Afande Awadhi unachofanya sio sahihi

Rajabu Msechu

Member
Apr 13, 2016
35
18
Kwa wale watumiaji wa barabara za Dar es salaam bila shaka watakuwa wanamfahamu fika huyu polisi anayejulikana kwa jina la AWADH mwenye cheo cha SP ambaye mara nyingi huwa namuona kwenye barabara ya Al-Hassan Mwinyi hasa maeneo ya ubalozi wa Ufaransa na sehemu zenye utata wa foleni.

Kwanza kabisa ningependa kumpongeza kwa juhudi binafsi anazozionyesha na kujituma kwa manufaa ya watumiaji wa barabarani, lakini hata hivyo Wahenga hawakukosea waliposema ''Kizuri Hakikosi kasoro''.

Nina maana gani kusema hivyo? Labda niwape mkasa kidogo kuhusiana na huyu Askari wa Usalama barabarani ambao nimeushuhudia kwa macho yangu asubuhi kweupe pasi na kupepesa.

Nilikuwa nipo kwenye foleni naelekea City Center kwenye shughuli zangu za kujitafutia mkate wangu wa kila siku, nilipofika maeneo ya Ubalozi wa Ufaransa nikawa natazama magari yaliyokuwa yanatoka kwenye barabara ya OCTAS ambapo kwa wakati ule yalikuwa mengi.

Ghafla Awadh akawa amefika eneo la tukio akiwaelekeza madereva namna ya kuweza kupita na kupunguza msongamano, wakati akiwapa maelekezo na kuyaruhusu magari mengine kuingia kwenye barabara ya Al Hassan mwinyi, kuna mwanadada mmoja alikuwa yupo ndani ya gari yake aina ya IST rangi ya cream.

Huyu mwanadada alikuwa kwenye foleni ileile aliyokuwa ikiongozwa na Awadh, lakini katika hali ya kushangaza Awadh alimfuata yule dada akaanza kumchapa makofi na kama kuona hiyo haitoshi akamchomolea upepo wa tairi ya kulia ya gari yake na kumnyang'anya funguo.

Yule Dada akawa analia huku amelalia usukani wa gari, kusema ukweli kitendo kile kiliniuma sana hasa ukizingatia jinsia zao ni tofauti na mbaya zaidi yule ni mtoto wa kike.

Moja kwa Moja nadhubutu kusema alimfanyia unyanyasaji wa kijinsia kweupe, nilitamani nitoke kwenye usafiri wangu niende nikamtete sema kuna roho ikaniambia nisiende.

Nikawa najiuliza kama yule mwanadada amekosea, why hakufuata taratibu za kumpiga faini mpaka amdhalilishe kiasi kile?

Afande Awadh tunakuhiji ubadilike na kama huwa unafanikiwa kuingia huku bila shaka utakuwa umeshapata ujumbe wako.
 
Alimpiga makofi??? Kwa kosa gani sasa? na nini tena sababu ya kutoa upepo wa tairi? Aisee huyo jamaa ana tatizo.
 
Sasa huyu dada alifanyaje na tairi isiyokuwa na upepo? Duh! I hope hakunyamaza bali alidai haki yake.
 
Alichofanya huyo Afisa wa Polisi siyo sahihi, kama kweli kilifanyika. Kitu cha kufanya kwa mwathirika ni kupeleka malalamiko kwenye Dawati la Jinsia kwenye Kituo chochote cha Polisi au Kitengo cha Malalamiko Makao Makuu ya Jeshi la Polisi au kwenda Mahakamani baada ya kwenda hospitali na PF.3.
Bado kuna urasimu kwenye kutoa malalamiko katika Jeshi la Polisi hasa kama maafisa wao ni wahusika. Hapa linakuja suala la nani atamwajibisha Polisi?
 
Sio kama kuna solution utaipata hapa au unataka tujadili kimbea, we kama raia mwema ulitakiwa kuchukua uamuzi wa kutoka na kumsaidia au kusikilliza chanzo cha tatizo na sio kuja kulalamika kwenye jukwaa ambalo hata huyo afande hujui kama anapita kusoma hapa tujue kuchukua maamuzi yanayowaathiri raia wenzetu najua ungetoka na kupata maelezo pande mbili ungepata kitu unaweza kuta hata ni wivu wa kimapenzi baina yao wahusika. Nilishawahi ona clip toka kenya raia wakimsaidia kilema aliyekuwa akiburuzwa na police wa jiji maarufu kama Kanjoo na ilionesha jinsi gani nguvu ya umma inafanya maamuzi sahihi sasa wewe na wengine mliokuwa kwenye foleni mlikuwa wabinafsi hamkichukua hatua na huyo afande hataacha kuwapiga makofi watu wengine sababu ya kupuuza itaendelea ivo hata kama sio kesho itakuwa mwakani.
 
