Adhabu kubwa ya mpenzi anayekusaliti

Adhabu kubwa ya mpenzi anayekusaliti

gbefa

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2016
Posts
3,807
Reaction score
15,849
Wasaalamu wakuu,

Iko hivi kwa upande wa sisi wanaume wengi tunapobaini kuwa wapenzi wetu wanatusaliti, hutunisha misuli kuonesha umwamba kwa kuwatwanga makonde wapenzi wetu au kuwafanyia mbaya wale waliowanasa. Lakini uchunguzi wa wana mapenzi unaonesha kuwa ubabe haukomeshi tabia ya usaliti.

Kuna wengi ambao waliwafumania wake zao, wakawapiga na kuwajeruhi, lakini wakajikuta hawakukomesha tatizo, zaidi ya kuwapa usugu wapenzi wao wa kuendeleza wizi tena kwa dharau na kejeli huku wakibembelezana kwa maneno haya: “mzushi kaenda kazini njoo sasa hivi wapendanao Gesti” au “vipi yule ----- alikuuliza jana ulipochelewa kurudi” Jamaa anaweza kumuuliza hivyo mke au mpenzi wa mtu.

Katika hali ya kawaida usaliti ni jambo linalouma kwa kiwango kikubwa. Katika mapenzi hakuna suala la kuazimana mume/mke. Watu huazimana magari na pesa, lakini laazizi hakuna jasiri wa namna hiyo! Hivyo ndivyo lakini, kupiga au kuachana baada ya kufumaniana kunasaidia? Jibu hakusaidii, kwani ukimpiga adhabu inaishia hapo hapo, kesho yake watakaokutana watakusaliti tena kupozana machungu.

Maamuzi ya kuacha naye hayasaidii kwani ukimwacha mpenzi wako hujamtibu, utakuwa umetoa mwanya wa yeye kuendelea kukusaliti na kukuumiza zaidi pale macho yako yatakapowaona wameshikana mikono mitaani kwa uhuru na raha zao.

Ukiamua kuua na wewe utauawa, huku wanadamu wenzako wakikucheka kwa uzembe wa kufikiri. Jamani usaliti upo kila siku, si tunawaona wake na wapenzi wa watu wanaingizana gesti kila siku?

Hivyo, kama hujamfuma mpenzi wako leo kuna siku utakutana na meseji kali akibembelezana na ‘kidume’ mwingine kwa maeneo fulani. Utafanyaje baada ya kubaini hivyo, maana kama ni tukio basi utakuwa umeona lile la stejini laivu bila chenga. Twende pamoja ili tuelimishane kama wadau wa mapenzi njia sahihi ya kufanya ili kumwadhibu mpenzi msaliti.

Kwanza, baada ya kuwaona uso kwa macho wakisaliti penzi, unatakiwa kutoa ishara zitakazoonesha kuwa umewaona, halafu ondoka eneo hilo. Ukifika home mtu mzima endelea kunywa maji ili kupoza presha. Akirudi mpenzi wako jitahidi kumkaribisha kwa bashasha, lakini usimuulize ulichoona mwache aendelee kujiuliza mwenyewe.

Au kama umenasa meseji za kimahaba kutoka kwa mwizi wako, zitume kwenye simu yako kwanza, kisha baada ya kumaliza uchunguzi wako mtumie tena SMS hizo mkeo/mumeo. Ukifanya hivyo usimuulize, endelea kumpenda na ikiwezekana ongeza matunzo. Nunua ‘mikuku’ akaange kila siku na umpe penzi moto moto.

Nakwambia ukifanya hivyo mpenzi wako ataumia sana na hataendelea kukusaliti kwa kuwa atakuwa anawaza unafikiria kumfanya nini? Na kwa yule uliyemshika naye, vivyo hivyo usizozane naye, mwache! Utashangaa anahama eneo maana atakuwa anafikiri unamwandalia kombora kumbe wewe wala, umeamua kujituliza tu!

Wadau wa mapenzi hii ndiyo dawa ya mtu msaliti. Mwadhibu kwa upole, wanasaikolojia wameithibitisha adhabu hii kuwa ina uchungu mara 1,000 zaidi ya kupiga au kukemea. Ukisema umwache siyo dawa kwani unaweza kutafuta mwanamke/mwanaume mwingine naye akawa na tabia zile zile, ikiwa ndivyo utaacha wangapi basi katika maisha haya?

Adhabu ya mpenzi anayekusaliti ni kumnasa kwenye usaliti wake kisha kumpuuza huku wewe ukiendelea na mambo yako kama kawaida, ukifanya hivyo utakuwa unamtibu ugonjwa wake wa kupenda penda hovyo na hii ndiyo dawa hasa ya kumponya msaliti, lakini pia inasaidia kupunguza maumivu ya penzi. Kumchunga na kumlilia machozi hakusaidii.

Uwe na wakati mdau

Nawasilisha
 
Kwanza, baada ya kuwaona uso kwa macho wakisaliti penzi, unatakiwa kutoa ishara zitakazoonesha kuwa umewaona, halafu ondoka eneo hilo. Ukifika home mtu mzima endelea kunywa maji ili kupoza presha. Akirudi mpenzi wako jitahidi kumkaribisha kwa bashasha, lakini usimuulize ulichoona mwache aendelee kujiuliza mwenyewe.

Au kama umenasa meseji za kimahaba kutoka kwa mwizi wako, zitume kwenye simu yako kwanza, kisha baada ya kumaliza uchunguzi wako mtumie tena sms hizo mkeo/mumeo. Ukifanya hivyo usimuulize, endelea kumpenda na ikiwezekana ongeza matunzo. Nunua ‘mikuku’ akaange kila siku na umpe penzi moto moto.

