AFRIKA KUSINI : Nabii awanywesha waumini kemikali ya kusafishia injini, adai inaponya

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
ee389501e53d855a9fcbfac0e153772f.jpg
Mtu mmoja anayejiita nabii nchini Afrika Kusini amesababisha wafuasi wake kunywa kemikali ya kusafishia injini, akidai kuwa ina uwezo wa kuponya na ina ladha ya asali

Theo Bongani Maseko wa Kanisa la Breath of Christ Ministers, anasema kuwa kemikali hiyo hushambulia virusi kwenye mwili wa binadamu, na kutambua mashetani

Mtu huyo ni kati ya wanaume kadhaa ambao wamezua shutuma kwa kuwamwagia watu dawa ya kuua wadudu na pia kuwashauri kula wanyama

Bwana Maseko alinukuliwa akisema kuwa kemikali hiyo haina athari za kiafya

"Ina ladha ya asali, nimekunywa mara mbili".

Aliongeza kuwa watu watatu wameponywa kwa kunywa kemikali hiyo.

Chanzo : BBC
 
mijitu mijinga ndio iliwao na wanaojiita wachungaji,manabii,wapakwa mafuta wa bwana na majina lukuki.
 
Back
Top Bottom