AFTER HOUR: Album bora kabisa ya THE WEEKND.

mike2k

JF-Expert Member
May 12, 2016
1,458
3,127
Kwangu best sad album ina nyimbo 19 imeimbwa na msanii The Weeknd kutoka Canada.
Hii album ni moja ya album bora kabisa kuwahi kuisikiliza ilitoka October 2019 now ni 2021 still ina burudisha moyo wangu uliopondeka.
Album inaitwa AFTER HOUR. Humu ndani The Weeknd anaelezea true story aliyopitia baada ya kuachana na mwanamke wake Bela Hadid. Ameelezea pande zote mbili makosa yake na tabia zake chafu ndo chanzo cha hiyo break up. Nyimbo zipo in series kuanzia Wimbo wa kwanza mpaka wa mwisho. Audio na video.
Wimbo wa kwanza
Unaitwa
Alone again
Humu anaelezea siku za mwanzo after break up akili haitaki kuamini amekuwa alone again.
Too late
Aliachwa na Bela hadid baada ya kucheat na Selena Gomez. Akiwa na Celine ndo akagundua alipoteza mwanamke mzuri Bela..so akiwa anataka kurudi kwa bela ndo anashtuka ni too late.
Hardest to love
Kwenye hii ngoma kawa honest kaeleza ukweli namna alivyokuwa na tabia za ovyo kiasi kwamba amekuwa ngumu kupenda.tabia za msanii kubwa kama yeye ni pombe,umalaya na madawa ya kulevyaa so ikampelekea kuachwa mwanamke aliyempenda kwa dhati Mrembo na mwanamitindo Bela Hadid.

Scared to live
Maisha ya upweke yakamfanya hata selena Gomez aondoke. Amekosa wanawake wote so now amechanganyikiwa kabisa..amerudia tabia zake za zamani pombe,umalaya,starehe na madawa ya kulevyaa. Hii imempelekea kuwa na hofu ya kuishi.
SNOWCHILD
ngoma hii anazungumzia maisha yake before hajawa billionea na kuchanganywa na mapenzi na umaarufu. Anaelezea pia namna Bela Hadid amekuwa na mchango mkubwa kwake katika kumfanya awe real Gentleman. Snowchild ni muuzaji wa dawa za kulevya.
ESCAPE FROM LA
Humu The weeknd anamkumbuka Bela Hadid alivyokuwa anamuambia kuhusu kuhama Los Angel aka Sin City. Alikuwa anamsisitiza sana kuwa maisha ya hili jiji yanaharibu uhusiano wetu.. paparazi na umaarufu yanatunyima furaha yetu. Sasa anakumbuka anamwomba arudi aje amtoe Los Angeles coz amekuwa malaya, mtumiaji wa madawa ya kulevya...licha ya umaarufu alioko nao lakini bila Bela hadidi ni useless.

Heartless
Hii track ni muendelezo wa ESCAPE FROM LA sasa ameanza kukubaliana na ukweli kuwa Bela Hadidi hatorudi tena so amerudi kwenye tabia zake za mwanzo umalaya,pombe,starehe na matumizi ya madawa ya kulevya kwa sababu ni heartless. Humu anaelezea jinsi anavyotumia ovyo utajiri wake kwa sababu tumainia la moyo wale limeondoka hana hisia na chochote.

FAITH
Baada ya kurudi kwenye tabia zake zamani ameamua kujisifia namna anavyofaidi kutumia aina tofautitofauti za madawa ya kulevya...kwa sababu amepoteza imani. Amerudi kutumia haya madawa coz stress za mapenzi zinataka kumuua.

BLINDING LIGHT
Hii ni moja ya ngoma kali sana katika hii album. Ni mwendelezo wa faith. Kwenye video yake utamuona amelewa kachanga unga na pombe kali anaondoka club saa nane usiku anachukua mercedez mid engine car anaiendesha rafu kama kutaka kujiua hivi kwa ajali. Humu anaelezea jinsi Bela Hadid alivyokuwa mwanamke wa muhimu kwake coz alikuwa anamjulia sana kuanzia kitandani mpk kwenye maisha ya kawaida sasa hayupo anammis ile mbaya. Anamuomba arudi coz maisha ya umaarufu yanamfanya akose mtu wa kumsimamia na kumuelekeza chochote so ame BLINDING BY THE LIGHT.
IN YOUR EYES
NI Muendelezo wa BLINDING LIGHT anasema kuwa anafahamu kabisa kuwa bela hadidi na yeye anaumia pia kuharibika kwa uhusiano wao..analitambulia hilo kupitia macho yake. Baada ya kuachana bela hadidi kwenye interview alikuwa akiulizwa kuhusu uhusiano wao alikuwa hajibu analia tu.

Save your tear
Hii amewaelezea wote wawili bela Hadidi na selena gomez.
2019 akiwa kwenye tamasha la Coachella the weeknd alikuwa anatumbuiza akiwa kwa stage akamuona Bela Hadidi akiwa na mwanaume mwingine anauamia ila Bela Hadid ana pretend kama haumii ila anashindwa na yeye anatoka nje akiwa analia.
Selena Gomez alimwacha weend baada ya kugundua kuwa nachati na Bela Hadidi so akaona anazingua akavunja uhusiano. So anaambiwa na the weeknd kuwa asiumie coz hana moyo wa kupenda tena hata yeye haelewi ni kwanini aliondoka na kumuumiza. Kwenye video ameona asimuache Bela hadidi hivi akamchamba kidogo koz amefanya plastiki surgery na wanawake wengi wa Los Angel wamefanya PS na ndo ulevi wake sura nzuri so amejikuta anatembea nao ovyo.

AFTER HOUR
Hii ni dark song. Anarudi kuelezea ule usiku wa kwanza akujua kuwa sasa Bela Hadidi hatokuja rudiana naye tena. Anaelezea jinsi alivyokuwa anawaza. Anamuomba sana aweze kurudi coz hali yake ni mbaya amechanganyikiwa kabisa.
Hii album imeandaliwa na XO record humo ndani nyimbo zimeandaliwa vizuri sana. Na video zimetengenezwa kama episode. Director wa video ni yule wa Goodfather. Aina ya music ni alternative RNB

N.B nitawaletea behind the scene wakiwa studi wanarecord hii album. Performance yake kwenye chart mbalimbali za music.
Video zake zote za hii album.
Show ya NFL SUPERBOWL ambayo ali perfom hii album.
 
Oyaa kuna album inaitwa BEAUTY BEHIND THE MADNESS hii ndo album kali ya jamaa hzo zingine porojo. Bila shaka leo ndo umesikiliza hio album
 
Oyaa kuna album inaitwa BEAUTY BEHIND THE MADNESS hii ndo album kali ya jamaa hzo zingine porojo. Bila shaka leo ndo umesikiliza hio album

Nimesikiliza kila album ya The Weeknd. Nime share na wapenzi wa music mzuri. Na nitazidi kushare album nzuri zinazo trend na zisozotrend.
Next tutaenda kuichambua Appolo by fireboy DML
 
Nimesikiliza kila album ya The Weeknd. Nime share na wapenzi wa music mzuri. Na nitazidi kushare album nzuri zinazo trend na zisozotrend.
Next tutaenda kuichambua Appolo by fireboy DML
Ukiichambua Appolo nitag maana mimi ninaamini Appolo ni album kali kwa mwaka 2020 kuliko twice as tall , made in lagos na a better time
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom