#COVID19 Afrika yakabiliwa na utata katika kupambana na ugaidi wakati wa kuishi na COVID-19

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111188067900.jpg

Gazeti la The Nation la Kenya liliripoti kuwa kundi la kigaidi la al-Shabaab hivi karibuni limetekeleza mfululizo wa mashambulizi katika kaunti ya Mandera, nchini humo na kusababisha vifo vya watu wengi na uharibifu mkubwa, na huenda nusu ya ardhi katika kaunti hiyo inadhibitiwa na kundi hilo.

Mashambulizi hayo yameufanya ugaidi wa kikanda ambao unaonekana kutoweka baada ya kutokea kwa maambukizi ya COVID-19 kutajwa tena na jamii ya kimataifa, na pia kuleta utata mkubwa kwa vita dhidi ya ugaidi barani Afrika wakati bado tunaishi na COVID-19.

COVID-19 imeleta pigo kubwa kwa mfumo wa kisiasa wa kimataifa na maendeleo ya uchumi. Uchumi wa dunia unafufuka polepole kwa sababu ya mitazamo tofauti ya kutetea na kupinga utandawazi, na jamii ya kimataifa inalazimika kupunguza nguvu ya kupambana na ugaidi, kitu ambacho kimeyapa “fursa” makundi ya kigaidi. Kundi la IS limejitahidi kujikuza wakati wa COVID-19, kuongeza matangazo kuhusu ugaidi na kusababisha baadhi ya sehemu za Afrika kujitumbukia kwenye mikono ya magaidi.

Aidha, kwa muda mrefu, sera hasi na inayojitafutia faida ya Marekani katika kupambana na ugaidi pia imeleta athari mbaya, na kwamba sera ya kubembereza na kupigana na kundi la Taliban la Afghanistan kwa wakati mmoja, na vitendo vya kumwua mkuu wa jeshi la Iran jenerali Qassem Suleimani, na kuhimiza upatanishi kati ya nchi za kiarabu na Israel bila ya kuzingatia maslahi ya Palestina vimezusha mivutano kati ya pande mbalimbali, ambayo inazidi kuwa mikubwa. Aidha, Marekani imehusisha vita dhidi ya ugaidi na haki za binadamu, na kuichukulia kama ni karata yake katika kuzungumza na China, jambo ambalo kwa kiasi fulani limesaidia shughuli za kigaidi.

Ikiwa ni sehemu ya kuondoa msimamo mkali, kupambana na ugaidi kwa silaha haiwezi kuwagusa watu kimawazo, lakini ujenzi mpya wa uchumi na maendeleo ndio hatua za kimsingi. Miaka mitano iliyopita, serikali ya Kenya ilitoa “mkakati wa kitaifa wa kupinga msimamo mkali wa kimabavu”, unaolenga kuhimiza maendeleo ya sehemu zinazoathiriwa na msimamo mkali wa kidini na kusisitiza mradi wa kuwapa wanawake madaraka na kuwatolea mkopo, ili kuepuka watu wa kawaida kuathiriwa na msimamo mkali.

Katika zama za leo wakati shughuli za ugaidi zinazidi kuwa za kimataifa, kazi ya kupambana na ugaidi ya nchi yoyote haiathiri nchi hiyo yenyewe tu. Nchini Kenya, wapiganaji wa kundi la al-Shabaab la Somalia wamekalia zaidi ya nusu ya ardhi katika kaunti ya Mandera, kudhibiti barabara nyingi, kuendesha misikiti mingi, kuwatoza kodi wafanyabiashara, kuharibu vifaa vya mawasiliano ya simu, na pia kufanya biashara ya dawa za kulevya. Kama Kenya, China pia ni mhanga wa ugaidi. Kundi la kigaidi la Turkistan ya Mashariki limeshirikiana kwa karibu na makundi mengine ya kigaidi ya kimataifa, na kutokana na msaada wao, waliingia na kufanya mashambulizi ya kigaidi mkoani Xinjiang, China, na kukwamisha sana maendeleo ya uchumi na jamii mkoani humo.

Siku hizi nchi nyingi za Afrika zimetambua ulazima wa kuondoa msimamo mkali kikamili na kimfumo, na kutoa mbinu zao za kitaifa na kikanda katika msingi wa kuangalia thamani ya jadi ya kiafrika na kutumia utaratibu wa kutatua migogoro ya ndani. Katika vita dhidi ya ugaidi, kukinga ni muhimu kuliko kupambana nao. Katika sekta hiyo, China imechukua hatua za kuwazuia magidi kurudi na kuvuka mipaka ya nchi, kupambana na ugaidi kwenye mtandao wa internet, na pia kutoa elimu na msaada kwa magaidi. Mkoa wa Xinjiang haujashuhudia mashambulizi ya kigaidi kwa miezi karibu 50, huku kazi ya kuondoa umaskini mkoani humo ikiwa imepata maendeleo makubwa na wakazi wa huko wanaishi maisha salama na yenye fursa.

Kwa nchi nyingi za Afrika, wakati tunapolazimika kuishi na COVID-19, ili kukuza uchumi, inatubudi tufungue mipaka ya nchi, hivyo jinsi ya kuwazuia magaida wakati huo ni changamoto ya sasa. Wakati wa COVID-19, ugaidi bado ni adui wa pamoja duniani, na nchi mbalimbali zinatakiwa kufuata sera ya pande nyingi, kuongeza mshikamano na kukabiliana na changamoto ya kiusalama isiyo ya jadi kama vile ugaidi.
 
Back
Top Bottom