Nilikatiza njia ya shortcut ndani ya kambi ya jeshi ile nafika kwa uwanja mara pah naona raia wenzangu wameinamishwa chini wameshika masikio.
***** nilikuwa na dogo nimemshikilia kwa mkono nikasema nikirudi tu hawa jamaa hawaniachi, nikaamua kuendeleza mwendo kupita pale pale wengine wameinamishwa, ile nimewakaribia nikamkazia macho yule mwamba naye akanikazia, nikaonesha ishara ya salamu kwa kichwa akaniangalia nikapita.
Aiseeeee hii siku sinto isahau manake ningeshikishwa masikio mbele ya mtoto sijui ingekuaje.
Hao wanao nyanyaswa na JW ni wanafunzi na wanyarugusu waliotoka kijijini leo.Hawa jamaa ni shida Kuna siku jamaa yangu alijichanganya huko kambini akapewa adhabu ya kuhamidha tofali 500 kuxitoa upande mmoja ma kuxipeleka upande mwingine akapambana na kuweza kuhamisha tofali 350 huku jasho likiwa limemtoka gafla akaonana na ndugu yake ambae ni mjeda na ana cheo kikubwa akamwelezea kosa na adhabu aliyopatiwa akawa anamuomba msaada huyo mjeda akasema nitakusaidia usijali hebu rudisha hizo tofali ilipozitoa nafikiri tatizo litakuwa limeisha! Da jamaa aliishiwa pozi
Watoto wa maskini wakiingia jeshini wanawaza kutesa maskini wenzao.Sasa hivi sifa ni pesa sio upot, aje na upot wake aje na mwenye pesa zake hata Dem, alaf tuwafungulie mbwa wakali tuone ni nani atakaeng'atwa
yani hapo lazma pot ang'atwe na upot Wake maana hana pesa.
Hao wanao nyanyaswa na JW ni wanafunzi na wanyarugusu waliotoka kijijini leo.
Jw mpaka akupe adhabu mpaka wawe wengi pia anaangalia na aina ya mtu.
Mara mbili nilishuhudia hao jw wakisalimisha maisha yao kwa mbio baada ya kupokea kipondo kutoka kwa mbabe mmoja
Ulimuweza kweliii yaan.Kuna bwege mmoja nae eti ni mwanajeshi....
Alinikuta road nimekula pens ya jeshi la US jamaa sijui tamaa akaipenda pens ile kaja kasimamisha pikipiki yake.Akaniita kibabe sana ww njoo hapa mm nilimsikia Ila nikajifanya sijamsikia maana nilikuwa nimesimama na wadau tunapiga story za kulaumu serikali.Wadau wakanishtua oya unaitwa nikawajibu nimemsikia achaneni naye hawezi kuniita kidharau vile halafu na Mimi niende.
Mara paap jamaa akaanza kusogea mdogo mdogp nikaona mara wadau wanaanza kusogea pembeni taratibu jamaa akafika huyu hapa namwangalia naona naona Hana cheo chochote mabegani wala mkononi nikajua hapa na dili na private.
Kafika anaanza kusema dogo nakuita unaleta mapuuza huku ananishika bega kidharau....nikamjibu sijakusikia afande huku natoa mkono wake began kwangu nikamwambia niambie nikusikiliza (Ila nilijua tu hapa ishu ni hii pens ya kijeshi).....
Mjeda: mbona unavaa nguo zetu
JkT: Nguo zenu zipi afande
Mjeda : Dogo unajibu jeuri sio
JKT: ujeuri kukuuliza nguo zenu zipi (hapo akaona simwogopi namkazia,wambea wako kwa mbali wanaongezeka)
Mjeda uchwara: naomba hiyo pens uliyovaa
JkT: nikatabasamu nikamwambia hii mbona sio nguo zenu JW au unataka tu kunidhalilisha kumbe ilikuwa Kosa kumletea unyonge
Mjeda uchwara: Dogo unanipotezea muda
JKt: Nikambadilikia na Mimi nikamwambia kama umeingia Tamaa unataka hii pens sio ishu nitakupa Ila mpaka unitafutie nguo mbadala ya kuvaa
Mjeda uchwara: unassema !!?