Aisee jombaa kwanza nivizuri kuleta huo mkasa hapa, lakini polisi na wao ni binadam kinachowadanganya ni zile sare tu, ebu nguvu ya umma na yenyewe iamke inapotokea matukio kama haya ya unyanyasaji, mbona sijawahi kuchomolewa funguo!. Natambua raia ana nguvu kisheria kuliko hata huyo afande nani sijuiii...., jamaa huwa wanajitoaga akili sana.
 
kazabwa mabao? ... kuanzia juu hadi barabarani everybody is acting with impunity. wakiulizwa wanasema hapa kazi ..
 
HUyo afande jana alifanya mengi sana ya aibu... kuna wakati alipiga mkono wa magari ya kutokea sta peters kwa dk zaidi ya 17...

Sometimes hao askari mnaowasifia ndio wanaosababisha foleni daresalame

Alichokifanya huyo afande kina warranty kufunguliwa mashtaka na more likely kifungo kabisa
 
Sio kama kuna solution utaipata hapa au unataka tujadili kimbea, we kama raia mwema ulitakiwa kuchukua uamuzi wa kutoka na kumsaidia au kusikilliza chanzo cha tatizo na sio kuja kulalamika kwenye jukwaa ambalo hata huyo afande hujui kama anapita kusoma hapa tujue kuchukua maamuzi yanayowaathiri raia wenzetu najua ungetoka na kupata maelezo pande mbili ungepata kitu unaweza kuta hata ni wivu wa kimapenzi baina yao wahusika. Nilishawahi ona clip toka kenya raia wakimsaidia kilema aliyekuwa akiburuzwa na police wa jiji maarufu kama Kanjoo na ilionesha jinsi gani nguvu ya umma inafanya maamuzi sahihi sasa wewe na wengine mliokuwa kwenye foleni mlikuwa wabinafsi hamkichukua hatua na huyo afande hataacha kuwapiga makofi watu wengine sababu ya kupuuza itaendelea ivo hata kama sio kesho itakuwa mwakani.
Huu mchezo hauhitaji hasiraaa
 
Mleta mada ukipaswa kushuka na kumfuata huyo polisi na kupata Maelezo. Kitendo tu cna kujiamini na kumfuata tu kingembabaisha huyo polisi, pia nauwakika ungepata support kutoka kwa watu wengine walioona hilo tukio. Wewe ndo mwenye makosa kwa kutochukua hatua
 
mleta mada unanikumbusha basi moja miaka ya nyuma kidogo lilimshusha mama na mtoto porini katika mbuga ya simba hakuna hata abiria mmoja kupinga lile swala..yule mama baada ya kuona kazingilwa na Simba alimpandisha mwanae katika mti yeye aliliwa yule mtoto alipoona gari inapita alipiga kelele yule mzungu akamfata na kimsaidia though lugha ilikua tatizo alimuelewa alilikimbizia lile basi na kumpeleka yule mtoto kuonesha wote walichokifanya..nakumbuka dereva na konda wake walifungwa ndefu ndio hayo uliotuletea wewe mdada anapigwa na police wa kiume wote mpo busy harafu unakuja huku tutatoa msaada gani zaidi ya kuhuzinika tuu.
 
Isije kuwa ameanza kuwa na ulemavu wa akili...
Polisi wamchunguze asije ua waendesha magari
 
Hamjui kwa nini askari inaita upande mmoja kwa dakika 17,kwa kua hamsikii maelekezo ya radio.inawezekana kabisa upande huo kulikua na msongamano wa magari,na kuna msafara ulitakiwa kupita huko,hapo lazima uyatoe magari.
Kuhusu kumkata vibao mwanamke,huyo ni askari hana tofauti na wa defender,kama mwanmke kachomeka kiasi cha kuhatarisha usalama wa wengine ni haki yake kulambwa makofi,hawezi kuachiwa kisa mwanamke
 
Back
Top Bottom