Zeddicus
JF-Expert Member
- May 5, 2012
- 627
- 534
Najua wengi miongoni mwetu tutakuwa na ufahamu kuhusiana na huu utumishi adhimu kwa mustakabali wa usalama wa taifa lolote lile, kwa faida ya wale wasiofahamu kwa undani kidogo kuhusu huu utumishi nimewaletea makala kama ilivyoandikwa ktk blog ya Evarist Chahali.
Kuna ukweli mmoja usiofichika wala kupingika kwamba watu wengi sana wanapenda kazi ya ushushushu, yaani Uafisa Usalama wa Taifa. Hiyo sio kwa Tanzania pekee bali sehemu nyingi duniani. Ukiingia mtandaoni utakutana na watu wengi wanaozungumzia taaluma ya intelijensia au/na wahusika katika hali ya kutamani kuifahamu taaluma hiyo nyeti au kuwa mhusika.
Nitaanza mlolongo (series) wa makala kuhusu taaluma hiyo adimu. Hata hivyo ni vema nikatahadharisha mapema kwamba nitakachoandika ni kile tu kinachoruhusiwa kuandikwa hadharani. Kimsingi,taaluma ya ushushushu inatawaliwa na usiri,na mengi ya yanayohusiana na taaluma hayo yanabaki kuwa siri. Hata hivyo,kuna maelezo ambayo yapo wazi japo inahitaji uelewa wa aina flani kuchora mstari kati ya kipi ni siri na kipi ni ruksa kuwa hadharani.
Kwa tafsiri rahisi, ushushushu ni taaluma inayohusu ukusanyaji wa taarifa za kiusalama kwa njia za siri (clandestine methods). Japo kwa kiswahili ushushushu ni intelijensia, kiundani kuna tofauti kati ya ushushushu unaofanyika ndani ya nchi na unaofanyika nje ya nchi.
Kwa Uingereza, Idara ya ushushushu inayoshughulika na masuala ya ndani inajulikana kama MI5 na inayohusiska na ushushus nje ya nchi ni MI6.Kwa huko nyumbani, tofauti hizo zipo ndani ya muundo wa taasisi husika, kwa maana kwamba kuna taasisi moja tu lakini ndani yake kuna mgawanyo wa kimajukumu ya ndani na ya nje.
Kadhalika, japo mashushushu wamekuwa wakifahamika pia kama spies, ukweli ni kwamba spy ni shushushu anayefanya kazi nje ya nchi yake,kitu kinachojulikana kiusalama kama ujasusi au espionage kwa Kiingireza.
Japo mataifa mbalimbali yana miundo tofauti ya Idara zao za Usalama wa Taifa,lengo na kazi kuu ni ukusanyaji wa taarifa hizo.Kwa minajili ya makala hizi, nitazungumzia zaidi mazingira ya Tanzania.
Kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996, Idara yetu ya Usalama wa Taifa ni idara ya serikali iliyo chini ya Ofisi ya Rais,ambayo ina jukumu la kukusanya na kuchambua taarifa za usalama na kuziwasilisha 'mahala kunakohusika' katika namna ambayo Mkurugenzi Mkuu wa Idara hiyo ataona inafaa.
Kimsingi, mkuu'halisi' wa Idara hiyo ni Rais mwenyewe,ambaye kwa lugha ya kiusalama anafahamika kama 'sponsor.' Wakuu wa Idara za usalama popote pale duniani hufahamika kama spymaster. Maeneo makuu ya kazi za Idara ya Usalama wa Taifa ni kukusanya na kuchambua habari za kiusalama zinazohusiana na ujasusi (espionage),uzandiki (subversion),uhujumu (sabotage) na ugaidi (terrorism). Lakini jukumu la Idara hiyo si kukusanya taarifa hizo na kuzichambua tu bali pia kuzuwia matukio hayo yanayofahamika kama matishio ya usalama wa taifa.
