Afrika ondokeni kwenye mfumo wa Vyama Vingi

Afrika ondokeni kwenye mfumo wa Vyama Vingi

Siasa inataka mtu mmoja mmoja ajitambue, ajue haki na wajibu wake, atetee maslahi yake na walio wengi (taifa), akiwa ndani au nje ya chama cha siasa.

Changamoto ya African ni kwa wananchi walio wengi Kutojitambua na hii ndiyo iliyowapeleka mababu utumwani, ukoloni na hata sasa ukoloni mamboleo.

Ni lazima wananchi wapambane pale wanapoonewa kuanzia ndani hadi nje. Historia inaonesha uwepo wa mapambano ya haki tangu mwanzo kabisa wa uwepo wa mwanadamu.

Woga ni umasikini. Hata hivyo, ni lazima kupigana vita kwa kutumia akili na siyo vya wenyewe kwa wenyewe.
 
Kwa upande mwingine China (chama kimoja) imeinua watu zaidi ya milioni 800 kutoka umaskini, hii inatokana na ripoti ya World Bank. GDP ya China imekua wastani wa ~9–10% kwa miongo kadhaa.
Naona unapenda kutoa mfano wa China, ila unafumbia macho ukweli kuwa Wachina wana umakini na uthubutu ambao nchi kama Tanzania haiwezekani kufanya.

Kwa mfano, Tanzania ikiiga utendaji wa China kwa kumaanisha 98% ya watawala na watendaji wa Taasisi za umma karibu zote watanyongwa hadharani au kufungwa maisha kwa makosa ya udanganyifu, ufisadi, uhujumu uchumi, wizi, mauaji, upendeleo (nepotism), na uhalifu mwingine..

Wachina Hawakufika hapo walipo kwa kufanya mizaha.

Kwa jinsi Waafrika walivyo waroho na wabinafsi, kukumbatia mfumo wa chama kimoja ni kukaribisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kudumu, na mifano ipo mingi
 
Waafrika hawawezi kukuza uzalendo wa kulitetea mataifa yao maendeleo yanayoendana na kazi ya karne hii, ikiwa tupo mfumo wa vyama vingi, hapa kunakuwepo kusalitiana ni dakika na sekunde yoyote, kupandikiza chuki za kisiasa miongoni mwa wananchi ili kupata wafuasi
Mbona maccm wenyewe kwa wenyewe hupandikiziana chuki, majungu, fitna, kuwekeana sumu na kuuana?

Ukweli ni kuwa hakuna nchi yoyote Afrika iliyopata maendeleo kupitia udikteta wa chama kimoja.

Ila zipo nchi zenye demokrasia ya vyama vingi zilizopiga hatua kubwa, mfano Botswana, Ghana, Cape Verde, Mauritius
 
Mbona maccm wenyewe kwa wenyewe hupandikiziana chuki, majungu, fitna, kuwekeana sumu na kuuana?

Ukweli ni kuwa hakuna nchi yoyote Afrika iliyopata maendeleo kupitia udikteta wa chama kimoja.

Ila zipo nchi zenye demokrasia ya vyama vingi zilizopiga hatua kubwa, mfano Botswana, Ghana, Cape Verde, Mauritius
Mkuu, sijataja chama chochote cha siasa. Kingine wacha kupotosha watu aidha kwa kujua au kwa kutokujua.

Soma hapa upate hizo nchi zako:
👉👉 Nchi 11 zenye Uchumi Mkubwa (Pato Ghafi) barani Afrika mwaka 2025 - BBC News Swahili
 
Hiyo mifumo inaundwa na watu walioko kwenye vyema kama vile wabunge watunga sheria ambazo wanapewa wataalamu kuzisimamia. Huko kwenye bunge ni watu kutoka kwenye vyema ambao kwa mujibu wako ni wapiga kelele.
Wabunge wanapatikana sio lazima kupitia vyama vingi, hata chama kimoja wabunge wanapatikana. Na kuundwa mifumo haiundwi na vyama vy siasa.
 
Which revolution Africans need rather than monoparty system?
Monoparty is not a revolution for Africa, Tanzania we were under monoparty for about 30 fuckking years.
 
Wabunge wanapatikana sio lazima kupitia vyama vingi, hata chama kimoja wabunge wanapatikana. Na kuundwa mifumo haiundwi na vyama vy siasa.
Unawaweza kuwapata wabunge bila kuwa na hata chama kimoja pia, tufute vyama vyote tu kabisa.
 
"wananchi wanaojitambua" unamaanisha nini hasa. Let say watu 60M unamaanisha katika hao utachagua wanajitambua?
Swali lako limekaa kama la kipuuzi hivi; lakini baada ya kutafakari juu yake kwa kina nimeona huenda siyo la kipuuzi, bali linaonyesha upungufu wa uelewa kwa uapnde wako.

Kwanza inabidi ujuwe maana ya hilo neno "kujitambua" ni ipi, na jinsi linavyotumika katika mjadala husika

Katika maswala ya kisiasa, siyo wananchi wote wa nchi hiyo yenye watu 60 milioni kama ulivyotolea mfano;, kwamba wote watakuwa katika ngazi moja ya utambuzi kwenye siasa; na usitegemee wote kushiriki kwa pamoja kubadili mwelekeo katika nchi hiyo.

Hapa Tanzania usitegemee kamwe kwamba mabadiliko yatapatikana kwa wananchi zaidi ya milioni 60 kushiriki (kujitambua) kwenye maswala yanayotakiwa kubadilishwa; kama kuwaondoa madarakani hawa waovu wanaoyashikilia kwa mabavu bila ridhaa ya wananchi.
 
Unawaweza kuwapata wabunge bila kuwa na hata chama kimoja pia, tufute vyama vyote tu kabisa.
Tuwe kama waarabu, au siyo?

Lakini inabidi nikiri hapa wazi, sijui kama kwenye nchi hizo, kama Saudi Arabia; UAE wanao wabunge.
Ila najuwa hakuna vyama vya siasa.
 

We need checking and balancing of the system. USSR na zile Eastern countries mbona walifaili sababu ya mambo ya chama kimoja.
Chama kimoja kutawala kinaleta umangimeza, ubabe na watu wachache kujipa nafasi za umungu mtu. Kutishia na kuwaogopesha wengine bila sababu za maana.
Mfumo wa chama kimoja unaleta rushwa na kujisahau kwa watawala. hauna tija miaka ya sasa. na anayetaka kulazimisha mfumo wa aina hiyo ajiandae kuanguka maana forces zote kubwa za dunia hii zitapambana naye.
Mara nyingi hoja kama hizi zinaletwa sababu ya watu wachache wabinafsi ambao kwa sasa wananufaika na njia mbovu mbovu za kupata riziki. wanataka njia hizo ziendelee milele na milele wakati hakuna mtu anayeishi milele.
Africa inasikisha...Angalia Cameroon, Equtorial Guine, hata Uganda na kushangaa...what next? Mbona kama all the signs shows a problem?
 
Cha kushangaza ni kua hata wewe saivi ukiambiwa uchague nchi yoyote ya kuishi duniani utachagua nchi yenye vyama vingi kutokana na ubora wa maisha.

Kama unabisha basi jaribu kufanya utafiti wa ubora wa maisha kwenye hizo nchi ulizo tolea mfano.
 
Naunga hoja mkono.

Afrika demokrasia hatujawahi kuwa nayo,

Ngumu sana kuipokea.
 
Wewe jamaa una akili sana ...Nahisi mmeshaanza kuzinduka.. Hongera na heshima yako Mkubwa.

Sipendi vyama vya siasa.
 
Back
Top Bottom