JkT: kama ulivyosikia sikupi hii nguo mpaka unipe kwanza nguo nyengine au unataka raia wa jamhuri ya Tanzanis nitembee uchi...sikia force namba yako na jina lako nishavichukua.fanya unachotaka kufanya afande hii nguo sivui mpka unipe nguo nyingine.
Mjeda uchwara: kimyaaaa
JkT:Afande me nataka kusepa Nina ratiba zengine kama unachukua pens nambie.
Mjeda uchwara: kimyaaa alajipigia simu na kwenda kwnye pikipiki yake na kusepa.
Jkt: huyo nikaelekea mtaani kivua nguo yao isiniletee nuksi.
Hawa mabwege(wanajeshi uchwara wasiojitambua) watawaonea wajinga wajinga.
Kwa kitu kama hichi na namna uliyofanya ni sahihi kabisa, huu uonevu wa kombati hautakiwi ila kwa yule aliyeziba geti na kufanywa kitu kile ajilaumu mwenyewe maana jamaa hawana ujuaji wakiwa eneo lao la kazi. Nilishawahi shuhudia mjeda akiwapigia mateke ya uso washkaji zake kisa kumletea ujuaji eneo la kazi.Kuna bwege mmoja nae eti ni mwanajeshi....
Alinikuta road nimekula pens ya jeshi la US jamaa sijui tamaa akaipenda pens ile kaja kasimamisha pikipiki yake.Akaniita kibabe sana ww njoo hapa mm nilimsikia Ila nikajifanya sijamsikia maana nilikuwa nimesimama na wadau tunapiga story za kulaumu serikali.Wadau wakanishtua oya unaitwa nikawajibu nimemsikia achaneni naye hawezi kuniita kidharau vile halafu na Mimi niende.
Mara paap jamaa akaanza kusogea mdogo mdogp nikaona mara wadau wanaanza kusogea pembeni taratibu jamaa akafika huyu hapa namwangalia naona naona Hana cheo chochote mabegani wala mkononi nikajua hapa na dili na private.
Kafika anaanza kusema dogo nakuita unaleta mapuuza huku ananishika bega kidharau....nikamjibu sijakusikia afande huku natoa mkono wake began kwangu nikamwambia niambie nikusikiliza (Ila nilijua tu hapa ishu ni hii pens ya kijeshi).....
Mjeda: mbona unavaa nguo zetu
JkT: Nguo zenu zipi afande
Mjeda : Dogo unajibu jeuri sio
JKT: ujeuri kukuuliza nguo zenu zipi (hapo akaona simwogopi namkazia,wambea wako kwa mbali wanaongezeka)
Mjeda uchwara: naomba hiyo pens uliyovaa
JkT: nikatabasamu nikamwambia hii mbona sio nguo zenu JW au unataka tu kunidhalilisha kumbe ilikuwa Kosa kumletea unyonge
Mjeda uchwara: Dogo unanipotezea muda
JKt: Nikambadilikia na Mimi nikamwambia kama umeingia Tamaa unataka hii pens sio ishu nitakupa Ila mpaka unitafutie nguo mbadala ya kuvaa
Mjeda uchwara: unassema !!?
JkT: kama ulivyosikia sikupi hii nguo mpaka unipe kwanza nguo nyengine au unataka raia wa jamhuri ya Tanzanis nitembee uchi...sikia force namba yako na jina lako nishavichukua.fanya unachotaka kufanya afande hii nguo sivui mpka unipe nguo nyingine.
Mjeda uchwara: kimyaaaa
JkT:Afande me nataka kusepa Nina ratiba zengine kama unachukua pens nambie.
Mjeda uchwara: kimyaaa alajipigia simu na kwenda kwnye pikipiki yake na kusepa.
Jkt: huyo nikaelekea mtaani kivua nguo yao isiniletee nuksi.
