AFRIKA KUSINI: Umati wamshambulia mchungaji kuuzia watoto dawa za kulevya na kuendesha danguro

Reucherau

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
756
1,740
- Mchunguji mmoja aliponea chupuchupu baada ya kushambuliwa na umati kwa madai ya kuuzia watoto wa shule dawa za kulevya

- Umati huo ulifika kwa lango la kanisa lake na kutaka kumwona lakini alipoenda kuwaona alishangaa kwani walianza kumshambulia

0fgjhs19llanhrb8o8.80e76d6f.jpg

Umati wamshambulia mchungaji kwa kuendesha danguro!

Mchungaji mmoja alinusurika kifo baada ya kushambuliwa na umati uliokuwa na ghadhabu eneo la Atteridgeville, Afrika Kusini. Mchungaji huyo alikashifiwa kwa kuuza dawa za kulevya na kuendesha danguro.

Nabii Samson Sangojinmi, kiongozi wa kanisa la Celestial Church of Christ anashukuru Mungu na maafisa wa polisi waliomuokoa kwani angeuawa na watu hao.

0fgjhs7k5lp8rrg0j.8c605fa9.jpg

Umati wamshambulia mchungaji kwa kuendesha danguro!

Kulingana na ripoti, vijana hao waliosemekana kuwa walevi waliingia kanisani kutafuta dawa za kulevya na vitu vingine walivyosema vilikuwa vikiendelea kanisani humo.

Mwanamke mmoja alidai kuwa aliona watoto wa shule wakiwa na sare wakiingia nyumbani mwa mchungaji huyo.

“Baadhi ya wasichana tunaowapata humo huwa wamelewa na kuvalia nguo fupi, ishara kwamba wanafanya ukahaba,” alisema mwanamke huyo na kuongeza kuwa walikuwa wametosheka hasa kwa sababu polisi walikuwa wamekataa kumchukulia hatua.

0fgjhs1korjjl644tg.a8c5257c.jpg

Umati wamshambulia mchungaji kwa kuendesha danguro!

Walichoma nyumba zake mbili na kumshambulia vibaya na kumjeruhi. Lakini alikana madai yao.
 
Back
Top Bottom