Admin wa Tume Huru ya Taifa Uchaguzi amefanya kwa Makusudi au ndio ukweli? Chapisho lililopo kwenye tovuti lina makosa ya uandishi!

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
780
Reaction score
1,831
Tume huru ya uchaguzi wametoa chapisho ambalo lina makosa ya kiuandishi jambo ambalo sio la kawaida kwa taasisi..
kwanza kabisa mwanzoni linasomeka hivi....

Tume Huru ya Taifa ya Uchafuizi imetangaza kuwa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika Siku ya Jumatano ya tarehe 29 Oktoba, 2025​





Mara baada ya hapo kuna muendelezo wa chapisho hilo kama ifuatavyo
Tume Huru ya Taifa ya Uchafuizi imetangaza kuwa Siku ya Jumatano ya tarehe 29 Oktoba, 2025 ndio itakuwa Siku ya Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani kwa Tanzania Bara ambapo jumla ya wapiga kura 37,655,559 wamejiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele kwenye hafla ya uzinduzi wa ratiba ya uchaguzi iliyofanyika kwenye makao makuu ya Tume, Njedengwa jijini Dodoma.

β€œTarehe 09 Agosti, 2025 hadi tarehe 27 Agosti, 2025 itakuwa utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais. Tarehe 14 Agosti, 2025 hadi tarehe 27 Agosti, 2025 itakuwa utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani na tarehe 27 Agosti, 2025 itakuwa siku ya uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais, uteuzi wa wagombea ubunge na uteuzi wa wagombea udiwani,” amesema Mhe. Jaji Mwambegele.

β€œTarehe 28 Agosti, 2025 hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kitakuwa kipindi cha kampeni za uchaguzi kwa Tanzania Bara. Tarehe 28 Agosti, 2025 hadi 27 Oktoba, 2025 kitakuwa kipindi cha kampeni za Uchaguzi kwa Tanzania Zanzibar ili kupisha kura ya mapema na Tarehe 29 Oktoba, 2025 siku ya Jumatano itakuwa ndiyo Siku ya Kupiga Kura”., ameongeza Mhe. Jaji Mwambegele.

Akazingumza kuhusu idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi huo, Mhe. Jaji Mwambegele amesema jumla ya wapiga kura 37,655,559 wamejiandikisha na kuongeza kuwa idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 26.55 kutoka idadi ya wapiga kura 29,754,699 waliokuwa kwenye daftari, mwaka 2020.

Ameongeza kuwa kwa upande wa Zanzibar, Wapiga Kura 725,876 wapo katika Daftari la Wapiga Kura la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na wapiga kura 278,751 wameandikishwa na INEC kwa kuwa hawakuwa na sifa za kuandikishwa na ZEC.

β€œKatika idadi ya wapiga kura 37,655,559 waliopo katika daftari, wapiga kura 36,650,932 wapo Tanzania Bara na wapiga kura 1,004,627 wapo Tanzania Zanzibar,” amesema Jaji Mwambegele.

Ameongeza kuwa kati ya wapiga kura hao, 18,943,455 ni wanawake sawa na asilimia 50.31 na wapiga kura 18,712,104 ni wanaume sawa na asilimia 49.69 na wapiga kura 49,174 ni watu wenye ulemavu.

Amesema jumla ya vituo 99,911 vitatumika kupigia kura ambapo vituo 97,349 vitatumika kwa ajili ya kupigia kura kwa Tanzania Bara na vituo 2,562 vitatumika kwa ajili ya kupigia kura kwa Tanzania Zanzibar.

β€œIdadi hii ya vituo 99,911 ni sawa na ongezeko la asilimia 22.49 ya vituo vya kupigia kura 81,567 vilivyotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020,” amesema.

Jaji Mwambegele ametoa wito kwa wadau wote ikiwa ni pamoja na wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa kuzingatia sheria, kanuni, miongozo na maelekezo yatakayotolewa na Tume.

======

Tume wamerekebisha kosa la uandishi lililokuwepo kwenye chapisho hilo na sasa linasomeka vizuri kama inavyoonekana hapa chini:

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kuwa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika Siku ya Jumatano ya tarehe 29 Oktoba, 2025

 
Rudia kusoma ,nchi hatuna tume huru ya uchafuzi
Nimesoma...

Unachopaswa kueleza ni kuanisha kosa specific ili tuelewe kwa urahisi...

