Africa Cup of Nations (AFCON) 2017, Special thread

Mimi siku zote AFCON...Timu zangu ni Misri,Algeria,Morocco, ...hawa jamaa huwa nawakubali sana haswa Egypt....ukiacha waarabu huwa nawapenda Nigeria. ....ila michuano hii nitaanza na Uganda
 
Swadaqta l'akhy..hao walikua mashine si mchezo..

Misry ilikua inaheshimika mno,soka lao lilikua la kipekee sana Afrika...kwa sasa tunaiona Algeria ikishambulia zaidi mpaka mjerumani alitokwa jasho w/c...ngoja tuone AFCON ya mwaka huu itaamua vipi...
Hata hiyo Algeria alikuwepo miaka ya 80 mtaalam akiitwa mustapha rabah madjer huyo mtu alikuwa hodari sana enzi hizo kulikuwa na gazeti linatoka kwa mwezi linaitwa Africa now lilikuwa maarufu sana picha za rangi zilizo koza unamuona mtu kweli zamani acha iwe zamani
 
Al'akhi unakumbukumbu nzuri sana Mshllh, Algeria nimeanza kuifuatilia miaka sio mingi sana..ila nasikia miaka hiyo ilikuwa inatisha mno...

Kweli kila kitu na mwanzo wake na mwisho wake
 
Al'akhi unakumbukumbu nzuri sana Mshllh, Algeria nimeanza kuifuatilia miaka sio mingi sana..ila nasikia miaka hiyo ilikuwa inatisha mno...

Kweli kila kitu na mwanzo wake na mwisho wake
Ukanda huo ulikuwa na watu ila kiujumla africa ya kaskazini na pia magharibi walikuwa mbali kimpira Morocco ya kina mohamed timoumi na badou zaki huyu alikuwa nyanda mzuri sana magharibi ya kina upuku nti wa ghana na huku Cameroon ya kina thiofile abega huyu mpaka mchezaji wetu ramadhani lenny alibatizwa jina la abega kwa uhodari wa huyu jamaa so Africa vipaji vilikuwepo toka zamani .
Pana huyu selif keita traore wa mali ambae alienda ufaransa mwaka 1972 kujiunga na saint etienne na kisha vilabu vingine barani ulaya kama OM valencia na vingine huyu baada ya kustaafu alifungua academy ambayo seidou keita yule alie kuwa Barcelona ambae ni mpwa wake alijifunza mpira pale .
 
Swadaqta! Dah nimejifunza mengi kutoka kwako, nilikua siyajui yote haya,shukran aise
 
Ukanda mwingine ulikuwa afrika ya kati nayo ilikuwa timu moja ya Zaire mwaka wa 1974 walikuwa miamba kweli walitwaa mwali na kwenda world cup ila kilichotokea huko ni khatari walifungwa na yugoslavia bao 9 kundi lao wakiwa na brazil ambao waliifunga Zaire 3 na Scotland pia walifungwa Zaire 2 .
Cha ajabu walikuwa na mchezaji wao khatari sana pierre ndaye mulumba aliweka rekodi ya kufunga magoli mengi penye mchuano mmoja huo mwaka 74 sasa mwaka 94 yaani baada ya miaka 20 CAF wakamkumbuka na kumuita Tunisia achukue zawadi yake baadae karudi kwao huko majambazi wakamvamia na kumwambia kapewa zawadi na pesa akawajibu hana ila kunusuru roho yake akawapa Belgium francs 2000 jamaa wakasema anawatania wakampiga risasi ya mguu . Penye interview analalamika nchi nyingine watu kama yeye wana heshimiwa ila kwake imekuwa kinyume baadaye aliondoka na kwenda south Africa kama asylum seeker sijui aliishia wapi !
 
Hapa unajipa uzelendo tu usiokuwa nao naamini lazima kuna timu ya magharibu au north africa unaipenda.
Huwezi ipenda uganda mbele ya misri,algeria,morooco,cort de ivory, ghana,na nyingine nyingi
Ndugu yangu musolin5 ndio mapenzi yake yapo hapo kwa korongo inabidi tuyaheshimu jamani .
 
Karibuni,
Huu ni uzi maalumu kwa ajili ya AFCON 2017, Njooni tusemezane, Matokeo, news, n.k

Mbarikiwe!

Mkuu, ili kuboresha huu uzi nadhani itapendeza kama ukituwekea makundi ya timu shiriki.....
 
GROUP D
1be94be7215727acdba48057d8db468c.jpg
803300adf58cc1ae6442dfb10dc42a97.jpg
d689fd7f16c517d66e857042eb9edb50.jpg

c8336b1200525e8c6908ff47bcfff496.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Back
Top Bottom