African varsities pathetic in academic publications` | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

African varsities pathetic in academic publications`

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by pareto 8020, Apr 19, 2010.

 1. p

  pareto 8020 Member

  #1
  Apr 19, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  By Ani Jozen
  13th April 2010
  "African universities produce roughly one percent of academic titles issued annually around the world, a prominent local publisher said yesterday.
  Launching close to 40 publications of the College of Arts and Social Sciences (CASS) at the University of Dar es Salaam on the occasion of Mwalimu Nyerere Intellectual Festival Week, publisher Walter Bgoya said the situation of academic publications in Africa was ‘pathetic"


  Wiki iliyopita ilitoka article kwenye Guardian kuhusu wataalam wetu wa vyuo vikuu kuwa nyuma katika masuala ya publications.
  Tathmini hiyo ni sahihi kabisa, kwani ukitizama Journals na Articles zinazotambulika kimataifa, ni vigumu sana kukuta publications za wanataaluma wetu.
  Tatizo la msingi linalowakabili nadhani ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kufanya utafiti ambao utapelekea kutoa publications.

  Tanzania kama ilivyo nchi nyingi za Afrika haijawa na bajeti ya kukidhi tafiti nyingi zenye kulenga kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili kama nchi katika sekta za sayansi na maendeleo kwa ujumla. Ukiangalia tafiti nyingi zinazofanywa na vyuo vyetu, zinakuwa Foreign Funded.
  Na ukweli ni kwamba hawa Foreigners wanapofadhili utafiti, huwa na objectives zao wenyewe, na wala sio kutukwamua sisi na matatizo yetu. Na mara nyingi mwisho wa tafiti hizo, publications zinazotoka, authors wa kitanzania wanakuwa sio lead authors….utakuta ni author wa 6….na kuendelea

  Kwa mtazamo wangu, ni lazima, SERIKALI za AFRIKA kufanya commitment ya kufinance RESEARCH za wanataaluma wake kwa malengo ya kutatua CHANGAMOTO zinazotukabili….

  KWa nchi zilizoendelea, serikali na makampuni, yanawekeza sana katika research..sisi lazima, tufuate nyayo hizo…hivyo ndivyo INDIA na CHINA, zimejikwamua…..hivi sasa wenzetu hawaongelei kuwa source ya cheap labour pekee, bali wanaongoza katika research na innovation zenye lengo la kumsaidia mwananchi…ndio maana leo TATA….wameweza kuunda gari jipya linalouzwa kwa bei ya chini kuliko gari lolote duniani NANO-USD 3000….na ndio maana leo hii HUWAWEI ya China ndio inaongoza katika kutoa teknolojia za mawasiliano duniani.
  Katika kufanya utafiti nilikuta habari njema kwamba TZ, imeamua kutenga 1% ya GDP kwa ajili ya utafiti: Angalia extract ya budget speech ya mwaka jana:

  ·
  1. Shughuli za Utafiti na Maendeleo (Research and Development (R&D) kutengewa kiasi cha angalau asilimia 1.0 ya pato la Taifa GDP.

  1. Mheshimiwa Spika, Serikali ilifanya maamuzi tarehe 17/2/2009 ya kutenga asilimia 1 ya pato la Taifa kwa ajili ya Utafiti na Maendeleo (Research and Development). Asilimia 1 ya pato la Taifa kwa sasa inakadiriwa kufikia kiasi cha Shs. billioni 311.
  Lakini cha kushangaza ukisoma mpaka mwisho wa hotuba, utaona hizo fedha haziko reflected popote pale, sio kwenye wizara ya sayansi wala kwnye wizara ya elimu……….ANAGALIA

  H: MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2009/2010
  1. Mheshimiwa Spika, ili kuwezesha Wizara yangu kutekeleza mipango iliyojiwekea katika mwaka wa fedha 2009/2010, sasa naliomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya Sh. 38,677,630,000. Kati ya fedha hizo Sh. 24,267,464,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, yaani mishahara na matumizi mengineyo, na Sh 14,410,166,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
  Kwa upande wa fedha za Maendeleo, fedha za ndani ni kiasi cha Shs 13,962,842,000 na fedha za nje ni kiasi cha Shs 447,324,000.

