AFADHALI baba wa kambo kuliko mama wa kambo

AFADHALI baba wa kambo kuliko mama wa kambo

Mshinga

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
3,532
Reaction score
1,130
Wamama wengi wa kambo hawana huruma kwa watoto wa kambo,wana ukatiri na manyanyaso ya hali ya juu,watoto wa kambo wanapigwa,wananyimwa chakula,wanapewa kazi nyingi,wanasingiziwa kwa baba yao ili tu waonekane si watii,wakorofi,hawana nidhamu,watukutu na wapigwe kwa hayo makosa ya kusingiziwa.

MAMA wa kambo wanawashawishi wanaume wasiwalipie ada ama wasiwapeleke shule hawa watoto,hii ni roho mbaya ya mama wengi wa kambo.MAMA WA KAMBO KUMSOMESHA MTOTO WA KAMBO NI NDOTO HATA ANGEKUWA NA UKWASI VIPI.

Watoto wanaolelewa na baba wa kambo wana unafuu mkubwa, wengi hawapigwi,hawanyanyaswi,hawasingiziwi makosa na wengi wanapatiwa mahitaji muhimu ikiwa pamoja na kusomeshwa kwa pesa ya baba wa kambo.

WOMEN PLEASE.................!!
 
umerudi mkuu na lawama kwa wadada kama kawaida!!ulikua waapi?

Tunakosoana tu kwenye mapungufu si lawama.
Nilikuwa hapa hapa mjini nikifanya kazi muhimu kwa ajili ya mipango ya kulisaidia taifa na watu wake, kulisaidia bara la Afrika na watu wake,Na kutakuwa na matumaini makubwa kama waafrika mtaunga mkono.Muda ukifika nitaweka wazi.
 
Hapo sasa atakapomgeuza mwana wa mwenzie mke mdogo upendo ukizidi
 
Walau kwa hili nimeshuhudia mwenyewe kwa macho yangu, nitakuunga mkono kwa thread hii kwa kuwa yaliyosemwa ni kweli kabisa.
 
watoto nao huwa wana-form alliance na baba yao kumnyanyasa mama yao wanaemuita wa kambo maksudi, tena ukute huyo mama BWANA Mungu hajamjalia kuzaa watampeleka sana wote (watoto na baba yao) hasa kuanzia rika la form three kwenda juu, mama yao anakuwa kama house girl akiangialia tv wanabadili channel, sebure inakuwa disco la night club, mama akiwasemesha tu baba anaingilia kati na sometime anaenda mbali zaidi kwa kuacha hela za matumizi kwa watoto. tuwe na upendo mi binafsi nimelelewa na mama wa kambo lakini upendo aliokuwa nao kwangu ni wa juu sana, yuko tayari amdanganye mzee (baba) ili anifinchie hela ya kwenda nayo shule baada ya likizo
 
Back
Top Bottom