Ni kwa vile utendaji wa kazi wa Idara yoyote ile ya Usalama wa Taifa unaegemea katika usiri mkubwa ndio maana kwa 'mtaani' kuna hisia tofauti kuhusu umuhimu wa taasisi hiyo. Ukweli ni kwamba laiti umma ungefahamu nini kinafanywa (au kinapaswa kufanywa) na Idara hiyo basi kwa hakika ingethaminiwa zaidi ya kuogopwa tu.
Ni muhimu hapa nisisitize kuwa ninazungumzia 'hali mwafaka' yaani kwa Kiingereza ideal situation. Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi miongoni mwa wananchi wakiishutumu Idara yetu ya Usalama wa Taifa kuwa imeleemea mno kwenye siasa hasa kuibeba CCM,imezembea mno kiasi cha kuruhusu ufisadi kushamiri, na imekuwa ikilaumiwa pia kutokana na matukio mbalimbali yanayotishia usalama wa Taifa kama vile ugaidi.
Wanaotoa lawama hizo wapo sahihi kwa kiasi flani,kwani kushamiri kwa maovu katika jamii sambamba na mwendelezo wa matukio yanayotishia usalama wa taifa ni viashiria kuwa Idara ya Usalama ya nchi husika ina mapungufu kiutendaji.
Hata hivyo,ni muhimu kutambua kanuni moja muhimu ya ufanisi au kushindwa kimajukumu kwa Idara ya Usalama wa Taifa popote pale.Ni kwamba wakati Idara husika inapaswa kuwa macho katika kila sekunde kuzuwia matendo ya kidhalimu, wanaopanga kufanya matendo hayo wanahitaji mara moja tu kufanikisha azma yao.
Mfano halisi ni kwenye matukio ya ugaidi. Wakati gaidi anahitaji fursa moja tu kufanikisha tukio la kigaidi, Idara ya Usalama inahitaji kila fursa- kila sekunde, dakika,
saa, siku, wiki, mwezi, mwaka-kuhakikisha gaidi hafanikiwi.
Kadhalika, wakati inaweza kuwa rahisi kuilaumu Idara ya Usalama wa Taifa inaposhindwa kuzuwia tukio flani, kwa mfano shambulio la kigaidi nchini Kenya, kiuhalisi suala zima la ukusanyaji wa taarifa za kiusalama ni gumu mno.
Hebu pata picha: unaletewa tetesi kuwa kuna mtu anataka kulipua bomu kanisa au msikiti. Mara nyingi tetesi hizo huwa hazibainishi jinsia ya mtu huyo,wajihi wake,ni mwenyeji au mgeni na vitu vingine muhimu vya kuweza kumtambua japo kwa ugumu.
Kutokana na ugumu wa zoezi la kukusanya taarifa za kiusalama,ndio maana wahusika-mashushushu/maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa-wanapaswa kuwa watu wenye akili isiyo ya kawaida, au angalau wenye uwezo mkubwa wa kutumia akili.Neno lenyewe intelijensia linahusiana na matumizi ya akili.
Lakini si akili tu, bali pia maafisa usalama wa taifa hupaswa kujifunza na kuendeleza hisia ya sita (6th sense). Mwanadamu wa kawaida ana hisia 5: HARUFU kwa kutumia pua; LADHA kwa kutumiamdomo/ulimi, KUGUSWA (touch) kwa kutumia ngozi, KUONA kwa kutumia macho, KUSIKIA kwa kutumia masikio. Lakini kwa mashushushu wanapaswa kuwa na hisia ya ziada ya kutambua kitu zaidi ya kutumia hisia hizo 5 kuu. Si kazi rahisi hata kidogo.
Afisa usalama wa taifa anapatikanaje?
Kwa Tanzania, zoezi la uajiri wa mashushushu hufanyika kwa usiri mkubwa (angalau taratibu zinapaswa kuwa hivyo). Na hata kwa mashirika ya kishushushu ya nchi nyingine, ajira za wazi kama nilivyoonyesha hapo juu hazimaanishi kuwa waajiriwa wote wa mashirika hayo hupatikana kwa uwazi.
