Afrika Kusini: Mchungaji Alph N Lukau afufua maiti na kuacha gumzo kubwa

Kwani shida ni kufufua mtu ama ? mbona maandiko yameweka wazi kwamba waamin wanaweza kufufua,MATHAYO 10:8,me nafikiri wakristo wasio amini kwamba mtu anaweza kufufuliwa ndio wa kuwaashangaa .
Hata mie nawashangaa watu wanavyopinga miujiza ya mchungaji labda tuwawekee video yake hapa ili wanaopinga wajue ni kweli tukio limetokea.

Kwenye kuponya vilema na mapepo wanakubali ila hili ndiyo wanakana!

 

Aisee...sasa walimuweka vipi na simu kwenye jeneza...

Halafu ety Ni cameraman wa mchungaj ..
Ukiikuta mijitu kama hii Ni kucharaza tu na fimbo..inatuchafulia dini

Sent using Jamii Forums mobile app
tapatalk_1551272557100~2.jpeg
 
Habari wanaJF,

Siku hizi kumekuwa na kuibuka Kwa makanisa kama uyoga na wachungaji wote au manabii wanafanya Mambo ya kimiujiza ujiza tu,sikatai na nimekulia Kwenye Dini ya kikristo yenye imani Kali na Mungu kweli huwa anatenda Kweli ukifunga na ukapiga goti na kumlilia.

Ila siku hizi MUNGU amekuwa akifanya miujiza akiona camera tu,inasikitisha sana kwakweli maana Mahubiri yamekuwa yakishangaza Hata ukimsikia mchungaji au Nabii mambo anayozungumza yanasikitisha sana na Ukristo umekuwa ukitumika kama biashara Kwa hawa fake pastors.Huwa najiuliza kwanini wakristo hatujiulizi maswali magumu na kukumbuka maandiko yaliyokwenye Biblia kuwa Siku za mwisho kutakuwa na manabii wa uongo,na wanajidhihirisha waziwazi.

Mfano maigizo ya mchungaji wa South Africa aliyejifanya amemfufua mtu kumbe ni uongo na huyo aliyejifanya kafufuliwa ni cameraman wa Kanisani hapo,Baada ya Waandishi kuwafuata wanajificha kwanini wafiche kama ni jambo? Baada ya dili kubumbuluka na kuumbuka wajificha,lengo ilikuwa kutengeneza uongo ili apate wafuasi na kupiga pesa.,inasikitisha sana.

Serikali wakati wa kuanzisha haya makanisa binafsi ongezeeni vigezo saiz imekuwa kero.

Video Hapo chini mwandishi wa SABC News aliyekuwa anafuatilia suala la mtu kufufuliwa.
Ndiyo maana Kagame ameweka masharti magumu. Kuanzisha kanisa ni lazima uwe na shahada ya kwanza ya Theology, usiwe na ishu za utapeli huko nyuma na uwe na wadhamini (watu wanaokufahamu tabia zako na wanaoweza kukushuhudia).
 
Duh,, wajinga ndio waliwao
Kumekuwa na kasumba wakristo wengi wameacha kumtegemea Mungu wanategemea manabii na miujiza ya uongo
Almost 90% ya watumishi Ni matapeli na waongo
Yapasa kila mmoja kusimama kwa zamu yake,, wengi wanaopenda miteremko ndo huishia kulizwa huko

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona funeral home alikorent gari ya kumbebea "marehemu" wameamua kumshitaki...
Screenshot_20190227-081031~2.jpeg
 
Naona funeral home alikorent gari ya kumbebea "marehemu" wameamua kumshitaki...
View attachment 1033370
Mijitu Kama hii inafanya dini ionekane mbaya,,mi wananikera yaani
Kwanini asiende hospital maiti zimejaa huko
Wamshitaki tu

Huyo kijana kwenye jeneza nae akapimwe akili,,akikutwa Ana akili Safi Basi wote pamoja na mchungaj wake wasombwe ndani..anaupata wapi ujasiri wa kuigiza ujinga huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyefufuliwa aumbuliwa na mfanyakazi mwenzake||

Baada ya kusambaa kwa habari zilizoleta sintofahamu kutoka nchini Afrika Kusini za mchungaji kumfufua mtu, mapya yanazidi kuibuka juu ya tukio hilo ambalo mpaka sasa imekuwa vigumu kwa wengi kuamini kuwa ni kweli limefanyika.

