kuchangumu
JF-Expert Member
- Apr 2, 2014
- 724
- 290
Wanaume wengi wanapobaini kuwa wapenzi wao wanawasaliti, hutunisha misuli kuonesha umwamba kwa kuwatwanga makonde wapenzi wao au kuwafanyia mbaya wale waliowanasa.
Lakini uchunguzi niliofanya unaonesha kuwa ubabe haukomeshi tabia ya usaliti.Kuna wengi ambao waliwafumania wake zao, wakawapiga na kuwajeruhi, lakini wakajikuta hawakukomesha tatizo,
zaidi ya kuwapa usugu wapenzi wao wa kuendeleza wizi tena kwa dharau na kejeli huku wakibembelezana kwa maneno haya: "mzushi kaenda kazini njoo sasa hivi Wapendanao Gesti" au "vipi yule bwegge alikuuliza jana ulipochelewa kurudi" Jamaa anaweza kumuuliza hivyo mke au mpenzi wa mtu.
Adhabu nzuri ya mpenzi anayekusaliti ni kumnasa live kwenye usaliti wake kisha kumpuuza huku wewe ukiendelea na mambo yako kama kawaida, ukifanya hivyo utakuwa unamtibu ugonjwa wake wa kupenda penda hovyo na hii ndiyo dawa hasa ya kumponya msaliti, lakini pia inasaidia kupunguza maumivu ya penzi. Kumchunga na kumlilia machozi hakusaidii.
Karibuni!