African Millionaires: Ali Mufuruki

Utajiri wa mfuruki kwa kiasi kikubwa uemechangiwa na balozi ami mpungwe...na ndio business partner wake,aliyoyafanya ami mpungwe kwenye mashirika yetu ya umma na madini yetu akishirikiana na makaburu kipindi cha mkapa ndio matokeo yake kuibuka kwa bwana mufuruki!
Aisee naona kuna ukweli huyu Mpungwe ni mwenyekiti kwenye makampuni mengi yenye asili ya Afrika Kusini ,inaonekana yeye badala ya kutuwakilisha yeye akawa anajiwakilisha,hata ukiangalia Mufuruki kwa sasa ndie msimamizi wa makampuni mengi yenye mizizi ya kutoka SA,kumbe nyuma yake yupo Ami du haya ngoja nikapige mbizi Kivukoni nijirudie zangu Kigamboni
 
Natamani sana kujua historia yake,Ali Mafuruki katokea wapi,ujasiriali kauanza lini?maana mi ananikonga sana kwenye vipindi vya Televisheni namna anavyojua kujenga hoja.Mfano,ni kama wiki mbili zimepita kwenye kipindi cha This week persepective cha Adam Simbeye TBC1 wakiongelea shilingi kushuka thamani, mbele ya kamishna wa BOT na katibu hazina (huyu jamaa alikuwa TASAF kabla),Ali alisema serikali ndo inaongoza kwa kufanya manunuzi kwa kutumia dola.

Akasema ukienda mlimani city baadhi ya maduka vitu vinauzwa kwa dola na bei zimebandikwa kwa dola,nyumba ufukweni zinapangishwa kwa dola akasema hiyo kitu ni kosa na kuwa serikali inayajua hayo lakini haichukui hatua,ushauri wake wa kuwa heshima kwa shilingi yetu uanzie serikalini niliuona wa maana sana.

Ali ni nani hasa huyu?
Hata mimi nilikiangalia kipindi hicho jamaa kwa kweli alinokosha kwa hoja zake kuhusu matumizi ya dola,akatoa na mifano ya India nei a SA,nilifurahi alipompinga yule jamaa wa Benki Kuu aliyesema eti ni kosa kama mnunuzi wa vitu atalazimishwa kununua vitu kwa dola,lakini Bw Ali alisema huko India au SA ukienda na dola dukani unaambiwa nenda bureau au benki ukabadilishe halafu ndio ununue vitu,kwa maana nyingine alikuwa anatueleza kuwa katika nchi hizo hata hapo jirani Kenya huwezi ukakuta duka limeweka bei ya vitu vyake dola.Pia ni mtu anayeenda na wakati yeye alikuwa na tablet wakati wenzie walienda mikono mitupu na mikaratasi
 
attachment.php


He is one of the most successful businessman in the country at the 40 years

Umri wake ni late 50's kati ya 57 na 59. Kuna thread nyingi juu yake humu unaweza kupitia lakini hayo ya ufisadi mtakuwa mnamzushia.

https://www.jamiiforums.com/celebri...airman-and-ceo-infotech-investment-group.html

https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/46108-african-millionaires-ali-mufuruki.html

https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/170843-ali-mufuruki.html
 
Katika orodha ya mabilionea watano waliotajwa hapa nchini tanzania; wa kwanza ni Said Salim Bakhressa $620 milioni, wapili Gulam Dewji $560 milion, watatu Rostam Aziz $420 milioni, wanne Reginald Mengi $280 milioni na watano ni Ali Mufuruki $110 milion, je huyu Mufuruki ni nani? ni mara ya kwanza kusikia jina lake, na je wanajanvi kuna mtu anayejua historia yao? Jamani naomba tujuzane.
 
Ali Mufuriki, Mmiliki wa maduka ya nguo maarufu kama Woolworth, hapa Tanzania na Uganda. Pia mwanahisa wa kampuni tanzu ya Woolworth Africa kwa asilimia 35, iliyoko nchini Africa kusini. Anamiliki pia kampuni ya Infotech, pamoja na pay Tv mpya mjini ya Zuku. Ni moja ya nyota njema zinazochipukia Tanzania.
 
jamaa ni kichwa ... mmiliki wa infotech na mazaga zaga kibao

inaoneka huyu ni mtu creative sana, sijawaimsikia jina lake likitajwa kati ya matajiri wanao sikika sana hapa Tanzania,
 
Ali Mufuriki, Mmiliki wa maduka ya nguo maarufu kama Woolworth, hapa Tanzania na Uganda. Pia mwanahisa wa kampuni tanzu ya Woolworth Africa kwa asilimia 35, iliyoko nchini Africa kusini. Anamiliki pia kampuni ya Infotech, pamoja na pay Tv mpya mjini ya Zuku. Ni moja ya nyota njema zinazochipukia Tanzania.


Woolworth ndio awe na hela yote hiyo au kuna mambo yamejificha! Biashara ndogo hizo. yasije kuwa kama ya mhindi wa pembe za ndovu.
 
Woolworth ndio awe na hela yote hiyo au kuna mambo yamejificha! Biashara ndogo hizo. yasije kuwa kama ya mhindi wa pembe za ndovu.

kaka hizo ni njia za kujionyesha kuwa wana-vyanzo sahihi vya mapato ila kuna vitu vyao nyuma ya pazia...kwani r-aziz hatumjui anavyojipatia utajiri??...wekeni wazi vyanzo vya mabilioni yao ikiwamo kuua uchumi wa taifa letu kwa manufaa yao binafsi.
 
Ukifatilia kwa udani waliotajwa wanne wana vidoa vidoa, isipokuwa huyu Kafuruki nilikuwa sijawahi msikia. Je hana kashfa yoyote?
 
Woolworth ndio awe na hela yote hiyo au kuna mambo yamejificha! Biashara ndogo hizo. yasije kuwa kama ya mhindi wa pembe za ndovu.
Huyu jamaa ni Venture capitalist, yeye anawekeza ndani na nche ya nchi. Hawa waliofanya utafiti wa hizi takwimu hawakuweka wazi ni vigezo gani wametumia. Kwani kwa mpango huu hata Mzee Matonya alitakiwa awe kwenye list. Wamemsahau hata Legwanani wa Africa Mashariki?
 
Mfuruki ni Mjasiriamali wa siku nyingi sasa, M&M communication, kampuni ya wakala wa Matangazo it was once the leading company na bado inafanya vizuri.
Wadau natamani sana kujua wasifu wa Gulam Dewji, anafanya biashara gani mpaka awe na utajiri huo?
 
Mfuruki ni Mjasiriamali wa siku nyingi sasa, M&M communication, kampuni ya wakala wa Matangazo it was once the leading company na bado inafanya vizuri.
Wadau natamani sana kujua wasifu wa Gulam Dewji, anafanya biashara gani mpaka awe na utajiri huo?

Huyu ndie mmiliki wa makampuni ya Mohamed Enterprises, ni baba yake na Muhammed Dewji mbunge wa Singida mjini na Mkurugenzi wa Makampuni hayo.
 
Back
Top Bottom