Afaulu Mtihani wa Udereva Baada ya Kufeli mara 950 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afaulu Mtihani wa Udereva Baada ya Kufeli mara 950

Discussion in 'International Forum' started by Mbonea, Nov 8, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  </SPAN>


  Cha Sa-soon muda mfupi baada ya kufaulu mtihani wa kuandika wa udereva
  Sunday, November 08, 2009 2:05 AM
  Mwanamke mmoja wa nchini Korea Kusini ambaye alikuwa akifeli mtihani wa udereva wa kuandika kila alipokuwa akiingia kufanya mtihani huo, amefanikiwa kufaulu mtihani huo baada ya kufeli mara 949.


  Cha Sa-soon mwenye umri wa miaka 68, alianza majaribio yake ya kufaulu mtihani wa udereva mwezi aprili mwaka 2005 lakini alikuwa akifeli mtihani huo kila alipojaribu bahati yake.

  Cha alikuwa akifeli mtihani wa mwanzo wa udereva wa kuandika akipata maksi 30-50 wakati maksi zinazohitajika ni 60-100.

  Baada ya kufanya mtihani huo karibia kila siku kuanzia mwaka 2005, Cha amefanikiwa kufaulu mtihani huo kwa kupata maksi 60 katika mara yake ya 950 ya kuingia kwenye mtihani huo.

  Hivi sasa Cha ana kazi ngumu ya kufaulu mtihani wa vitendo wa udereva ili aweze kupata leseni ya udereva.

  Cha anafanya biashara ya kuuza chakula na vifaa vya majumbani akiuza bidhaa zake kwa kuzipitisha mlango kwa mlango kwenye maendeo ya watu wenye fedha. Kutokana na sababu hiyo Cha alisema anahitaji gari kwaajili ya biashara zake.

  "Ni kitendo cha kuvunja rekodi ya dunia " alisema Choi Yong-Cheol polisi anayesimamia mitihani ya udereva katika mji wa Deokjingu.

  Polisi wanakadiria Cha ameishatumia zaidi ya dola 4,000 katika jitihada zake za kufaulu mtihani huo.  Source: AFP
   
 2. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh! Haya aiseee
   
 3. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Hii kali
   
 4. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Nadhani huu ni mfano wa kuigwa!
  Winners never quit! and quiters never win!
   
 5. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Verry ryt my dia
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Atakuwa mke mzuri sana huyu mama., na bila shaka nyumba yake ni ya amani tupu na bwanaake...Sijui huku bongo kwanini hatuwapati wa hivi!

  Wanawake wa kibongo hawa, utawasikia..."aah, mi siwezi kabisa hata kufungua mlango wa nyumbani kwangu!...

  YAMENENEPA TUUU....Mnaboa bana,... jishughulisheni nyie...!
   
 7. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hahahahaaa.heee jamani! nacheka lakini kwa uchungu.mbona unaponda hivo? nafikiri wewe hujakutana nao akina mama wachakarikaji,mbona wengi tu,mfano Rita Paulsen,Getrude Rwakatare,na wengine wengi sana.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  ZD,
  Lakini hata hivyo kuna ukweli mkubwa sana juu ya hayo niliosema...Asilimia 70 ya wanawake ni wavivu na matipwatipwa yaliyojaajaa nyama-uzembe!..

  Wanangoja kuletewaletewa tu..!.."Baba Naniliu, usisahau hao dagaa eeh"..!!

  Limekaa tu, linabadilisha mikao uani!.fyuuuuup!

  Hao uliowataja ni katika 30% iliyobaki.
   
 9. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #9
  Nov 8, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Dah! haya bwana,japo ukweli huwa unauma kama nini.Point noted.I'll try my level best,.Lakini mkuu PakaJimmy hata wwe pi(au niseme wanaume) mnapaswa kulaumiwa! kwa sabb unaendekeza hali hiyo na hujasema chochote kwa mkeo kuhusu kujishughulisha.Na wengi sio kama hawawezi ila ni kujiamini tu ndio tatizo.hivyo waelimisheni na kuwa-push muone kama hawajaweza.
   
Loading...