Afande Awadhi unachofanya sio sahihi

Afande Awadhi unachofanya sio sahihi

Kumpiga makofi ni kosa kubwa, kutoa upepo ili gari lisitembee, sawa? Na Kunyang'anya funguo ili iwe nini? Kwanini asingemnyang'anya funguo tu? Huu ni uonevu.

Kabisa tujifunze kukataa uonevu kama huu, hivi mfano madereva wote pale wangeshuka na kumkomalia huyo askari si wangekuwa wamefanya jambo la maana sana. ?Imagine anamfanyia hivyo mwanao, mama yako , dada yako au mkeo?
 
Hapa si bure unalilia yako ya maungoni...hapa dada mwenye IST ya Cream kama upo single kuna mwekezaji huku!
 
M
Kwa wale watumiaji wa barabara za Dar es salaam bila shaka watakuwa wanamfahamu fika huyu polisi anayejulikana kwa jina la AWADH mwenye cheo cha SP ambaye mara nyingi huwa namuona kwenye barabara ya Al-Hassan Mwinyi hasa maeneo ya ubalozi wa Ufaransa na sehemu zenye utata wa foleni.

Kwanza kabisa ningependa kumpongeza kwa juhudi binafsi anazozionyesha na kujituma kwa manufaa ya watumiaji wa barabarani, lakini hata hivyo Wahenga hawakukosea waliposema ''Kizuri Hakikosi kasoro''.

Nina maana gani kusema hivyo? Labda niwape mkasa kidogo kuhusiana na huyu Askari wa Usalama barabarani ambao nimeushuhudia kwa macho yangu asubuhi kweupe pasi na kupepesa.

Nilikuwa nipo kwenye foleni naelekea City Center kwenye shughuli zangu za kujitafutia mkate wangu wa kila siku, nilipofika maeneo ya Ubalozi wa Ufaransa nikawa natazama magari yaliyokuwa yanatoka kwenye barabara ya OCTAS ambapo kwa wakati ule yalikuwa mengi.

Ghafla Awadh akawa amefika eneo la tukio akiwaelekeza madereva namna ya kuweza kupita na kupunguza msongamano, wakati akiwapa maelekezo na kuyaruhusu magari mengine kuingia kwenye barabara ya Al Hassan mwinyi, kuna mwanadada mmoja alikuwa yupo ndani ya gari yake aina ya IST rangi ya cream.

Huyu mwanadada alikuwa kwenye foleni ileile aliyokuwa ikiongozwa na Awadh, lakini katika hali ya kushangaza Awadh alimfuata yule dada akaanza kumchapa makofi na kama kuona hiyo haitoshi akamchomolea upepo wa tairi ya kulia ya gari yake na kumnyang'anya funguo.

Yule Dada akawa analia huku amelalia usukani wa gari, kusema ukweli kitendo kile kiliniuma sana hasa ukizingatia jinsia zao ni tofauti na mbaya zaidi yule ni mtoto wa kike.

Moja kwa Moja nadhubutu kusema alimfanyia unyanyasaji wa kijinsia kweupe, nilitamani nitoke kwenye usafiri wangu niende nikamtete sema kuna roho ikaniambia nisiende.

Nikawa najiuliza kama yule mwanadada amekosea, why hakufuata taratibu za kumpiga faini mpaka amdhalilishe kiasi kile?

Afande Awadh tunakuhiji ubadilike na kama huwa unafanikiwa kuingia huku bila shaka utakuwa umeshapata ujumbe wako.
Kamanda mpinga alishatoa namba zake za sim ungefanya msaada wa kumpigia ili aone jinsi askari wake wanavyofanya kazi, na cheo alicho nacho ni kiongozi, kwa sasa wana hasira kwani rushwa imepungua madereva wengi sasa wanajua sheria haki zao. ukiona tukio kama hilo jaribu kuchuka video au numer ya gari ili ashughulikiwe, ikithibitika huyo kibarua ni lazima kiote nyasi.
 
Ngoja nimtafute Awadh mchana huu nitawaletea upande wake wa maelezo.
iwe iwavyo huyu awadhi anatatizo na ni mshirikina pia ... mimi sina gari lakini namfaham awadhi kila uchao madereva wanadiscuss jinsi anavyowatesa
 
Aisee jombaa kwanza nivizuri kuleta huo mkasa hapa, lakini polisi na wao ni binadam kinachowadanganya ni zile sare tu, ebu nguvu ya umma na yenyewe iamke inapotokea matukio kama haya ya unyanyasaji, mbona sijawahi kuchomolewa funguo!. Natambua raia ana nguvu kisheria kuliko hata huyo afande nani sijuiii...., jamaa huwa wanajitoaga akili sana.
Either huna makosa ya barabarani yaliyo hatarishi kwako na kwa watumiaji wengine au hao askari unaokutana nao ni wahanga wa rushwa (rushwa inakufanya uwe mtumwa wa kila mtu) au hawajui haki zao/sheria.