  1. Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa napenda kukushukuru wewe binafsi, Naibu Spika, wenye viti wa Bunge pamoja na Bunge lako Tukufu kwa kunisikiliza wakati nikiwasilisha hotuba yangu. Aidha, hotuba hii itapatikana katika tovuti ya Wizara ambayo ni www.mst.go.tz
  2. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

  WIZARA YA ELIMU
  155. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo haya, sasa naliomba Bunge lako Tukufu lituwezeshe kutekeleza hayo yote niliyoyaeleza kwa kupitisha makadirio ya matumizi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo
  ya Ufundi ya Jumla ya Shilingi 507,492,983,000 kwa mwaka wa fedha 2009/2010 kama ifuatavyo:

  (a) Shilingi 377,691,167,000 zinaombwa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambapo Shilingi 153,249,075,200 zinaombwa kwa ajili ya Malipo ya mishahara
  na Shilingi 224,442,091,800 zinaombwa kwa ajili ya Matumizi Mengineyo; na

  (b) Shilingi 129,801,816,000 zinaombwa kwa ajili ya Mipango ya Maendeleo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
  156. Mheshimiwa Spika, nakushukuru wewe pamoja na Waheshimiwa Wabunge Wote kwa kunisikiliza.

  157. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.


  We need to be serious about it, hata kama RESEARCH and DEVELOPMENT zimetushinda..basi walau tuanze na COPY and ADOPT
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Pamoja na hayo kuna matokeo mengi ya tafiti zetu hayachapishwi. Wahadhiri wengine wanapata hata uprofesa bila kuchapisha makala za maana kwenye majalida ya kimataifa. Kwa hiyo kunakuwa hakuna pia motisha wa kuchapisha kazi zao. Hata hivyo kizazi kipya kilichoajiriwa hivi karibu kinakabiliwa na hatari zaidi kwani sasa kila kitu ni biashara tu. Wanatafuta pesa kwa kwenda mbele!
   
 3. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwani huwa huoni humu ndani ya JF sometimes inakujaga hile post ya MKUKUTA eti wanaionaje wana JF as kuna ma-mesiah humu ndani. Kama hawakuona umuhimu wa kupeleka wasomi wao wawafanyie tafiti na kuomba strategic ya development dont expect any money to go on the innovative side of things anytime sooner.

  Seriously body muhimu kama MKUKUTA ulitegemea hao wasomi wetu wa 'sayansi ya jamii' wameshafanya ma study kuchunguza nini vyanzo na nini kina hitajika na jinsi ya kuanza kutatua. Hivyo MKUKUTA inajijua inaelekea wapi na kujipanga vipi kimatumizi kutokana na budget yao na serikali inashauriwa vipi widhara zingine zicheze part zao.

  Wao ndio kwanza eti wana JF nao wachangie ushauri utachangia nini iwapo ujui what is really going on in the ground, in the first place. Matatizo ya umaskini 'Mmburahati' tofauti na kijijini kwetu 'Nyabula'. Wote wanahali sawa likini different appraoches are needed in helping them. Wangekua na tafiti nadhani wangejua where to start sio kupoteza budget kubahatisha tu no wonder some refer to the project as a waste of resources.
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Nadhani suala muhimu sio ku-publish per se. Suala muhimu ninavoona ni kuweka misingi mizuri ya kufanya tafiti na kujua wengine duniani wanafanya nini. Vyuo vingi vya kiafrika havina access na publishers wengi wa kimataifa na vitabu kueza kusoma kazi za wengine. Kutokuwa na references za maana ni tatizo kubwa sana. Ukitaka kujua ukubwa wa tatizo fungua tafiti yeyote iliofanywa Tanzania halafu angalia upande wa references uone vituko. Tusipoeza kujua wengine wanafanya nini ni vigumu sana kueza kuwafikia ktk medani za utafiti.
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  ku publish kunaweza pia kutumiwa kama moja ya njia ya kujitangaza duniani.
  kwa vile vyuo vya kwetu havi publish kitu, hata kupata joint research projects inakuwa tabu, coz haijuulikani nani anaefanya research kama ile kwa tanzania.
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu katika mambo ya taaluma (academics) na utafiti (research) hakuna kitu kama hicho. Kuchapisha taarifa za utafiti ni muhimu sana. Kuna hata msemo unaosema kuwa "in research you either publish or perish". Kwa hiyo huwezi kufanya tafiti halafu ukakalia matokeo. Pia huwezi kuwa mwanazuoni asiyepublish!
  Waafrika sasa wana nafasi ya kupata published papers zaidi kuliko kama miaka 5 iliyopita. Kuna sources nyingi sana. Kwanza kuna free online journals na pia kuna mitandao miningi sana ambayo inawapatia fursa watu kutoka nchi masikini kuona na kutumia paper mbali mbali hata za miaka ya 70 na 80 (mfano, HINARI (http://www.who.int/hinari/en/).

