Aenda Chato kwa baiskeli kutoa pole na kuonesha jinsi gani Wajasiriamali walivyoguswa na msiba

menny terry

Senior Member
Mar 18, 2011
186
225
Bado tupo kwenye siku 21 za maombolezo kufuatia kifo cha Hayati Dr. John Pombe Magufuli, John Shayo ni Katibu wa Wajasiriamali wanaofanya biashara Magufuli Bus Terminal Mkoani Dar es Salaam ambaye ameamua kwenda hadi Chato kwa Baiskeli ili kutembelea Kaburi la Hayati Dr. Magufuli.

Shayo amesema ameamua kwenda Chato kutoa pole na kuonesha jinsi gani Wajasiriamali walivyoguswa na msiba huo na katika safari yake atakuwa anasaini vitabu vya maombolezo katika Wilaya zote atakazopita, pia kusalimiana na Wakuu wa Wilaya na Wabunge katika Ofisi zao za Majimbo na Wilaya.

Amesema anatumia Baiskeli mwanzo hadi mwisho na ameanzia safari yake mkoani Singida ilipo Familia yake akipitia Wilaya za Igunga, Nzega, Kahama mpaka atakapofika Chato.

Pia, safari yake ni ya kuwapa moyo Viongozi wa Kiserikali na Vyama vya Siasa na kuwakumbusha Wananchi kuhusu kufanya kazi kwa bidii ili kumuenzi JPM kwa vitendo.

#MillardAyoUPDATES #PumzikaBaba

0856e2ef-c764-4f82-808b-4a16210bfa39.jpg
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
7,079
2,000
Mjasiriamali gani huyo ambaye ana muda mchafu hivyo wa kuzurura na baiskeli?

Mzee alisema tuchape kazi, sasa kumuenzi ni kuchapa kazi tu, na sio kuzurula.
 

uchumi2018

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
818
1,000
Ni jambo zuri ,cha msingi akumbuke kwamba pori la biharamulo siku hizi kuna simba wasije wakamrestisha in peace tukaomboleza mara ya pili.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom