Dawa ya msaliti hii hapa, wala usiumize kichwa

Dawa ya msaliti hii hapa, wala usiumize kichwa

Lupamba's grandson

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2015
Posts
1,230
Reaction score
1,199
HII NDIYO ADHABU KUBWA YA MPENZI ANAYEKUSALITI

Wanaume wengi wanapogundua kuwa wapenzi wao wanawasaliti, wanatunisha misuli kuonesha umwamba kwakuwatwanga makonde wapenzi wao au kuwafanyia mbaya wale waliowanasa. Lakini uchunguzi wa watalaam wa mapenzi unaonesha kuwa ubabe haukomeshi tabia ya usaliti.

Wapo wengi ambao wamewafumania wake zao, wamewapiga na kuwajeruhi, lakini wakajikuta hawakukomesha tatizo, zaidi yakuwapa usugu wapenzi wao wa kuendeleza wizi tena kwa dharau na kejeli huku wakibembelezana kwa maneno kama vile:"mzushi kaenda kazini njoo sasa hivi Wanaenda zao Gesti au sehemu yoyote wanayoijua" au utasikia"vipi yule alikuuliza jana ulipochelewa kurudi"

Jamaa anaweza kumuuliza hivyo mke au mpenziwa mtu Katika hali ya kawaida usaliti ni jambo linalouma kwa kiwango kikubwa. Katika mapenzi hakuna suala la kuazimana mume/mke au mpenzi. Watu huazimana magari na pesa, lakini kwa mpenzi hakuna jasiri wa namna hiyo!Hivyo ndivyo inavyokuwa lakini, kupiga au kuachana baada ya kufumaniana kunasaidia?

Jibu ni kwa hakusaidii, kwasababu ukimpiga adhabu inaishia hapo hapo, kesho yake watakutana watakusaliti tena na kupozana machungu. Maamuzi ya kuachanaye hayasaidii kwani ukimwacha mpenzi wako hujamtibu, utakuwa umetoa mwanya wa yeye kuendelea kukusaliti na kukuumiza zaidi pale macho yako yatakapowaona wameshikana mikono mitaani kwa uhuru na raha zao.

Kwa sababu ukiamua kuua na wewe utauawa, huku wanadamu wenzako wakikucheka kwa uzembe wa kufikiri. Jamani usaliti upo kila siku, kwani si huwa tunawaona wake na wapenzi wa watu wanaingizana gesti kila siku? Sasa kama hujamfuma mpenzi wako leo kuna siku utakutana na meseji kali akibembelezana na ‘kidume chake' mwingine kwa maeneo fulani.

Utafanyaje baada ya kubaini hivyo, maana kama ni tukio basi utakuwa umeona lile la stejini laivu bila chenga. Twende pamoja ili tuelimishane kama wadau wa mapenzi njia sahihi ya kufanya ili kumwadhibu mpenzi msaliti. Kwanza, baada ya kuwaona usokwa macho wakisaliti penzi, unatakiwa kutoa ishara zitakazoonesha kuwa umewaona, halafu ondoka eneohilo.

Ukishafika home, mtu mzima nini pale endelea kunywa zako maji ili kupoza presha.Akirudi mpenzi wako jitahidi kumkaribisha kwa bashasha, lakini usimuulize ulichoona mwache aendelee kujiuliza mwenyewe. Au kama umenasa meseji za kimahaba kutoka kwa mwizi wako, zitume kwenye simu yako kwanza, halafu baada ya kumaliza uchunguzi wako mtumie tena sms hizo mkeo/mumeo.

Ukifanya hivyo usimuulize, endelea kumpenda na ikiwezekana ongeza matunzo. Nunua ‘mikuku' akaange kila siku na umpe penzi moto moto.Nakwambia ukifanya hivyo mpenzi wako ataumia sana na hatoweza kukusaliti kwa kwasababu atakuwa anawaza unafikiria kumfanya nini? Na kwa yule uliyemshika naye, vivyo hivyo usizozane naye, mwache! Utashangaa anahama eneo maana atakuwa anafikiri unamwandalia kombora kumbe wewe wala, umeamua kujituliza tu!Wadau wa mapenzi hii ndiyo dawa ya mtu msaliti.

Mwadhibu kwa upole, wanasaikolojia wameithibitisha adhabu hii ninayokweleza hivi sasa kuwa ina uchungu mara 1,000 zaidi ya kupiga au kukemea. Ukisemaumwache siyo dawa kwani unaweza kutafuta mwanamke/mwanaume mwingine nayeye akawa na tabia zile zile, sasa kama ikiwa utaamua kuacha, utaachana na wangapi katika maisha haya maana usaliti upo?

Adhabu ya mpenzi anayekusaliti ni kumnasa kwenye usaliti wake kisha kumpuuza huku wewe ukiendelea na mambo yako kama kawaida, ukifanya hivyo utakuwa unamtibu ugonjwa wake wa kupenda penda hovyo na hii ndiyo dawa hasa ya kumponya msaliti, lakini pia inasaidia kupunguza maumivu ya penzi. Kumchunga na kumlilia machozi kili siku hakusaidii.
 
nitakapomfuma nakata nywele zake zote na mkasi piga picha nakuwapa global publisher
 
Ushaur mzur sana ila yataka mwenye subra kwasababu fumaniz bwana mandaliz yk huwa hayapo natokea tu na adhabu inategemeana na eneo la tukio presha ya mapenz asikwambie mtu
 
Njia nzuri lakini utakuwa na ujasiri wa kuishinda hasira ya wakati huo?
 
Hii theory iko simple sana kuifanya ila itakapokuja practical yake utachemka mkuu, achana na moyo wewe
 
Kifupi inaitwa " Mental torture" haitokei ghafla, unatakiwa uwe na masters ya ukimya.
^^
 
Kazi kweli kweli
 

Attachments

  • 1430054455985.jpg
    1430054455985.jpg
    18.8 KB · Views: 1,292
Rahisi kuyasema na kuyaandika kama ulivyofanya hapa..!! Lakini si rahisi kufikiri kama unavyofikiri pindi ukikutana na hali hiyo tena kwa mtu unayempenda sana..

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Sio rahisi kihivo. Wachache sana wanaoweza. Binafsi cwez kukaa na kitu moyon. I might die of stress
 
ukiweza hivyoo ujuee soon utakuwa MAREHEMU maana MOYO utakuwa umechanikachanika we unajaribu kuunga kwa mi plasta/soletape........... yaan KIFO chaghafla
 
Hii njia inafanya kazi kwa mtu anayekupenda kwa dhati tu, ila km yupo tu utasumbuka bureee, i tried it once it worked then aliposahau tu nikamdump, he never forgot aliumia hadi kesho anasemaga
 
Kuna watu vichwa maji kweli kweli...
akiona mara ya kwanza umekazako kimya, kesho atarudia tena kwa kiwango cha juu zaidi huku akitamba bila hofu..
(hana lolote yule, kwanza haniwezi... atanifanya nini)
binadam wanatofautiana sana
 
Back
Top Bottom