Afariki Baada ya kutoa fedha ATM Mashine

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,150
Afariki Baada ya kutoa fedha ATM Mashine
3564874.jpg

Tuesday, November 17, 2009 10:35 AM
MWANAUME mmoja aliyefahamika kwa jina la Chacha W mwenye umri wa miaka 35 amefariki dunia ghafla mara baada ya kumaliza kutoa fedha kutoka kwenye mashine za kutolea fedha [ATM] katika Tawi la Mbezi Makonde jijini Dar es Salaam. Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Sebastian Masinde amesema, tukio hilo limetokea mishale ya 11:45 jioni, huko katika tawi la Benki ya NBC Mbezi Makonde.

Amesema, kabla ya kupatwa na umauti hayo marehemu alifkia katika tawi hilo kwa lengo la kupata huduma za kibenki na kuingia moja kwa moja katika chumba za mashine hiyo aliingiza kadi yake kama kawaida.

Amesema alipofanikiwa kutoa kiasi cha fedha alichokihitaji ndipo kifo kilipomkuta kwani alipochomoa kadi yake ndani ya ATM ghafla akaanguka chini na kufariki dunia papohapo.

Hata hivyo Kamanda huyo amesema jeshi hilo hawajathibitisha chanzo cha kifo cha mtu huyo, na amehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi zaidi juu ya kifo chake.
 
oooyeahhhhh...mapenzi siasa tupu...vifo vya kina kolimba/nk siasa tupu
 
Back
Top Bottom