Habari kutoka Afrika Kusini zilizochapishwa kwenye mtandao wa Eye Witness zinasema kwamba mtu huyo aliyefufuliwa anajulikana kwa jina la Brighton, ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya mbao ya PTY katika mji wa Pretoria, na tayari ameshakamatwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi.

Akimuelezea Brighton, mmiliki kampuni hiyo Vincet Amoretti, amesema kwamba kwa mara ya mwisho Brigton alionekana ofisini Februari 19 huku akiwa amechelewa akitokea mazishini siku ya February 16 na 17, na alichelewa kurudi baada ya wazee kumuomba akae kwa siku moja zaidi.

Vincent ameendelea kueleza kwamba si mara ya kwanza kwa Brighton kufanya hivyo kwa mchungaji wake (Alph Lukau), kwani alishawahi kumsaidia kwenye muujiza mwingine ambao alijifanya kiwete na kupata uponyaji, huku akimsifia kuwa ni mchapakazi kwa kuweza kufanya kazi sehemu mbili.

“Unaweza kufikiria ni maisha gani alikuwa nayo!?. Alifanya kazi kwangu, akafa, akafufuliwa na sasa amekamatwa na polisi”, amesema Vicent. Hata hivyo tume inayoshughulika na masuala ya dini na utamaduni imesema haitalifumbia macho tukio hilo, na kwamba lazima hatua za kisheria zichukuliwe.
 
Kumbe hats roho mtakatifu anadanganyika huyo alitakiwa kutambua kama kristo alivyo tambua na watakatifu wa kale
hichi unacho kisema ndicho na mimi nahisi , i,m not sure . mfano ninavyomjua alpha lukau ,ni mtu very humble , kwa sisi tunaosoa theology kwa mrengo huu wa kilokole , na kama yesu alivyosema , ufalme wa shetani hauwezi ukapingana wenyewe kwa wenyewe. kwa south africa pastor anayekuja kwa kasi sana ni huyu ,akifuatiwa na bushiri , wote hawa wanatakiwa kuondoka south africa . wapishe wazawa , kama charis mission nk .

ukiangalia zile kampuni za kufanya maziko , kama black felix funeral services , kingdom blue coffins na king and queens ambayo ilitoa gari kwa ajili ya kuifuata maiti , utaratibu mzima wa kikampuni kwa wao ulikiukwa .
ukimsikiliza kiongozi wa south africa anayeshughulika na maswala ya kudhalilishana kiroho ( movement against abuses in church.) ndugu solomon izang ashoms , yeye anadai si mara ya kwanza kanisa hili linaletwa katika tuhuma mbalimbali ,,, aliulizwa ulichukua hatua gani ulichukua ,,, akadai nilitishiwa maisha . point ni kwamba wanataka kumkandamiza mwenye kanisa , alpha likau ,,, angalia Bushiri anapopitia leo , ,anatuhumiwa kutorosha fedha kwenda malawi ,,, mahojiano na uchunguzi unavyoendelea yote ni ubabaishaji ,,, mfano eti unahoji kuwa , chanzo chako cha fedha ni kipi hasa ,,, jamaa anawaambia , nina bishara za forex nk .... serikali inataka kuwafukuza wageni wenye power ya kiuchumi nchini south africa .

ni kweli serikali kwa mujibu wa taratibu lazima waamue , utaratibu nafuatwa na heshima ya nchi inakuwepo .. na ndiyo maana south africa kuna taasisi nyingi zinaangalia haya makanisa na kodi za serikali zinalipwa kupitia makanisa haya .

kwa muujiza huu .... ukweli utaadhirika ila bado na simama na Alpha lukau .. Mungu atampigania . south africa imekuwa ni sehemu hatari sana kwa watumishi wa Mungu ... hili ni jaribu kwa viwango vyake atavuka tu ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni wakati wa serikali kuingilia kati huu uhalifu unaofanyika makanisani Kwa kuwanyonga hao mitume feki na hao wanao dai kufufua wafu wakamatwe na kupelekwa mochwari wakichindwa kufufua wanyonge tu hakuna namna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom