Hizo ni ndoto za kyenda wazimu, tatizo letu ni uelewa mdo na kukaririshwa maneno, wenye akili timamu wanataka hoja na si mambo ya mtaani, mtu kanywa gongo zake huko anakurupuka na kusema ccm ni adui, maana yake imetangazwa vita au ndo mpango wenyewe huo, kama watu hawajapata dola wanachachawa hivi je wakiipata si itakuwa balaa tupu, hii nchi iko huru na vyama vyote vipo kwa mujibu wa katiba yetu. chama kinaondoka kwa utaratibu na si kwa jinsi hiyo ya kilevilevi. Je huko unakofikiri kwamba kuna asali na maziwa, umewafanyia utafiti na kujilidhisha kuwa wanaweza? au unapigwa saundi ya mdomo2 na unawaamini, utauziwa mbuzi kwenye gunia na utakuwa wa kwanza kutujuza ndani ya JF.