshahara au maendeleo?
 
Back
Top Bottom