Afrika na utumwa wa kifikra

msakaa jr

JF-Expert Member
May 18, 2017
6,512
6,723
Nawasalimia ndugu zangu katika ukweli na ukuu wa mwafrika!

Hivi kwanini mafukara na wasioelimika kwa kiasi kikubwa wanaonekana kuathiriwa na dini hizi za kigeni, Ukiristo na Uislam? Kuna tatizo gani katika makundi haya?

Ni ajabu waafrika tumehadithiwa hadithi zisizo na uthibitisho si wa mantiki wala sayansi ispokuwa kwa roho mtakatifu na sisi tukaamini - huu si utumwa wa kifikra?

Hebu fikiria kidogo tu ni kwa namna gani utampata roho mtakatifu bila kumuamini ili uweze kuelewa yanayozungumzwa katika vitabu vyao? Huu si mtego wa kifikra?

Unakuta Afrika leo hii tumejaza makanisa na misikiti kuliko viwanda utadhani sie ndio waarabu na wazungu, kwamba sie ndio tunamjua Mungu wa Bible na Quran zaidi ya wenye hadithi zao lakini papo hapo matendo ya kinyama, ufukara na maradhi ndio vinazidi kutuandama kuliko jamii yoyote duniani - huu si utumwa wa kifikra kweli?

Ni ukweli kwamba sisi tunaingia makanisani na misikitini kusali sana zaidi ya jamii zingine lakini bado umaskini, maradhi kutostaarabika imekuwa utambulisho wetu duniani - lazima kuna sehemu tunakosea waafrika.

Wazungu na Waarabu wametuchagulia Mungu yupi sahihi na tumuabudu. Tumeingizwa katika mifumo ya tamaduni zao kuanzia lugha, elimu hadi mavazi lakini bado haturuhusiwi kuhoji hata kama wanayotwambia hayaeleweki wala hayatuongezei thamini yoyote katika maisha. Halafu bado tunaamini Mungu wa wanaotuona maadui na jamii dhaifu kuliko zote duniani anaweza kumaliza matatizo yetu - huu si utumwa wa kifikra kabisa?

Si vibaya kutambua mchango chanya wa hawa wageni lakini tukumbuke wahindi, waChina, waJapan, waKorea wao pia walitawaliwa lakini leo hii wanatunishiana vifua na mabeberu- kwanini wao wapo hivi? Waliutambua ukuu wao, hawakuuacha.

Tatizo waafrika tumepokea hizi dini za kishenzi tukaacha tamaduni ambazo ndio nguvu na ukuu wa jamii yoyote Ile duniani ulipoegemea.


NB:Imani bila elimu ni jazba

Karibuni kwa mawazo zaidi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka nini kifanyike urudi kwenye matambiko ya wazee wako wa zamani?
 
Back
Top Bottom