Nakwambia ukifanya hivyo mpenzi wako ataumia sana na hataendelea kukusaliti kwa kuwa atakuwa anawaza unafikiria kumfanya nini? Na kwa yule uliyemshika naye, vivyo hivyo usizozane naye, mwache! Utashangaa anahama eneo maana atakuwa anafikiri unamwandalia kombora kumbe wewe wala, umeamua kujituliza tu!
Hiyo ni adhabu moja inayoumiza mno, ila yataka moyo kuitekeleza.
 
Hiyo ni adhabu moja inayoumiza mno, ila yataka moyo kuitekeleza.
Kunjua moyo mkuu kuna mambo huwa hayakwepi kama haya yaani ni kila mahali.. Na hii ndio dunia yetu so tuwe alert muda wowote ikitokea take easy
 
Mmmh mtoa mada tafadhali usije ukanipa kesi ya kujeruhi mi moyo huo sina
Hii adhabu inafanya kazi vizuri sana kwa anayeadhibiwa, tatizo ni kwamba inamwadhibu pia mtoa adhabu. (Inautesa sana moyo wa mtoa adhabu)
Kunjua moyo mkuu kuna mambo huwa hayakwepi kama haya yaani ni kila mahali.. Na hii ndio dunia yetu so tuwe alert muda wowote ikitokea take easy
 
Hii adhabu inafanya kazi vizuri sana kwa anayeadhibiwa, tatizo ni kwamba inamwadhibu pia mtoa adhabu. (Inautesa sana moyo wa mtoa adhabu)
Mkuu unaelewa kitu kinaitwa kunjua moyo!?
Then kumbuka ukipenda ni adhabu so ili uendane na muktadha inabidi ukubaliane na hali kingine adhabu hii inatesa pande mbili lakini ni yenye mafanikio makubwa sana ikitokea ikafanikiwa 100%
 
Yamkini sijui huko kukunjua moyo....tafadhali nieleweshe.
 
Yamkini sijui huko kukunjua moyo....tafadhali nieleweshe.
Kukunjua moyo ni kukubalina na hali halisi.. Sio hali ipo hivi ww unajisemea moyoni haiwezekani hapa na pale unafanya kitu kwa kutumia hasira
 
Mleta mada una mke/mume..??

Hii ipo applicable kwa girlfriend/boyfriend au mke/mume wa ndoa..??

Umeshawahi kumfumania mpenzi wako..??

Ulichoandika ni totally cha KUFIKIRIKA. Maamuzi ya nini utafanya HUWA YANAKUJA HAPO HAPO baada ya kuwakuta, huwezi kuyapanga kabla eti utafanya nini. Hizi ni just wishes, ila hubadilika unapokutana na tukio husika.

Hii ni sawa na mtu kusema "yaani mimi hata nikiwa na hela vipi, ntakuwa na gari moja tu ya kutembelea". Then unashangaa mtu huyo huyo, anakuja kuwa na gari 6, na wala haoni tatizo.

So, hakunaga jibu la moja kwa moja la nini kitafuata baada ya fumanizi. Akili yko itakavyokutuma hilo ndo jibu lenyewe.
 
Kukunjua moyo ni kukubalina na hali halisi.. Sio hali ipo hivi ww unajisemea moyoni haiwezekani hapa na pale unafanya kitu kwa kutumia hasira
Yaani umfume umpendae halafu moyo wako ukubaliane na hali haraka kiasi hicho,kwamba ni kawaida tu ngoja niongeze mapenzi kwake ili nimwadhibu.... Inawezekana ila mtoa adhabu atautesa moyo kwani ataishi kinafiki mno. Vinginevyo mtoa adhabu naye awe msaliti hivyo awe anapata faraja kwa mchepuko wake.

Ila yote katika yote hii ni adhabu nzuri mno inayofanya kazi vizuri mno,japo wakati mwingine hutoa matokeo tofauti na lengo la mtoa adhabu, kwani nimeshuhudia wengi wa wasaliti wakiishia kuwakimbia watoa adhabu kwa kuhofia maisha yao.
 
Ogopa sana mtu mkimya hujui anawaza nini au anapanga kufanya why do u get scared!? hapo lazima mtu ajifunze kwa tahadhari kubwa.. Kingine uenda mfumaniwa hata akakimbia kwa kuwa ana imani tena sasa unaisi anajisikiaje!?
 
Mleta mada una mke/mume..??

Hii ipo applicable kwa girlfriend/boyfriend au mke/mume wa ndoa..??

Umeshawahi kumfumania mpenzi wako..??

Ulichoandika ni totally cha KUFIKIRIKA. Maamuzi ya nini utafanya HUWA YANAKUJA HAPO HAPO baada ya kuwakuta, huwezi kuyapanga kabla eti utafanya nini. Hizi ni just wishes, ila hubadilika unapokutana na tukio husika.

Hii ni sawa na mtu kusema "yaani mimi hata nikiwa na hela vipi, ntakuwa na gari moja tu ya kutembelea". Then unashangaa mtu huyo huyo, anakuja kuwa na gari 6, na wala haoni tatizo.

So, hakunaga jibu la moja kwa moja la nini kitafuata baada ya fumanizi. Akili yko itakavyokutuma hilo ndo jibu lenyewe.
Mkuu nimetumia logic(based on experience) lakini kama unaona siko sahihi leta nondo zako hapa then tufanye comparison
 
kuna watu hata uwaoneshe mabaya yao kwa njia ya upole kama iyo bado wataendelea na kuhisi ww hujiwezi juu yake.

dawa ni kuzaa na ndugu yake tu iwe dada, binamu ama yeyote yule. eeeh jino kwa jino
 
Back
Top Bottom