  Hapo kwenye blue, naona unaongea ki-jumla jumla. Kama utapenda basi wasiliana nami nikupatie papers ambazo zimetolewa na Watanzania kama first authors an zina reference za kutosha. Kama una mifano ya papers zenye upungufu wa reference na zimetoka kwenye journals za maana basi naomba unitumie nakala. Na kama hiyo imetokea basi hiyo journal nayo ina matatizo!

  Kweli mkuu, hiyo ni mojawapo ya faida za ku-publish.
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi ile DUP (Dar es Salaam University Press) ipo? Na inenda sawa na malengo yaliyowekwa ilipoanzishwa? Au ni sehemu ya kupigia photocopy tu? Halafu je Tumaini, St. Augustine, KCMC, Bugando wanazo university presses. Just curios!!!!!!!!
   
 8. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135

  Mkuu hapo nakubaliana na wewe na pia napingana na wewe, OK its fine kutaka kujua wenzetu wapo wapi na ina tegemea tunataka kufanya research ya nini?. Kama ni kutaka kujua how a theory on poverty can be explained in terms of our social structure, ok we can imitate some of the psychology associated with it and the basic factors to poverty.

  Lakini there's no point of any Tanzanian academic kwenda kutaka kujua how to work out the best way to improve the lives of people living in urban or rural areas in Tanzania. Knowing he has already aquired the reasoning lines to formulate his own home theory for the benefit of us Tanzanians and the work be a future refference to up and coming scholars in the field.

  Hapa mi naona ndio tatizo, it seems we are trying to escape showing our own talents, and understanding where are we getting it wrong. Hiving said that now it makes alot of sense when our president not long ago declared he's not sure why we are in poverty and why he insists on this EAC believing it is some part of the solution in reducing poverty.

  Nimeingia maktaba nimekuta kitabu cha sociology from a south african scholar kina zungumzia social problems za south africa using western lines of reasoning but south africans refference books or western scholars who have done other reseaches there for evidence ni wapi kwingine in africa umeona kitabu kama hiki. Kwa maana hiyo future south african scholars wataendelea kuendeleza the trend na itakuwa the key so long as they get the right reasoning lines.

  Sasa why does a social-ecomic scholar needs to get a refference from a western scholar just to conduct his research on abuse of power given to the president and the ineffetiveness it causes on the chain of command. Au how to implent a policy that would forsee the long term of ignorance in tanzania or suggesting ways to the government to encourage entrepreneurship in tanzania. na kama wapo waliofanya hizi research au za design hiz kwa nini hawaziweki public tukaziona.
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ninachosema ni kuwa tatizo pekee si tu ku-publish. Ndio maana ya neno per se..yaani kuna matatizodada ambayo nayo ni muhimu kuyatatua sambamba na hilo la kuchapisha kazi zetu ktk journals za kilimwengu au makongamano ya kisomi ya kilimwengu. Huezi ukapublish ktk this competitive world pasi na kuwa na misingi iliojengeka ya ki-research. Huezi ukategemea vinginevo as simple as that.

  Huezi ukafanya research zilizoshiba bila kuwa na backrgriound ya kutosha, na huezi ukawa na background ya kutosha bila ya kuwa na vitabu vya rejea na availability nzuri ya papers. Kumbuka kuwa papers nyingi zinauzwa online and u will be lucky if u find public domained-papers, na kupata hard copies ya journals ili watu wengi wafaidike kwa wakati mmoja ni muhali esp. kwenye ishu za copyright, ndio maana vyuo vya dunia ya kwanza vinalipia hizi huduma na kila researcher au mwanafunzi anaeza ku-access kutoka ktk PC yake.

  Tatizo la kupata rejea ktk vyuo vyetu ni KUBWA SANA. Kumbuka kwamba kuna reseraches (sio zote) ambazo zinahitaji theoretical background ili researcher aongeze kitu kipya, sasa huezi ukaepa hicho kihunzi bila ya kuwa na nyenzo za kujijuza. Kaa huongezi kitu kipya kwenye disciplines, research zetu haziwezi kuwa published kwenye journals za 'kilimwengu', vitaishia kukuhuku chinichini na nobody will take us seriously.
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu sina hakika kama haya mambo ya utafitia unayajua kiasi gani. Nimesema kuwa kuna journals nyingi sasa ni free online, lakini pia kuna nyingine nyingi ambazo zinatolewa bure kwa watu wanaotoka kwenye nchi zinazoendelea. Kwa hiyo uhabada wa taarifa siyo tatizo kubwa kwa sasa kama unavyosema.