Kimsingi, na pengine tukitumia mfano 'mwafaka' wa Idara yetu ya Usalama wa Taifa, kinachoangaliwa kwa mtu anayetakiwa kuajiriwa ni 'vitu vya ziada' pengine tofauti na watu wengine. Katika mazingira stahili (ideal situation) shushushu mtarajiwa anatarajiwa kuwa na uwezo mkubwa wa akili, yaani kama nilivyoeleza katika makala iliyopita kwamba kazi yenyewe ni ya matumizi makubwa ya akili, kwahiyo mtarajiwa anapaswa kuwa intelligent kweli kweli.
Tukiendelea na mazingira hayo stahili, taasisi ya ushushushu huanza kitambo 'kumwinda' wanayetaka kumwajiri. Sehemu mwafaka zaidi za kusaka mashushushu watarajiwa ni katika taasisi za elimu. Sababu kuu za msingi za kutumia taasisi za elimu kama 'soko' la 'kuchagua mashushushu watarajiwa' ni, kwanza, umri wa wanafunzi wengi huwa mwafaka kuonyesha tabia zao halisi, na pili, taasisi ya elimu hutoa ushahidi mzuri wa kiwango cha akili cha shushushu mtarajiwa.
Sehemu nyingine iliyokuwa mwafaka kuwasaka mashushushu watarajiwa ilikuwa kwenye kambi za jeshi la kujenga taifa. Wakati taasisi za elimu zinatoa fursa nzuri kutambua uwezo wa akili wa shushushu mtarajiwa, kambi za JKT zilikuwa zikitoa fursa nzuri ya kuangalia uwezo wa kimwili, hususan uvumilivu (indurance). Kwa waliobahatika kupitia JKT wanafahamu bayana kuwa mafunzo ya awali (takriban miezi 6 ya mwanzo) yalikuwa yanaufikisha mwili katika kiwango cha juu kabisa cha uvumilivu. Ni katika mazingira kama hayo ndipo taasisi za kishushushu zinaweza kupata fursa ya kuona 'uwezo wa ziara' au 'usio wa kawaida' wa shushushu mtarajiwa.
Kadhalika, zamani kulikuwa na shule mbili-katika-moja iliyokuwa na mchepuo wa kijeshi. Shule hiyo ni Tabora School, ambayo kimsingi ni Shule ya Sekondari ya Tabora Wavulana (Tabora Boys) na Tabora Wasichana (Tabora Girls). Shule hizi ambazo kimfumo zilikusanya wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao kutoka takriban kila wilaya ya Tanzania zilitoa fursa nzuri kwa Idara ya Usalama wa Taifa kupata maafisa wake watarajiwa.
Uzuri wa shule hizo ni kwamba zilitoa fursa mbili kwa mpigo: fursa kwa mashushushu kupima uwezo wa kiakili wa mtarajiwa na pia kuona uwezo wake kimwili kupitia mazoezi na mafunzi ya kijeshi katika shule hizo. Vilevile, shule hizo ambazo pia zilikuwa na maafisa wa jeshi kama walimu, na wanafunzi wanaovaa sara zinazofanana na za kijeshi , zilitawaliwa na nidhamu ya hali ya juu, sambamba na kuhimiza uzalendo
Lakini kwa vile ajira katika taasisi za kishushushu inazingatia zaidi mahitaji ya kimazingira, nyakati nyingine walengwa huwa watu waliopo makazini, kwa mfano wahadhiri, maafisa wa vyombo vingine vya dola - kwa mfano jeshi au polisi- na maeneo mengineyo.
Ila ajira za namna hii ni za nadra kwa sababu mara nyingi watu wa aina hiyo 'huajiriwa' kama 'watoa habari' au sources kama wanavyofahamika kiintelijensia. Kinachoweza kuiskumua taasisi ya kishushushu kulazimika kumwajiri mtu ambaye tayari ana ajira nyingine au yupo katika fani tofauti ni unyeti wa nafasi yake na umuhimuwa wake wa muda mrefu.
