Makosa ya Pauline Gekul yanaangukia katika Ugaidi na hayana dhamana

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,802
71,229
Kuna nguvu kubwa inafanyika kuyafanya makosa ya aliyekuwa Naibu Waziri Sheria na Katiba kuwa ni udhalilishaji wakati kiukweli sivyo.

Makosa ya Gekul kisheria kwa Tanzania au nchi zingine ni UGAIDI maana ameteka, kaongoza kundi la wahalifu wenzake, kutesa na vitisho vya kuua pamoja na huo unyanyasaji.

Kama haki itatendeka, basi tunategemea kumuona Pauline Gekul nyuma ya nondo kwa muda mrefu wakati kesi ikiendelea kuitafuta haki.

Kuifanyia figisu kesi hii itaonyesha hata boss wa Gekul wa zamani yaani Rais Samia hana uchungu na yaliyompata huyo kijana ambaye ni kama mwanae kwa sababu ya kumlinda senior member wa CCM.

Rais haingilii mhimili mwingine lakini kwa vile ofisi ya mwendesha mashtaka iko katika mhimili wake (executive) kutotimiza wajibu wake yeye hana pa kukwepea AIBU HII.

- Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

20231127_165316.jpg
 
Ungetuwekea ingredients za kosa la ugaidi ingependeza zaidi kutoka kwenye sheria husika. Lakini siamini kama kuna ugaidi unaohusisha individual tena mkiwa mmejifungia ndani, ule kwangu ni ujambazi tu.

Ugaidi niuonavyo mimi lazima uambatane na matumizi ya silaha za moto kwenye hadhara ya watu wengi, sio mafichoni, kwasababu naamini magaidi hawafanyi mambo yao mafichoni wanashambulia maeneo ya public.

Mfano kule Kenya, Westgate kama utakumbuka; USA ile September 11, au Kenya tena, eneo la Garisa kama sijakosea, waliposhambulia shule, au Boko Haram kule Nigeria.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Ila ni mzuri bhana na.ndoo maana watu wanamakasiriko yaan anawaongezea hasira

Anyway no one is above law, acha tuone
 
Back
Top Bottom