AFANDE MPINGA VIPI DALADALA NAMBA T658BCQ, VIPI?

chhatbhai

Member
Apr 12, 2016
8
1
Afande mpinga kwa kipindi kirefu nimekuwa nikiona askari wa barabarani wakikamata magari ovyo sana , hata yale ambayo unaona kabisa hayana makosa lakini askari wako wanalazimisha kuwaandikia faini na hao askari wako hawana wakumsikiliza mwenye gari au dereva, wakiishaandika wanakwambia wewe kalipe kwa huyo askari au nenda utalipa baadae ukiwa na pesa.
Mara mbili nikiwa kwenye daladala:
1)nambari T658BCQ gari linafanya kazi toka makumbusho kwenda Ununio, askari alilisimamisha na kumtaka dereva atelemke, yule dereva ni mtu wa makamo, akamuuliza kuna tatzo gani? askari akaleta ukali na kumkalipia akimtaka ateremke, yule dereva akamwambia kuwa hili gari hulijui? Ni la askari. yule askari alipong'ang'ania yule dereva akateremka na kumwambia kuwa nipige simu uongee nae? Yule askari akaanza kushusha munkali na kumuita pembeni na kumwambia kuwa tutazuga tutaandika makosa mawili, moja la bodi chakavu na la pili la exhaust kutoa moshi mchafu, mambo yakaishia hapo. hilo gari halikufanya lolote kati ya yaliyoandikiwa makosa, sikurekebisha ubovu wa bodi wala exhaust.
2) daladala zote zinazofanya kazi toka makumbusho kwenda Ununio ni magari yamechoka na kweli huenda yote ni ya askari kwani hata upakiaji wake unatisha sana. gari hizo zinapakia kupita kiasi na hakuna wakuzikagua au kuzikamata kwani njia hiyo haina polisi traffic, na hata akiwepo kwa bahati mbaya, hayasimamishi kuyakagua, KULIKONI? Hiyo njia haiko Tanzania?. nashauri upatpiye jicho ili uone kinachojiri, kwani upakiaji wa binadamu hivyo waweza kuwa chanzo cha kuambukizana ugonjwa.
NAWASILISHA
 
Back
Top Bottom