menny terry
JF-Expert Member
- Mar 18, 2011
- 509
- 667
Bado tupo kwenye siku 21 za maombolezo kufuatia kifo cha Hayati Dr. John Pombe Magufuli, John Shayo ni Katibu wa Wajasiriamali wanaofanya biashara Magufuli Bus Terminal Mkoani Dar es Salaam ambaye ameamua kwenda hadi Chato kwa Baiskeli ili kutembelea Kaburi la Hayati Dr. Magufuli.
Shayo amesema ameamua kwenda Chato kutoa pole na kuonesha jinsi gani Wajasiriamali walivyoguswa na msiba huo na katika safari yake atakuwa anasaini vitabu vya maombolezo katika Wilaya zote atakazopita, pia kusalimiana na Wakuu wa Wilaya na Wabunge katika Ofisi zao za Majimbo na Wilaya.
Amesema anatumia Baiskeli mwanzo hadi mwisho na ameanzia safari yake mkoani Singida ilipo Familia yake akipitia Wilaya za Igunga, Nzega, Kahama mpaka atakapofika Chato.
Pia, safari yake ni ya kuwapa moyo Viongozi wa Kiserikali na Vyama vya Siasa na kuwakumbusha Wananchi kuhusu kufanya kazi kwa bidii ili kumuenzi JPM kwa vitendo.
#MillardAyoUPDATES #PumzikaBaba