Africa is my religion

Citizen B

JF-Expert Member
May 13, 2019
6,675
9,036
Naandika huu Uzi kwa majonzi baada ya kuona dada zetu wakichukuliwa nchi za Afrika kama Tanzania Kenya Uganda Sudan etc. Na kuchukuliwa wakipelekwa nchi mbalimbali wakiahidiwa kazi na makazi na wengine huenda kama wakimbizi wa nchi za north Africa wakienda kutafuta maisha ughaibuni.

Lakini wengi wamejikuta wakigeuzwa kuwa watumwa huko wafikako.

Kumekuwa na trend ya nchi za mashariki ya kati kuendeleza utumwa. Sababu hasahasa ikiwa ni ubaguzi dhidi ya waafrika na nyingine ni dini.

Cha ajabu kinachonitia majonzi zaidi ni pale muafrika huru kama mtanzania baadala ya kukemea vitendo hivyo huvitetea kwakuwa vinashabiriana na dini yake.

Utakuta mtanzania anafurahi kusikia watanzania wenzake wakiuzwa huko Oman kisa yeye huona hao wa'oman ni ndugu zake kidini na wako sahihi na wengine kwa unafiki zaidi ili kutetea dini yao hufumbia macho vitendo hivi na kuigiza kama havipo na kukana haiwezekani au kusema haihusiani na dini ili kuendelea kufumbia macho vitendo hivi.

Mimi pia nina dini lakini brothers dini inabadilika siyo ngozi yangu. So I am African first before I am Christian or Islam.
Hata nikiwa ughaibuni nikaambiwa nichague kati ya waafrika wapagani na wazungu waumini wenzangu mimi nitaenda kwa waafrika

We were same until religion separated us
We were equal until money classified us
We were alike until race segregated us
 
mtu kama magu akiwaponda majukwaani badala mumuunge mkono mashuleni na mitaani mansema mabeberu ndio wanafanya tuishi.

hawa watu wanatuchulia kwa thamani ndogo kuliko hata wanavyomchukulia mbuzi.maana sisu tuanaajiriana sisi kwa sisi wao kwanini wanafuata ndugu zetu,wasipeane wao kwa wao huo ulaji!!!
 
Heri umeliona hili,tuna ukengemfu tumesahau wote hao walitufanya kuwa watumwa kwa mijeledi na hivi sasa kwa ulaghai na wamefanikiwa!! Tatizo hivi sasa ni elimu na maisha,watu wanaenda huko kwasababu huku shida sana.. tupaimarishe huku kwanza pawe patamu huko wataenda Kama watalii na wafanyabiashara au wafanyakazi wa kuheshimiwa.
 
Tatizo la waafrika ni watu wa KUABUDU zaidi kuliko kutafuta uhalisia.

Wakati wote mwafrika anatafuta kitu/mtu wa kukiabudu/kumwabudu ili abwage matatizo yake hapo kihisia..huku kiuhalisia matatizo yakiwa bado yanamwandama.

Ndio maana dini na madhehebu yamefurika kila kukicha lakini umasikini unizidi siku hadi siku.
Kwa maana hiyo tutaendelea kuwaabudu waarabu na wazungu tukiwa na matarajio ya kupata ahaueni kimaisha..NI JADI YETU!
 
Me cha msingi nachokiona ni kujua kwanza chanzo cha tatizo kwanin wa Africa wenzetu wanakimbilia ughaibuni kwenda kuwa watumwa kuliko kukaa kwenye nchi zao.Wa Africa tuache ubinafsi maisha huku kwetu ni magumu ndo maana mtu anaona bora akawe mtumwa nje kuliko kupambana hapa Africa .kwanza viongozi wabadilike tunapowapa dhamana ya kutuongoza bas watende Yale yaliyo mema na kuendeleza bara letu . Angalia nchi nyingi za kiafrica japo tumepata Uhuru miaka 50s iliyopita lakin still maendeleo hakuna umasikini umekithiri ajira hakuna magonjwa kama malaria ,surua,Ebola kipindu pindu bado ni tatizo sasa kwanin watu wasione bora kuwa watumwa Asia na ulaya kuliko kukaa Africa .Viongozi wajitathimini kwanza.
 
Back
Top Bottom