Njia hii ni kama ya dharura au ya katika mazingira maalumu kwani kuna ugumu wa kumshawishi mhusika akubali kuajiriwa, na pengine mtu huyo anaweza kuwa na mtandao mkubwa wa kijamii - kwa maana ya familia au marafiki - na hilo linafanya sharti kuu la ajira kwenye taasisi yoyote ya usalama wa taifa, yaani USIRI, kuwa mashakani. Ni rahisi kumkanya mwanafunzi wa sekondari, kwa mfano, kwamba asimwambie mtu yeyote kuhusu jukumu atakalokabidhiwa mbeleni, na akalihifadhi - pengine kwa vitisho- kuliko mtu mzima ambaye inaweza kumwia vigumu kumficha mkewe au marafiki wa karibu. Na kama tujuavyo, ajira katika sehemu hizo zina 'ujiko' wa namna flani, kwahiyo si ajabu mtu mzima akiambiwa 'kuna dili' sehemu akaanza kutangaza kabla hata hajapewa mafunzo.
Kimsingi hakuna muda maalumu wa kumfuatilia mtu anayetakiwa kujiunga na taasisi ya kishushushu. Panapo dharura, zoezi la ufuatiliaji laweza kudumu kwa muda mfupi, lakini pasipo haraka yaweza kuchukua miaka kadhaa.
Baada ya kuwatambua 'waajiriwa watarajiwa' - process inayofahamika kama spotting - hatua inayoweza kufuata ni kuwa kuwaendeleza watarajiwa hao (yaani kuwaandaa kwa ajili ya utumishi kwa taasisi husika). Neno mwafaka ni development. Katika hatua hii, mashushushu HALISI wanakutana na mashushushu watarajiwa.
Hatua hii inaweza kuchukua muda mfupi kutegemea mabo kahdaa au yaweza kuchukua muda mrefu pia. Hadi hapo, taasisi husika huwa haijafikia uamuzi wa kumwajiri mtarajiwa au la, bali inafanya marejeo ya ufuatiliaji wa awali na maendeleo ya mhusika katika kipindi hicho.
Sambamba na hatua hiyo, ni uamuzi kwa taasisi ya ushushushu kuanza kufanya ufuatiliaji wa kina kuhusu mtarajiwa. Ufuatiliaji huo hujulikana kama VETTING. Hata hivyo, uamuzi wa kufanya vetting hutarajia 'potential' ya mtarajiwa, hasa ikizngatiwa kuwa vetting ni process ndefu na inayoweza kuwa na gharama kubwa.
Kwa kifupi, process hiyo inalenga kumfahamu mtarajia 'nje ndani' yaani kila kitu kumhusu yeye. Na hapo ndipo utabaini urahisi wa kutafuta mashushushu wapya wakiwa wadogo mashuleni- kwa vile hufanya vetting kutokuwa ndefu sana kutokana na kutokuwa na mtandao mkubwa wa mahusiano kijamii au kimaisha, ilhali kwa mtu mzima kazini itamaanisha kuwafuatilia watu wengi na pengine kutembelea sehemu nyingi pia.
Na pindi vetting isipofanywa kwa umakini, dhamira nzima ya kufanya suala hilo kwa usiri linaweza kuathiriwa. Athari hizo si kwa taasisi ya kishushushu pekee bali pia yaweza kuyaweka maisha ya mtarajiwa hatarini.
Matokeo ya jumla ya vetting ndiyo yatakayoamua hatma ya ajira ya shushushu mtarajiwa. Nimesema 'matokeo ya jumla' kwa sababu hata baada ya kuajiriwa, shushushu huendelea kufanyiwa ufuatiliaji na mwajiri wake katika muda wake wote wa utumishi wake, na pengine hadi atakapoaga dunia. Kadhalika, vetting hujitkeza pia pindi shushushu anapotaka kuoa au kuolewa, ambapo mwenza wake hufanyiwa uchunguzi ili kuthibitika kuwa hatokuwa na madhara kwa utendaji wa kazi wa shushushu husika.
Mwisho.
Chanzo: Evarist Chahali blog