  Pia nikueleze kuwa kuna tafiti nzuri tu za Watanzania (achia mbali Waafrika wengine) zimetoka kwenye journals kubwa sana duniani kama Nature au Science. Kama unapenda basi tuwasiliane nikupatie nakala. Pia unaweza kwenye kwenye net ukatafuta (mfano google professional au pubmed).
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Sizungumziii taarifa pekee, nazungumzia credible source of info ambayo unaeza kui-cite kitu with confidence mbele ya wanataaluma wenzako. Unaongea na mtu aliepata degree kwenye vyuo vya kiafrika pia aliyepata changamoto sana kufanya research ktk mazingira hayo duni. Kwa sasa hivi siwezi jua hali halisi ya upatikanaji wa journals na vitabu ukoje ktk vyuo, lakini ni wazi naweza kupredict kwa kutumia hali niliyoishuhudia in those good old days. Matatizo ya ukosefu wa marejeo yanafit research yalikuwa makubwa sana na nachelea ktk nchi yetu kaa yetu na jinsi wanavoongeza intake bila kuangalia nyenzo zinazokidhi haja, nadhani hali inaeza hata kuwa mbaya zaidi.
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Hapo kwenye red, taarifa ni kuwa published papers kwa sasa siyo tatizo. Unaweza kupata zaidi ya 50% ya papers unazohitaji. Kwa hiyo hakuna sababu ya kuwa na wasi wasi na hilo. Shida yetu kubwa ni serikali kutotoa pesa za utafiti. Kwa hiyo kazi zetu nyingi zinategemea pesa za nje. Hata hivyo katika dunia ya utafiti pesa kutoka nje ni muhimu sana kwa utafiti. Ila kama tunengekuwa na pesa za ndani basi tungeweza kuamua nini kifanyike.
   
 13. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Mkuu DC, habari ya siku?

  nakubaliana na Abdulhalim kwa updande mmoja...manake ni chuo kipi hapa nchini unazungumzia ambapo unaweza kupata 50% ya marejeo?

  Ukizungumzia free onine journals, hapo ina maana uweze kuaccess..ni vyuo vingapi vina reliable, fast and available internet services, acha kwa wanafunzi tu, lakini hata kwa wahadhiri?

  Vitabu vingi vilivyopo maktaba, including journals, vimepitwa na wakati, vya miaka ya 70,80, na mwanzoni wa miaka ya 90, sasa unakuta utafiri umeshaenda mbali sana in a soace of one year. Na kama alivosema Abdulhalim inakubidi uwe na taarifa za kutosha kabisa kabla hujaamua kuchapisha chochote kipaya kuchangia sekta ya utafiti.

  Ukiongeza suala la kwamba hakuna fedha za kufanyia utafiti, watafiti wengi wameamua kujiingiza kwenye shughuli za consultancies tu ili kusubsidise mishahara midogo wanayopata..muda wa kupablish hakuna...ndo maana hawaonekani ki ivyo kama wenzetu wa dunia ya kwanza.
   
 14. F

  Felister JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2010
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sijui kama conditions in academia ya Tanzania inaeleweka na wengi. Utakuta some universities hata access tu ya internet ni miracle na ikipatikana ilivyo slow haielezeki, licha ya hayo research funds ndo usiseme ni hadith ya abunuasi, strategic human resources development ni almost zero tuna fanya gambling tu scholarship inayopatikana ni hewala. Analysis zetu ni very shallow kutokana na ukosefu wa proper training na abscence ya uptodate hard and softwares. Data base zetu hazina kichwa wala miguu because of poor recording and inconsistency. Sasa chapisho zenye akili zitatoka wapi? Mtu una tegemea data za historical events na kumbukumbu ya respondents. Hata research nyingi zinafuata imfrastructure development so hazitoi picha halisi ya nchi. Ukitaka fanya scrutiny ya haraka haraka uone sampling frame zinahusisha maeneo yapi kama si yale tu yaliyokaribu na barabara hasa kwa socio-economic researches. Wananchi wa maeneo hayo nao wananifurahisha wamegundua njia nzuri ya kujireward kwani hawaoni connection kati ya research na development so hakupi responce mpaka umlipe kwanza, kiwango itategemea how frequent hilo eneo limetembelewa na ni watu waaina gani wamelitembelea, kama international NGOs basi kazi unayo dau liko juu.


