AfroIT inahitaji waandishi na michango yenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AfroIT inahitaji waandishi na michango yenu

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kilongwe, Jan 4, 2011.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wanajamii,nina imani wengi wetu tuna moyo wa kuchangia elimu yetu kwa jamii.

  Timu nzima ya AfroIT inahitaji wataalam ambao wana moyo wa kujitolea kuandika makala mbalimbali zinazohusu ICT na teknohama kwa ujumla.

  Kwa sasa,hatuna uwezo wa kukulipa kwa kazi hii ila wanajamii wenyewe ndio watakaokulipa.Pia kwa kufanya hivi nina imani unajijengea uzoefu mkubwa wa kufafanua ulichokielewa kwani mada zote huwekwa kwenye AfroIT na mitandao rafiki ambapo mamia ya watu hutembelea na kujisomea.Hivyo utapata changamoto na ari zaidi.

  Kitu cha muhimu ni kuwa,hakuna mtu aliyezaliwa na kuanza kukimbia,hivyo usiogope kwakuwa huna uzoefu,uzoefu utaupata ndani ya AfroIT.Binafsi nilianzisha AfroIT pindi nikiwa digrii ya kwanza mwaka wa pili,sikuwa na uzoefu wowote,hii ilitokana na mawazo na upendo wangu kwa jamii kwani watanzania wengi tumekuwa watu wa kulaumu sana,sasa muda ufike tuanze kuonesha ari zetu kwa vitendo.

  Muhimu: Kila muandishi ataweza kuingia kwenye timu ya waandishi wa AfroIT na ataweza kupata faida zote za waandishi wa AfroIT zikiwemo kutambulika kama mwandishi wa AfroIT,kuruhusiwa kutumia Logo ya AfroIT,kushiriki katika kila uendelezi wa AfroIT na nyinginezo ambazo zinakuja jinsi siku zinavyosonga mbele.

  Mwisho: Tupo njiani katika kukamilisha AfroIT Kisima .Hii ni kitu kama Wikipedia(au Baidu Sayansi) ambayo italenga sana Afrika ya Mashariki(Lugha mama itakuwa ni Kiswahili),AfroIT Kisima itakuwa na kila kitu,sio tu ICT bali hata mambo ya Afya,mazingira,mechanics nk ambapo waandishi na members wote wa AfroIT watakuwa na uwezo wa kuchangia makala,kuhariri nk.Sio tu kuwa na mambo mengi bali pia Wana AfroIT Kisima wataweza kuwa na Social Network kati yao.

  Hii ni Phase ya Nne baada ya Phase ya tatu ambayo tunatarajia kuitoa Siku yoyote ya wiki inayokuja.

  Kushiriki uandishi tuandikie kwenye webmaster@afroit.com kama una maoni au ushauri basi nenda kwenye AfroIT Forums.

  Nyoni
  AfroIT Group
   
 2. edjizzo

  edjizzo Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Poleni kwa kazi kamanda . Nadhani kuanzia mwaka huu nitakuwa machangiaji mkubwa .. mara nyingi nimekuwa msomaji tu

  lakini nadhani focus yenu inatakiwa kuwa ICT. hata ikiwa kuna mada za Elimu, afya. Utawala, sheria ,n.k basi tujadili ni vipi ICT inaweza kuboresha au kusadia huduma na taaluma hizi na wanataaluma kwenye fani mbali mbali.

  ingawa nyie ndio wamumzi wa mwisho lakini binafsi sitapenda kuona mada za kisiasa zaidi zisizo na ladha wala idea ya teknolojia ya ICT.

  So no matter how you expand stick To ICT as your core Mission and Vission

  Mfano

  hapa jamiiforums watu wamejdili kisiasa sana nec na Uchaguzi. Afroit anzisheni mada tutayochambua NEC kiteknolojia tujue vifaa vya ki ICT vilivyotumika wakati wa uchaguzi, kazi zake, uwezo wake. Vilisaidia au vilichelwesha mambo?

  I mean mnaweza au tunaweza kuongelea thing from techonological/ICT point of view

  Nawasilisha.
   
 4. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mkuu ndani ya AfroIT ni mambo ya elimu kwenda mbele.Hata tunapozungumzia Afya na mengiineyo tunamaanisha Elimu Elimu.Ukiangalia hizo site mbili nilizotolea mifano ambapo tutaiga mambo fulani zote hakuna mambo ya Siasa.Ni maarifa juu ya maarifa.

  Binafsi kitu niachoamini ni kuwa kila mtu amezaliwa na kipawa chake,hivyo ni jukumu letu kugawana kila mtu kulingana na uwezo wake.kwani kila kitu muhimu lazima kuwe na uwiano.

  Hivyo tegemea kuona mambo mengi ya maarifa ndani ya AfroIT,tumeanzisha TanzMED.com kwa ajili ya afya kama njia za awali za kuendea AfroIT Kisima.
   
 5. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mfano mzuri.Kwa vyovyote vile uchaguzi wa 2015 kama mambo yatakwenda sawia basi tutakuja na kitu cha uhakika ili kuwawezesha watu kupata matokeo online mapema.Hakuna kisichowezekana kama tutaongea kwa vitendo kwani kuna mifano asilia mingi.
   
 6. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Mikono mitupu hailambwi
  Mambo ya kutafuta sifa kupitia michango ya kitaaluma kama hiyo yamepitwa na wakati
  Kwani nyie manendeshaje kampuni yenu,ni kwa njia ya huduma au **** ka-income mnapata,kama kapo kwa nini msigawame na hao wachangiaji

  Kama ni ipo kama JF kuwa wazi
   
 7. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Bwana Kilongwe,

  Huko kijiji cha ICT, mna-solve matatizo ya jamii lakini au mnandika Articles kujiridhisha ninyi wenyewe ...kwa raha zenu?!
   
Loading...