Adhabu ya viboko hutekelezwa wapi kati ya Mahakamani na Gerezani?

Mr pianoman

JF-Expert Member
May 22, 2019
2,550
6,108
Naomba kufahamu kuhusu hii adhabu na mahali inapotekelezwa mtu anapohukumiwa?

Pia ni makosa yapi ambayo mtu akiyafanya hupelekea kupewa hii adhabu?

Nani anatumika kuchapa viboko hivyo na hutumia kiboko gani; cha mti au ile ngozi?

Nahitaji pia kufahamu na mengine mengi unayoyafahamu kuhusu adhabu hii.

Asante.
 
Niko pale nasubiri wajuzi waje watupe somo
 
Naomba kufahamu kuhusu hii adhabu na mahali inapotekelezwa mtu anapohukumiwa?

Pia ni makosa yapi ambayo mtu akiyafanya hupelekea kupewa hii adhabu?

Nani anatumika kuchapa viboko hivyo na hutumia kiboko gani; cha mti au ile ngozi?

Nahitaji pia kufahamu na mengine mengi unayoyafahamu kuhusu adhabu hii.

Asante.
najua kwa ninyo yafahamu;
1 & 3: Adhabu hutolewa magereza na anayemchapa viboko ni afisa magereza mwenye cheo kuanzia assistant superintendent mbele ya daktari(mtoa huduma za afya)pamoja na hakimu- "kwenye vyeo vya maafisa wa jeshi,polisi na magereza sifahamu vizuri naweza kusahihishwa"
2:Makosa ambayo yanaweza kupewa adhabu ya viboko yameainishwa katika Sheria Ya Adhabu ya Viboko Sura ya 17"Corporal Punishment Act,Chapter 17",lakini mfano ni kama makosa ya madawa ya kulevya,ushirikina/uchawi,udhalilisha wa kingono na mengine mengi yameelezwa katika Sheria tajwa hapo .
 
Asante sana mkuu
 
Ngoja nikufaffanulie vizuri baada ya kuthibitika utahimili hivyo viboko utalazwa sehemu ukiwa umelalia tumbo makalio juu utavuliwa nguo na utafungwa hapo ulipolalia litachukuliwa blanketi litapakwa liquid fulani hivyo litakuwa bichi na litatandazwa makalioni mwako kuyafunika.Baada ya hapo sasa ndio viboko vitaanza kwa kutumia fimbo ya mti fulani ambayo inanesa na haivunjik.Ni viboko vya hatali sana utachapwa kuelekea idadi ya viboko ulivyohukumiwa japo wanaweza kusitisha iwapo itaonekana pengine unatokwa na damu.Pia kuna umri fulani ndio unapaswa kula viboko watu wazima miaka kama 60 70 80 hawachapwi hivyo viboko
 
Back
Top Bottom