ADVOCATES: Mbona hivo jamani???

ADVOCATES: Mbona hivo jamani???

bht

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2009
Posts
10,336
Reaction score
1,883
Hawa Learned Proffession:

nakwazika sana mnapotumia kiingereza mahakamani na upande mwingine masikini ya Mungu mtanzania mwenzio hata hajui unaongelea nini!!! (na anajiwakilisha mwenyewe)

sijui decree
siju P.O!!!
SIJUI STAY OF EXECUTION PENDING WATEVER!!!

Jamani huwa nasikitishwa sana na naendelea kusikitika!!

waheshimiwa kama mnaona hayo kwa nini msiwaambie mawakili watumie kiswahili???? kwa manufa yetu sote
 
1..Wanaonyesha kwamba wana fani iliyoenda shule..si unajua ili uonekane umesoma lazima uweke ile maneno?(msisitizo)..................2..Ni utamaduni wa kibongo, si umewasikiliza wabunge wanavyowekezea hii mambo wakiwa pale mjengoni?...........................3..Baadhi ya maneno kwa uhakika hayana Kiswahili chake (kisheria), na ni lazima yatamkwe hivyo!
 
PJ nafahamu kuna maneno kisheria huna uchaguzi bali kuyatumia yalivyo, hilo ni wazi
ninachokizungumzia hapa ni kutumia kiingereza bila umuhimu wowote
yaani kiswahili kingetumika bila mkwamo wowote afu wewe unang'ang'ana umombo
 
Jamani Sheria Zetu Mwajua Ziko Kwa Lugha gani?
 
Jamani Sheria Zetu Mwajua Ziko Kwa Lugha gani?

..Hilo liko wazi, lakin shida inakuja pale wakili anapojibishana na MSAFWA, kihiyo asiye na wakili!...Kumtamkia maneno ya kisheria ni kumpigia mbuzi gitaa, na kumpanikisha aonekane ni MKOSEFU however!
 
Jamani Sheria Zetu Mwajua Ziko Kwa Lugha gani?

Kiingereza
lakini tumekatazwa kutumia kiswahili hasa linapokuja suala kwamba mdau mwingine haelewi unaongea nini?

basi tuwekewe huduma ya mkalimani (siku moja tuligawiwa vipeperushi mahakama ya kazi vinavyohusu mahakama hiyo (hapa mtu unaweza kupata picha wateja wengi wa mahakama hii) mi nikamweleza karani kuw asielewi lugha ilotumika akaniambia hivo hivo ukiambulia neno inatosha) mweee!!
 
..Hilo liko wazi, lakin shida inakuja pale wakili anapojibishana na MSAFWA, kihiyo asiye na wakili!...Kumtamkia maneno ya kisheria ni kumpigia mbuzi gitaa, na kumpanikisha aonekane ni MKOSEFU however!

asikwambie mtu.....this thing 'frustrates'

unamwangalia mtu mpaka unatamani kulia kwa niaba yake
 
bht asikwambie mtu sisi members wa hii noble profession tuna bahati mbaya sana., hatuna tofauti na ndugu zetu W.A.H.A.Y.A linapokuja suala la kuchanganya lugha
 
shem bht wewe naamini ni mwansheria(advocate) lakini unapopatwa na uchungu kuwahurumia watanzania wenzio wasioambulia kitu, nakupa hongera sana......... tena ujue kuwa si wale vihiyo tu, bali hata walioenda shule wanapata shida kwani tasnia nzima ya sheria ina "lugha yake" ndiyo maana hata ms word huwa baadhi ya maneno inaonyesha ni mageni kwake lakini yako kwa usahihi............. pia chukulia maana ya maneno "defence, sentense, cost, capital, learned, ruling etc" yakitumika nahakamani huweza kubeba maana tofauti na yakitumika uswahilini............. kweli utumwa ni mzigo..............
 
PJ nafahamu kuna maneno kisheria huna uchaguzi bali kuyatumia yalivyo, hilo ni wazi
ninachokizungumzia hapa ni kutumia kiingereza bila umuhimu wowote
yaani kiswahili kingetumika bila mkwamo wowote afu wewe unang'ang'ana umombo

Bht,
hujaona viroja bado... wakili anaongea kiingereza na kusema ni lugha ya mahakama - ambayo ni kweli... upande usiokuwa na wakili hajui aa wala bee ya kiingereza... Mheshimiwa anamwambia karani wa mahakama atafsiri.... karani naye inglishi not richabo!
Patamu hapo...
 
Kiingereza
lakini tumekatazwa kutumia kiswahili hasa linapokuja suala kwamba mdau mwingine haelewi unaongea nini?

basi tuwekewe huduma ya mkalimani (siku moja tuligawiwa vipeperushi mahakama ya kazi vinavyohusu mahakama hiyo (hapa mtu unaweza kupata picha wateja wengi wa mahakama hii) mi nikamweleza karani kuw asielewi lugha ilotumika akaniambia hivo hivo ukiambulia neno inatosha) mweee!!

Dada Bht, naona kuna mahali unawaonea hao jamaa zetu. Sheria zimeandikwa kwa kithungu, watungaji nao wanaongea Ingilishi (badala ya English) na shule pia wanafundishwa hicho hicho. Pia kama hukijui ni aibu. Sasa nani yuko tayari kuibeba hiyo aibu? Nadhani kuna mahali inabidi yai au kuku vitafutwe ili kupata suluhisho.
 
Tatizo hilo sio kwenye sheria tu.

Majuzi wakati barabara ya Uhuru inafanyiwa matengenezo wakuu wakafunga njia kwa maneno "Road diverted" na mishale mingi ya kuelekeza njia mbadala. Watumiaji wenyewe wa barabara ile kwa kiasi kikubwa ni makonda ambao hawatumii hiki kiingereza chao, au magari ya mafuta yanaandikwa "Inflamable Liquid Gas." Matokeo yake watu wanaiba mafuta kwenye vifuko vya rambo wakati wa foleni.
 
mwishowe unakuja kuta maganga kama ndio mlalamikiwa akiulizwa kila kitu anakubali tu, kumbe hajaelewa,mpaka akipigwa nyundo ya mvua ndio anashtuka na kuanza kukimbilia kukata rufaa,kwanini wasiweke mkalimani??
 
Back
Top Bottom