  Maprofesor wengi wamezeekea ofisini na hawataki kurithisha taaluma zao kwa juniors kwasababu tu ya hofu ya life after office so no sharing of resources akipata any resource basi MKUKUTA binafsi kwanza. Mifuko nayo ya social security haioni hata aibu ya kumpa mtu aliye dedicate life time yake kwenye kufundisha na research kiwango hata pengine kinachozidiwa kwa mbali na mtu ambaye hafikii hata robo ya rank ya huyo profesor. No labour specialization, no objective rewarding of professionals no nothing imebakia tu shagala bagala...Huyo huyo mtu ni profesor, mfuga kuku, mkulima, muuza duka, mwansiasa atachapisha saa ngapi hizo articles?

  Hakuna kitu kigumu kama academics if you are serious on it. Unatakiwa usome almost all hours kupreuse huku na kule kupata recent informations na technologies...Na ukifanya hivyo ndugu yangu na condition ya Bongo ilivyo haichukui hata mwaka nywele zote zimekua nyeupe na data nyingi tu zime futika kichwani yaani mtu una muuliza jina lake yeye anaamua kupiga simu kumuuliza secretary eeeh hivi jina langu ni nani et? Acha mchezo nimekutana na si chini ya 3 profesors ambao hard disc zao zimesha futa memory nyingi za maisha ya kawaida na wengine wengi ambao wamesha pata mara nyingi tu blackouts. Ukiwachunguza ndo hao ambao wana machapisho ya maana kwenye reputable journals.

  Our leaders have to come back to their senses as no development would result from Africa bila kuwa serious on academic issues. Politic is just a development lubricant and never will it be a leading force to the development issues.
   
 15. p

  pareto 8020 Member

  #15
  Apr 20, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na hoja ya Felister, kwamba si rahisi kupata maendeleo bila kuwa makini katika masuala ya utafiti na uvumbuzi na masuala ya taaluma kwa ujumla.

  Sina uhakika kwamba katika mipango yetu ya maendeleo, component ya utafiti na matumizi ya matokeo ya utafiti inakuwa factored in. Kwa mfano sasa huu mkakati wa KILIMO KWANZA, sijui kama ume take on board component ya research…. Kwa sasa emphasis imewekwa zaidi kwenye kupata resources za ku mechanize agriculture-mikopo ya kununua matrekta, upatikanaji wa mbolea etc lakini sijui kama kumekuwa na any reference ya matokeo ya utafiti wa kisayasi wa tathmini ya mazao yapi yanafaa kulimwa wapi, mbinu zipi zinaweza kutumika kuboresha uzailishaji, teknolojia za aina gani zinaweza kufaa kwa mazingira ya kwetu (hasa vijijini ambapo hakuna nishati ya umeme), mbegu zipi zinaweza kuzalishwa kwa urahisi katika sehemu karibu na mashamba…
  It will be a great mistake, kama mpango wa kilimo kwanza haujaziusisha taasisi za utafiti wa kilimo za nchini kama Uyole etc.. Na pia ni muhimu kujifunza kwa nchi marafiki ambazo zimepiga hatua kubwa kama vile Brazil (utafiti wa kisayansi wa kilimo cha uzalishaji), India (utafiti wa kutengeneza vitendea kazi vya kilimo vilivyo affordable na practical katika mazingira ya nchi masikini) na Malawi (ambao wameweza kufanya mapinduzi ya kilimo- kutoka nchi omba omba ya chakula mpaka kuwa nchi inayo export chakula baada ya kuwatosheleza wananchi wake) angalia http://www.independent.co.uk/news/world/africa/malawis-farming-revolution-sets-the-pace-in-africa-821135.html.

  Sisi Tanzania tuna kila kitu…..tunao watu (80 percent ya watanzania wanaojishughulisha na kilimo; wanasayansi, vyuo vya utafiti (SUA, UYOLE etc), Ardhi tele, Maji Tele….All we need ni ku consolidate hizi resources ili kurevolutionalize kilimo chetu- inawezekana
   
 16. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sasa si unaona matatizo yenyewe ya maendeleo yalipo i too totally agree with you hapa.

  Umeona mfano mwingine huu wa 'kilimo kwanza' majuzi tu tumeletewa post za wizi wa mbolea wenye gharama za mabillioni, bila ya kurudia key problems ambazo might arise ulizozileta. Inaonesha ni jinsi gani mambo yalivyoanza kiuolela holela bila ya mipango, kujua ufatiliaji wake, kuhakikisha its not a failure and limiting foul play wao washaanza kuwekeza. Kwa upande wangu hii ni demonstration ya kuwa hii ni moja ya mikakati mingi ambayo aijakua throughly thought, bali ni kubahatisha tu.