Umma ufanye kazi lakini usimzuie askari kufanya kazi yake...ubabe peleka pub ukawe bouncer mlangoni.

Nb: baada ya kusema hayo niseme siungani na kilichofanywa na huyo Awadhi kama kweli kilifanyika.
 
Sijawahi kutoa rushwa wala kupokea rushwa.
 
mkuu Radika basi la kusini sina hakika ni mtwara au lindi ila ni tukio lilizungumzwa sana miaka ya 90...
 
Huyo Dada akimfikishia ujumbe Mme wake najua patachimbika leo .
 
wenye njaa tunadharauliana wenyewe.. tunaoneana kisa tunasema wenye pesa wanatunyantasa...

tuongee ukweli huyo dada angekuwa mke au mtoto wa tajiri kama bakhresa, mengi au gsm huyo afande angeweza mpiga makofi.. na kama angempiga angefungwa yeye hadi rpc angetoa maelezo kwenye media hilo seke seke lake
 
*Kwa Kweli Nashindwa Kusema Lolote Maana Story Ukiisikia Upande Mmoja Tu Huwa Si Rahisi Sana Kuhukumu Hasa Kama Tu Utajiuliza Maswali Mengi.

*Mleta Uzi Anasema Dada Alikuwa Sahihi Lakn Akapigwa Na Kutolewa Upepo.

*Hili Jambo Si La Kuliangalia Ki Jounalism Ni Jambo La Kiliangalia Kisheria Zaidi, Kuanzia Mwanzo Wa Tukio Hadi Mwisho Na Nini Ilikuwa Chanzo.
Hapa Ni Lazima Usikilize Maelezo Ya Askari Na Raia Ndio Utapata Jibu Sahihi.
Ni Kweli Pengine Askari Kafanya Kosa Lakn Si Vyema Tu Kuhukumu Kwa Kuwa Alofanya Tendo Hilo Ni Polisi So Tunahukumu Kwa Chuki.

*Japo Kumpiga Raia Ni Kosa Lakn Lazima Tujiulize Maswali Yafuatayo.
1. Kwanini Mtu Mzima Mwenye Akili Timamu Ampige Bila Kosa?.

2. Kwanini Askari Tena Ofisa Mwenye Zaidi Ya Miaka15 Kazini Na Cheo Cha Zaidi Ya Nyota3, Inakuwaje Ampige Huyu Dada Tena Pasi Tatzo Lolote?!.

3. Je Kuna Kitu Kinaweza Kutokea Bila Sababu?!.

Mtoa Uzi Mi Naamini Kuna Mahala Umepitiwa Kidogo Japo Tukio Lawezakuwa Kweli Lilikuwepo Ama Halikuwepo Lakn Haiingii Akilini Askari Mtu Mzina Umpige Vibao Mdada Tena Bila Kosa Kwa Kigezo Kwmb Wew Ni Askari. . .. Mmmmh Natia Shaka Lakn Wachunguzi Watajua Zaidi.
 
Huyo dada alipewa adhabu mara nne..
1. Kupigwa makofi
2. Kutolewa tairi upepo
3. Kunyanyaswa
4. Kuny'anganywa funguo

#AwadhiMustGo
 
Kwa wale watumiaji wa barabara za Dar es salaam bila shaka watakuwa wanamfahamu fika huyu polisi anayejulikana kwa jina la AWADH mwenye cheo cha SP ambaye mara nyingi huwa namuona kwenye barabara ya Al-Hassan Mwinyi hasa maeneo ya ubalozi wa Ufaransa na sehemu zenye utata wa foleni.

Kwanza kabisa ningependa kumpongeza kwa juhudi binafsi anazozionyesha na kujituma kwa manufaa ya watumiaji wa barabarani, lakini hata hivyo Wahenga hawakukosea waliposema ''Kizuri Hakikosi kasoro''.

Nina maana gani kusema hivyo? Labda niwape mkasa kidogo kuhusiana na huyu Askari wa Usalama barabarani ambao nimeushuhudia kwa macho yangu asubuhi kweupe pasi na kupepesa.

Nilikuwa nipo kwenye foleni naelekea City Center kwenye shughuli zangu za kujitafutia mkate wangu wa kila siku, nilipofika maeneo ya Ubalozi wa Ufaransa nikawa natazama magari yaliyokuwa yanatoka kwenye barabara ya OCTAS ambapo kwa wakati ule yalikuwa mengi.

