Afrika mashariki imara ( The great east africa )

yussufhajj

Member
Mar 24, 2016
27
8
Wakati umefika kwa Afrika Mashariki kuwa eneo imara katika bara la Afrika.

Baada ya kuwepo kwa soko la pamoja , uhuru wa forodha sasa tunatarajia kutumia fedha ya pamoja ambapo baadae tunategemea shirikisho la Afrika Mashariki.

Kuchelewa kwa kufikia Afrika Mashariki kuwa na shirikisho tayari kumezua mijadala mbali mbali ikiwemo nchi kunyosheana vidole wenyewe kwa wenyewe juu ya uchereweshaji huo.

Swali la kujiuliza nini hasa kinakwamisha kuwepo kwa shirikisho la Afrika Mashariki?

Je ni kweli kwasababu ya kuutekeleza mkataba wa jumuiya ya Afrika Mashariki kipengele kimoja hadi chengine? Au
Ni hofu tu miongoni mwa nchi washirika ? Ww una onahe hasa?
 
Shirikisho la Africa mashariki litawezekana pale tu Burundi, Rwanda na Uganda watakapoondoa mfumo wao wa kutawaliwa na wafalme! SIJUI NI LINI HIYO!!!!?
 
Mkuu hili swali ni wazi kabisa kwa wadadisi ya mambo:mbona ni Tanzania inayoonekana kuyumbayumba kwa mipango ya pamoja??
Pili binafsi naunga muungano wa forodha/ushuru etc lakini sio ya kisiasa(nchi zetu bado changa).
Tatu muungano wowote ule (liwe ya ndoa au kibiashara)lazima uwe wa kimaadili. Nini maadili yetu? Yako sambamba?
 
Back
Top Bottom