Hawa mabwege(wanajeshi uchwara wasiojitambua) watawaonea wajinga wajinga.
Milambo Barracks Tabora au wapi ?.We jamaa kama ni wewe kweli maeneo ya mirambo nisamehe sana 🤠🤠
Nguvu ya wanajeshi wa JW mara nyingi ipo katika umoja.Mara mbili nilishuhudia hao jw wakisalimisha maisha yao kwa mbio baada ya kupokea kipondo kutoka kwa mbabe mmoja
NaamMilambo Barracks Tabora au wapi ?.
Wew ndo uliempa kazi za mahovyo uyo dereva nachukia sana nyie wajeda vi here here wapenda sifaHawa Jamaa usiombe uingie kwenye 18 zao, utajuta kuwafahamu.
Siku moja Tulikuwa kwenye foleni ya kuelekea mjini, kuna jamaa wa Lori akaziba geti la kuingilia pale kambi ya Abdallah Twalipo uhasibu. MP akamfuata kistaarabu kabisa "mambo vipi Kaka?" Jamaa akaitikia "Safi kabisa afande". Afande akamuuliza hapa uliposimama si unajua Kama ni getini? Mwamba kwa kujiamini kabisa akaitikia ndiyo afande ila tatizo foleni haitembei, Sina jinsi, samahani sana.
Kama kawaida ya wanajeshi kujifanya wastaarabu kwenye matukio ya aina hii. Afande akamwambia sasa ndugu kwa kuwa foleni haiendi shuka tu hapa upumzike tupige stori, foleni ikitembea utaendelea na safari yako. Dereva wa Lori kwa mbwembwe akafungua mlango ashuke eti apumzike na wanajeshi. Hapo ndiyo 'ntiti' ulipoanza!!
MP akamwambia "kaka sijasema ushuke mlangoni, shukia dirishani" lilikuwa ni tukio la kuchekesha Sana kwa sisi wapita njia ila kwa lililomtokea lilikuwa ni tukio mbaya na la kufedhehesha.
Picha linaanza,gari anayoendesha jamaa ni Scania R 420,Chuma mpya kabisa ya Transit alafu imepanda hewani Kama farasi, imebeba mafuta inaelekea nje. Gari ikisimama dereva unamwona yule kuleee ghorofani. Sasa vuta picha dereva ameambiwa ashuke kupitia dirisha badala ya mlangoni. Sisi wengine wa pembeni Tulicheka Sana maana jamaa kwanza ni bonge alafu ili ashuke kwa kutumia dirisha inabidi ajikusanye awe Kama fungu la nyanya Kisha ndiyo atoe miguu nje. Ilimchukua karibia dakika 15 kushuka. Wakati huo MP alikuwa siriazi hacheki wala haongei. Yeye anamsubiri jamaa tu ashuke wapige stori. Dereva akadondoka chini Kama mzigo wa viazi mbatata vya Mbeya..Tiii!!
Suruali yote imechanika kwenye maungio ya miguu. Aliposhuka huku kijasho kinamtoka mjeda akaanza kupiga nae stori Kama hakuna kilichotokea "naona chuma imeshakunywa wese inasepa?" Dereva kinyonge akajibu yeah inaelekea Ndola, Zambia. Wakapiga stori Mara foleni ikafunguka magari yakaanza kutembea. Afande akamwambia dereva Sasa unaweza kwenda tu maana gari zinatembea. Dereva akatoa shukrani Kisha akaelekea kwenye gari yake asepe.
Cha ajabu wakati dereva anafungua mlango Mjeda akamwambia mzee baba si tulikubaliana tunapitia dirishani? Ahahahhaha kazi ya kupanda dirishani ikaanza tena. Nina uhakika Yule dereva alimtukana mjeda matusi yote ya hapa duniani ila kimoyomoyo.. Ile siku yule dereva hataisahau kamwe maishani.
Unakumbuka kisa chochote Cha wanajeshi na adhabu zao kwa raia pindi raia akijichanganya kwenye anga zao?