Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Inj. Cyprian Luhemeja ametembelea mradi wa maji wa Chalinze ili kujionea maendeleo ya mradi

mawazomgala

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
342
212
September 12, 2018

Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Inj. Cyprian Luhemeja ametembelea mradi wa maji wa Chalinze ili kujionea maendeleo ya mradi na kupanga utaratibu wa kuongeza kasi ya ujenzi.

Ikiwa ni siku yake ya nne tangu kutangazwa rasmi jumamosi Sept. 8, 2018, amefanya maamuzi ya kuongeza nguvu katika usimamizi na kutaka mkandarasi kampuni ya OIA ya India kutekeleza kazi usiku na mchana ili kuleta matokeo yanayotarajiwa.

Luhemeja amesema mradi utazinduliwa mwezi Disemba 2018. Leo anaendelea na ziara katika miradi ya usambazaji maji.
 
Ni jambo jema ikiwa kila kiongozi atawajibika na kusimamia utekelezaji wa mipango tunayojiwekea.
Tulizembea sana hapo awali.
Ni bahati sasa tumepata RAIS anayeonesha NJIA.
TUMFUATE!
 
Ila huu mtindo wa kuteleleza majukumu na kujirusha kwenye media si mzuri. Hawa wanataka waonekane na wateuzi wao kwamba wanafanya kazi. Sasa huyo jamaa alichokifanya ni moja ya majukumu yake na sio habari hapo ni ipi. Itafikia siku tutaandika, 'xx amefika ofisini kwake saa moja kamili ikiwa ni nusu saa kabla ya muda wa kazi kuanza'.
 
Lengo ni kuwahabarisha wananchi juu ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali,inaweza isiwe news kwako ikawa news kwa mtu mwingine
 
Back
Top Bottom