Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,193
- 3,011
Sasa si unaona matatizo yenyewe ya maendeleo yalipo i too totally agree with you hapa.
Umeona mfano mwingine huu wa 'kilimo kwanza' majuzi tu tumeletewa post za wizi wa mbolea wenye gharama za mabillioni, bila ya kurudia key problems ambazo might arise ulizozileta. Inaonesha ni jinsi gani mambo yalivyoanza kiuolela holela bila ya mipango, kujua ufatiliaji wake, kuhakikisha its not a failure and limiting foul play wao washaanza kuwekeza. Kwa upande wangu hii ni demonstration ya kuwa hii ni moja ya mikakati mingi ambayo aijakua throughly thought, bali ni kubahatisha tu.
Dunia ya leo aiitaji tena mwendo huo na bila ya hawa wasomi wetu kui-guide serikali ipasavyo na right strategies and policies huu umaskini wetu ni wa muda mrefu kwani mzungu awezi kuja kutufanyia research kwenye kila kitu mwisho tuige. Inabidi tuanze kujinyanyua wenyewe na wasomi wetu na sio raisi wetu pamoja na waziri mkuu wake kushtuka shtuka ugenini na kulilia wawekezaji sehemu ambazo tunaweza fanya wenyewe kukizi mahitaji ya watanzania ambao wapo disadvantaged.
Sio kila kitu kitoke nje vingine vyenye manufaa yetu itatulazimu tujifanyie wenyewe na tujifunze kujipangia wenyewe, after all we are responsible na maendeleo ya nchi yetu hivyo tunahitaji wasomi watakao tuletea haya maendeleo na kazi zao kinyumbani tu.
Br. Juma,
Umeaongea suala muhimu la utafiti kuwa sustainable. Kupiga hatua ktk maendeleo ya kiuchumi na kijamii, lazima system tunazoziadopt ziwe sustainable. Sasa kwa mwendo wa kusubiria tafiti zifadhiliwe na wageni ni wazi hatuezi fika popote. We have to find the way to finance our own projects, hiyo ni must do. Lazima kuwepo na continuity ktk mipango ya taifa. Hili tatizo sugu kabisa hata kwenye miradi ya kawaida ya kiserikali, achilia mbali hilo changa la m,acho la 'kilimo kwanza'..hamna continuity wala mipango ya muda mrefu.
Suala jingine ambalo nimeliona ni kikwazo na tatizo kubwa, ni muunganiko au tuseme ushirikiano baina ya watafiti na organs nyingine ktk jamii ambazo zinapaswa kutumia hizo tafiti in practicality. It is a shame tafiti nyingi zinafanywa kwa kutumia pesa nyingi na kuishia kuekwa kwenye makabati na kuishia kuliwa na panya na kukojolewa na mende. Hata ukitizama miundo ya wizara zetu, hakuna initiative ya kuona links za watafiti na watengeza sera. Na mbaya zaidi hali halisi ya sasa ya serikali kutojishughulisha na chochote zaidi ya ukuwadi.