Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,854
AFRIKA KUNA MATATA.
1)nawaambia wenyeji,wenyeji wa bara hili
Wenye nusu ya uchaji,tena waso wa bahali.
Walojawa ufujaji,wala wao hawajali.
Nimeuchoka uongo,Afrika kuna matata.
2)machafuko kila pala,vita vi kila mahali.
Sisi mamba wao ngala,kama hatuna akili.
Usingizi tumelala,wala hatuwazi mbali.
Nimeuchoka uongo,Afrika kuna matata.
3)tunauza bei ya che,za kwetu rasilimali.
Twalala hadi kukuche,tukiona ufahali.
Wao wakuwa vicheche,wanatukaba kabali.
Nimeuchoka uongo,Afrika kuna matata.
4)kutwa twapigana vita,kama vile majahili.
Wao wajenga ukuta,hayatuchezi machali.
Subiri yakitukuta,wakishika panga kali.
Nimeuchoka uongo,Afrika kuna matata.
5)utamu wa bara letu,wawaleta toka mbali.
Wajua akili zetu,zimeshafungwa kufuli.
Za kwao zisije kwetu,vyetu wapeleke mbali ?
Nimeuchoka uongo,Afrika kuna matata.
Shairi=Afrika kuna matata.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.