Mimi naona umekopi na ku paste tu taarifa nzima nzima hivyo hivyo ilivyo ya tume bila kubainisha hayo makosa ya kiuandishi wakati wewe ndo unasema umeona makosa...

Sema, makosa gani hayo?
 
Soma kwa makini
 
Uchafu-izi au alimaniisha uchafu-inzi...

Hawana mhariri hawa ndugu zetu?

Niliwahi kusoma kitabu cha WIZARD OF THE CROW cha Prof Ngugi...

Kilikuwa na vimaneno kama hivi...

MTUKUTU RAHISI... akimaanisha(MTUKUFU RAIS) Kwamba yule muongeaji mzee alikuwa anakosea ila ukweli alikuwa hakosei...

Sasa inakuwaje ukosee hivi kwenye uandishi wa tovuti ya tume huru?

Nawaza tu.
 
Usijali, kwenye katiba ya jamhuri ya muungano haiitambui "TUME HURU YA UCHAGUZI" bali inaitambua "TUME YA UCHAGUZI". Hiyo ni taasisi nyingine tofauti na Ile itakayosimamia uchaguzi mkuu
 
Soma kwa makini
Huelewi nini?

Kwanini unaanzisha jambo usiloweza kuliweka ktk clarity yake na uweze kulitetea kwa mifano halisi...???

Narudia tena, mimi sioni kosa lolote. Wewe umeona makosa, basi yabainishe tuyaone wote...

Kama ishu ni takwimu za wapiga kura walioandikishwa, hilo tumelihoji na linahitaji justification zaidi juu ya usahihi wa takwimu hizo...

Otherwise, wewe bado unatakiwa uoneshe hayo makosa mengine yaliyokufanya uanzishe mjadala huu...!!
 
TATIZO LIKO HAPO
Ameongeza kuwa kwa upande wa Zanzibar, Wapiga Kura 725,876 wapo katika Daftari la Wapiga Kura la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na wapiga kura 278,751 wameandikishwa na INEC kwa kuwa hawakuwa na sifa za kuandikishwa na ZEC.
  • wapiga kura 1,004,627 wapo Tanzania Zanzibar,” amesema Jaji Mwambegele.​
 
Mkuu ngoja nikusaidie kwenye Taaluma ya uandishi wa habari hasa print media ambayo inahusisha online writting ni kosa kubwa sana taasisi kubwa kukosea kimaandishi tangu jana chapisho liwekwe hadi leo chapisho halijafutwa au kuwekuwa masahihisho
Maana kadri unavyo liacha lianzidi kuzalisha maana ambayo inaleta changamoto hivyo kuzalisha maswali mengine kidhani
kwa Mantiki hiyo Tume huru ya uchaguzi wanatakiwa kuja na kusahihisha mbele za umma kwamba hilo chapisho limekosewa au liko sahihi ...
kadri wanavyo chelewa kuja kufanya masahihisho au kutoliondoa kabisa ndio linajenga sifa mbaya kwa kitengo cha habari ndani ya INEC
Nakupa mfano kwenye kuandika Headline kuna makosa kama ifuatavyo...........

Tume Huru ya Taifa ya Uchafuizi imetangaza kuwa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika Siku ya Jumatano ya tarehe 29 Oktoba, 2025​

Makosa yako wapi Baada ya kuandika UCHAGUZI wameandika UCHAFUIZI ....
Baada ya hapo kwenye Lead ya story yao wamerudia makosa yaleyale ....kwa mfano...
Tume Huru ya Taifa ya Uchafuizi imetangaza kuwa Siku ya Jumatano ya tarehe 29 Oktoba, 2025 ndio itakuwa Siku ya Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani kwa Tanzania Bara ambapo jumla ya wapiga kura 37,655,559 wamejiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

NOTE ..
kwanza unajiuliza hadi leo chief editors ,sub editors and content editors wa hii websites wako wapi tanga waweke chapisho hili mtandaoni ...
ukitaka kufahamu kuwa kukosea jina au kicho chochote kwenye uandidhi wa habari ni hatari kwa afya ...omba chombo chochote kiancho husika an magazeti kikosee kuandika jina la SAMIA SULUHU HASSANI kiandike Tofauti na jina lilivyo
ndivyo utakavyojua kuwa kesi ya defamation huwa inafanaya kazi
asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…