  Dunia ya leo aiitaji tena mwendo huo na bila ya hawa wasomi wetu kui-guide serikali ipasavyo na right strategies and policies huu umaskini wetu ni wa muda mrefu kwani mzungu awezi kuja kutufanyia research kwenye kila kitu mwisho tuige. Inabidi tuanze kujinyanyua wenyewe na wasomi wetu na sio raisi wetu pamoja na waziri mkuu wake kushtuka shtuka ugenini na kulilia wawekezaji sehemu ambazo tunaweza fanya wenyewe kukizi mahitaji ya watanzania ambao wapo disadvantaged.

  Sio kila kitu kitoke nje vingine vyenye manufaa yetu itatulazimu tujifanyie wenyewe na tujifunze kujipangia wenyewe, after all we are responsible na maendeleo ya nchi yetu hivyo tunahitaji wasomi watakao tuletea haya maendeleo na kazi zao kinyumbani tu.
   
 17. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #17
  Apr 20, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,867
  Trophy Points: 280

  wote waliotoa maada kwenye hii thread tumejengana, ili swala la kupata hayo material ni sawa na kuvuka kigamboni kwa mguu!

  UDSM? you can not believe ni moja ya vyuo vibovu kabisa linapokuja swala la kutafuta journals, hawana kabisa connections na hizo journals, kama sciencedirect au springerlink. Vyuovya wenzetu mtandao ukishakuwa wa chuo huna haja kusumbuka you just download papers utakavyo!

  Tuapoilaumu serikali lakini lazima hivi vyuo viwe vimejitayarisha, professors kutumia madesa ya mwaka 80, kuto wapa wanafunzi papers ni aibu!
   
 18. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Waafrika ni wavivu tu, ukishakuwa na Ph.D unalizika kabisa wanaojishughurisha ni wachache. Hizo fedha zinazotoka nje kwa ajili ya research wanazishugurikia mara nyingi si kwa malengo ya research bali kwa malengo ya ujira.

  ni sawa na wabunge wetu tu hawaendi mle bungeni kwa ajili ya kuwakirisha watu ,bali kwa ajili ya ujira.Serikali yetu inalitambua vizuri sana hili na hata mie ninaiunga mkono serikali ,hakuna haja kwa hali iliyopo sasa.
   
 19. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2010
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Hakuna database yoyote ya maana ambayo unaweza kupata access for free! It's a must kwa vyuo vyetu vitenge fedha na ku-subscribe hizi databases, including Web of Science, Scopus and the likes. Ni vigumu mno kuja na utafiti "innovative research" bila kujua wengine wanafanya nini katika eneo unalolifanyia kazi [Information gap]. Kimsingi, watu watatilia shaka utafiti ambao haukuzingatia "current level of knowledge" wa suala husika. Huwezi kutegemea wikipedia pekee. I am not even sure if you can cite wikipedia and expect your research to feature in leading peer reviewed journals. Hili suala ni muhimu mno. Utakuta chuo kinatumia milioni 80 kununua gari la mkuu wa chuo, wakati huo huo hawana fedha za ku-subscribe hizi databases. Ni shida!
   
 20. B

  Bibi Kizee JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu DC hili bado ni tatizo, binafsi huwa inaniwia ngumu mno kama nitaamua kuandika nikiwa Tz bado journal nyingi zinahitaji kulipia, napata nafuu kwa kuwa ninawatu wa nje ninaofanya nao kazi na hunisaidia mno, lakini kwa kutegemea resources za nyumbani hata nikiwa Mlimani ambapo kuna baadhi ya journal tunapewa free bado. nadhani inatakiwa fedha zinazotengwa kwa ajili ya tafiti au kuendeleza vyuo pia zitenge fungu kwa ajili ya kulipia open access ya some journals na pengine wawe wanaupdate mara kwa mara ili kuenda sambamba na ukuaji wa database za kimataifa.

  kingine pia ni pamoja na level ya research zetu ni ngumu mno kupublish kwenye international journal or high ranked journals tunaishia kwenye local or regional journals ambazo pengine hata uki-google huwezi zipata kwahiyo katika ni ngumu mno kuwa ranked kwa hili, hizi zinasaidia tu humu ndani watu kupanda na kuwa maprofessor.
   
Loading...