Ghafla Awadh akawa amefika eneo la tukio akiwaelekeza madereva namna ya kuweza kupita na kupunguza msongamano, wakati akiwapa maelekezo na kuyaruhusu magari mengine kuingia kwenye barabara ya Al Hassan mwinyi, kuna mwanadada mmoja alikuwa yupo ndani ya gari yake aina ya IST rangi ya cream.

Huyu mwanadada alikuwa kwenye foleni ileile aliyokuwa ikiongozwa na Awadh, lakini katika hali ya kushangaza Awadh alimfuata yule dada akaanza kumchapa makofi na kama kuona hiyo haitoshi akamchomolea upepo wa tairi ya kulia ya gari yake na kumnyang'anya funguo.

Yule Dada akawa analia huku amelalia usukani wa gari, kusema ukweli kitendo kile kiliniuma sana hasa ukizingatia jinsia zao ni tofauti na mbaya zaidi yule ni mtoto wa kike.

Moja kwa Moja nadhubutu kusema alimfanyia unyanyasaji wa kijinsia kweupe, nilitamani nitoke kwenye usafiri wangu niende nikamtete sema kuna roho ikaniambia nisiende.

Nikawa najiuliza kama yule mwanadada amekosea, why hakufuata taratibu za kumpiga faini mpaka amdhalilishe kiasi kile?

Afande Awadh tunakuhiji ubadilike na kama huwa unafanikiwa kuingia huku bila shaka utakuwa umeshapata ujumbe wako.
1. Kama ungekuwa mwanaharakati wa haki za binadamu, ungeshuka na kwenda kumuuliza sababu ya kumpiga makofi pasipo hukumu ya mahakama.
2. Jengeni tabia ya kutumia simu zenu kurekodi matukio muhimu kama hayo na kisha kuja kuyaleta sehemu kama hizi ili muweze kupata msahada wa kisheria.
3. Next time chagua kufanya moja kati ya hayo mawili au yote kwa pamoja.
 
Kwa wale watumiaji wa barabara za Dar es salaam bila shaka watakuwa wanamfahamu fika huyu polisi anayejulikana kwa jina la AWADH mwenye cheo cha SP ambaye mara nyingi huwa namuona kwenye barabara ya Al-Hassan Mwinyi hasa maeneo ya ubalozi wa Ufaransa na sehemu zenye utata wa foleni.

Kwanza kabisa ningependa kumpongeza kwa juhudi binafsi anazozionyesha na kujituma kwa manufaa ya watumiaji wa barabarani, lakini hata hivyo Wahenga hawakukosea waliposema ''Kizuri Hakikosi kasoro''.

Nina maana gani kusema hivyo? Labda niwape mkasa kidogo kuhusiana na huyu Askari wa Usalama barabarani ambao nimeushuhudia kwa macho yangu asubuhi kweupe pasi na kupepesa.

Nilikuwa nipo kwenye foleni naelekea City Center kwenye shughuli zangu za kujitafutia mkate wangu wa kila siku, nilipofika maeneo ya Ubalozi wa Ufaransa nikawa natazama magari yaliyokuwa yanatoka kwenye barabara ya OCTAS ambapo kwa wakati ule yalikuwa mengi.

Ghafla Awadh akawa amefika eneo la tukio akiwaelekeza madereva namna ya kuweza kupita na kupunguza msongamano, wakati akiwapa maelekezo na kuyaruhusu magari mengine kuingia kwenye barabara ya Al Hassan mwinyi, kuna mwanadada mmoja alikuwa yupo ndani ya gari yake aina ya IST rangi ya cream.

Huyu mwanadada alikuwa kwenye foleni ileile aliyokuwa ikiongozwa na Awadh, lakini katika hali ya kushangaza Awadh alimfuata yule dada akaanza kumchapa makofi na kama kuona hiyo haitoshi akamchomolea upepo wa tairi ya kulia ya gari yake na kumnyang'anya funguo.

Yule Dada akawa analia huku amelalia usukani wa gari, kusema ukweli kitendo kile kiliniuma sana hasa ukizingatia jinsia zao ni tofauti na mbaya zaidi yule ni mtoto wa kike.

Moja kwa Moja nadhubutu kusema alimfanyia unyanyasaji wa kijinsia kweupe, nilitamani nitoke kwenye usafiri wangu niende nikamtete sema kuna roho ikaniambia nisiende.

Nikawa najiuliza kama yule mwanadada amekosea, why hakufuata taratibu za kumpiga faini mpaka amdhalilishe kiasi kile?

Afande Awadh tunakuhiji ubadilike na kama huwa unafanikiwa kuingia huku bila shaka utakuwa umeshapata ujumbe wako.
Lini hiyo mkuu naomba sikuya tukio
 
Back
Top Bottom