Adsense , infolinks , adbrite na clicksor | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adsense , infolinks , adbrite na clicksor

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Mar 8, 2011.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mara kadhaa nimekuwa nazungumzia mifumo ya matangazo kwenye mtandao kwa kutaja zaidi Adsense na jinsi watu au makampuni yanavyoweza kufaidika na mfumo huu kwa kuweka nafasi za matangazo kwenye tovuti zao , blogu , majukwaa na sehemu nyingine kwenye mtandao zinazoweza kuangaliwa au kutembelewa na watu katika shuguli zao za kila siku .


  Nimeongezea Infolinks , Adbrite na Clicksor kama mifumo mingine ya utangazaji kwa njia ya mtandao ambapo pia nyingi sasa zimehamia kwenye mifumo ya simu za mikono na vifaa vingine vya mkono vinavyoweza kutumika kutembelea mitandao na kufungua kurasa za mitandao mbalimbali .


  Infolinks ni mfumo mpya kidogo wa matangazo hauna miaka mingi wenyewe unatumia zaidi MANENO au NENO au SENTESI katika kutangaza bidhaa au vitu mbalimbali kwenye mtandao lakini pia inategemeana na lugha mfano kwa sasa lugha ya Kiswahili haijaingizwa rasmi kwenye mtandao wa INFOLINKS hii maana yake kama una tovuti au blogu ukatumia lugha ya Kiswahili infolinks haitoweza kuweka matangazo yake kwenye kurasa za tovuti au blogu hiyo .


  Kwa ufupi wanaofaidika zaidi na infolinks ni wale wenye tovuti zenye lugha za kimataifa zinazozungumzwa na watu wengi na ambazo wengi hutumia kutafuta vitu kwenye mtandao kama kifaransa , kiingereza , kigerumani na nyingine ambazo zinaendelea kuingizwa sasa .


  Wakati Adsense ni matangazo yaliyowekwa kwenye frame maalumu , infolinks ni matangazo yanayoonekana ndani ya kurasa kwenye baadhi ya maneno au neno kwenye sentensi inayohusu kitu fulani mfano neno I LOVE AFRICA – Neno Love linaweza kuwa tangazo na likaunganishwa na tovuti inayoitwa LOVE.COM au inayohusiana na neno la LOVE ,na AFRICA ikaunganishwa na tovuti inayohusu Africa kama African Roots .com na nyingine nyingi .


  Malipo ya infolinks hutoka kila mwisho wa mwezi kama Pato lako ni zaidi ya dola 100 kwa njia ya paypal na 400 kwa njia ya cheki lakini pia unaweza kuchagua kutengeneza ATM CARD ya Infolinks ambayo utakuwa unatumia kuchukulia pesa kwenye mashine zote zenye mfumo wa VISA .
  ADBRITE
  Adbrite ni kama Adsense kwa muonekano wake , wakati Adsense inategemea matangazo toka kampuni ya Google kutumia mawakala wake , Adbrite inampa nafasi mtangazaji kwenda kwenye tovuti au blogu yenye Adbrite na kuweka Tangazo lake mwenyewe pamoja na bei anayopenda kutangazia tangazo hilo .


  Unapojiunga na Adbrite kazi yako ni kutengeneza Sehemu za kuweka matangazo ya watu mbalimbali kwenye kurasa za tovuti au blogu halafu watu au kampuni zikipenda eneo hilo ndio litaweka tangazo lake hapo na utalipwa kwa mfumo wa Kibenki au Cheki kutokana na jinsi ulivyouza matangazo kwa mwezi huo .


  CLICKSOR
  Clicksor ni mfumo wa matangazo pia lakini huu unatumia kurasa nzima na mfumo wa popup kama mnavyojua kuna program nyingi za kufanya popup zisifanye kazi hii ndio ubaya mmoja wa clicksor , lakini unapoweka kwenye tovuti basi mtu akigonga mapato unapata makubwa na unaweza kutangaza bidhaa nyingi kwa wakati mmoja kwa urahisi .


  USHAURI WANGU
  Matangazo yote hayo ni rahisi kuweka kwenye kurasa za tovuti au blogu lakini ili yafanye kazi vizuri na upate kipato cha angalau dola 20 kwa siku moja lazima tovuti au blogu hiyo itembelewe na watu zaidi ya 700 kwa dakika ambao pengine ndio wanaweza kugonga matangazo yako na kufanya uongeze kupato kutokana na kutangaza huko .


  Shuguli hizi zinahitaji uvumilivu wa hali ya juu na umakini sana wa kufuata sheria za matangazo kwa njia ya mtandao ambapo kila kampuni ina sheria na taratibu zake lakini vile vile kuzingatia mila na desturi za sehemu husika ambapo tovuti yako inaangaliwa zaidi .
   
 2. SamJet

  SamJet Senior Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 165
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimekua nikitumia adsense kwa muda sasa (ilegally since i was 16 to legal *now 19) na nikifananisha adsense na adwords, naona bora adsense. Why??

  Infolinks and Google Adsense Comparison: Income Plus Look and Feel


  My team and I have been experimenting with Infolinks and Google Adsense ads for a few weeks now. This is in our attempt to increase our revenues from the sites that we maintain. However, we deleted the Infolinks codes from my sites today because of the following reasons:
  1) My sites (because I still own and administer them) are not designed for Infolinks ads because I or any of my team members do some internal linking to our previous posts. Thus, the Infolink ads are sometimes sore to the eyes. I myself find the double underline words or phrases obtrusive. In this site, I have placed the codes for one day but removed it in less than 5 hours. I just wasn’t comfortable looking at my sites with too many underlined words/phrases. The look and feel of this site has gone from bad to worse (in my view).
  2) Infolinks vs Adsense Income. After reviewing the income we generated for 16 days, we have come up with the conclusion that Infolinks ads income is terribly lower than Adsense. In fact, our Adsense income is 3 times that of our income from Infolinks (taking the average eCPM and CPC for 16 days). In view of this, I have decided to discontinue using Infolinks in all the sites that I own. This does not mean though that I’m making thousands of dollars monthly from Adsense. Nah, that would take years more to achieve (if I will still continue publishing articles or blogging in the future) [​IMG]
  While others might disagree with these findings, my decision is firm and will remain the same. Some might claim that Infolinks is a good source of additional income. The truth is, that is a relative claim. Some “really big sites” I visit do not even use Adsense. Others rely solely on Chitika. Others make a killing on affiliate marketing.
  You see, based on my experiences in making money online, I have tried almost all types of advertisements in this site and other sites I own. Many factors affect the way an online publisher makes money with his website. In my case, I have been most effective in making money doing paid blogging. I have earned more than $5k reviewing products, articles and websites for PPP, SR, Reviewme, Buybogreviews, etc. I have tried most of them and have made some money I could use for my offline businesses and research. Paid blogging helped me finance some “charitable works” offline. While this is true in my case, others make a good sum of money serving contextual ads like Google Adsense, Infolinks, Kontera and non-contextual ads like Chitika, Widgetbucks (don’t use this), Amazon affiliate marketing, et al.
  In my opinion, making money online is finding the right way (or ways) to make money online. Looking from a distance, it’s just one big experiment. It’s a long-term trial and error. If one source of income is effective in your case, then I suggest you keep that, or else drop it. For one, it will only consume your site’s space, bandwidth and most probably, your precious time. For another, why keep something not worth keeping. [​IMG]
   
Loading...