Adha ya usafiri ruti ya Mawasiliano - Mbezi Louis

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,510
4,224
Ni muda mrefu sasa uongozi wa jiji umekuwa ukilifumbia macho tatizo hili la kukosekana kwa usafiri wa daladala kati ya Mawasiliano na Mbezi.

Watu wanajaa na kukaa muda mrefu kituoni wakiwemo wanafunzi na wamama wajawazito wakisubiri daladala ambazo hazipo kwa kigezo cha kulazimisha kuunga trip au kupanda mwendokasi na ubaya zaidi ni kuwa hakuna mwendokasi ya Mawasiliano - Mbezi.

Si sahihi kuondoa magari ya Mbezi maana hata machache yanayotoka Makumbusho huwa yamejaa yanapofika Mawasiliano.

Naamini daladala zipo za kutosha isipokuwa ni uongozi kutokujua namna ya kuzigawa na kusababisha mateso kwa raia.
 
Aseee hiyo njia ni janga ni hakuna kabisa daladala za Mawasiliano-Mbezi hasa mida ya jioni ya watu kutoka maofisini kurudi majumbani, ukitaka urahisi upande bajaji au kama ni una lengo la kufika hadi mbezi halafu uende njia ya malamba mawili ni bora mara elfu kumi upande daladala za Segerea kisha ukapande za mbezi ukitokea segerea la sivyo hapo mawasiliano utakesha
 
Panda gari za tegeta ushuke mpakani, upande gari za Mbezi kupitia chuo.
 
Aseee hiyo njia ni janga ni hakuna kabisa daladala za Mawasiliano-Mbezi hasa mida ya jioni ya watu kutoka maofisini kurudi majumbani, ukitaka urahisi upande bajaji au kama ni una lengo la kufika hadi mbezi halafu uende njia ya malamba mawili ni bora mara elfu kumi upande daladala za Segerea kisha ukapande za mbezi ukitokea segerea la sivyo hapo mawasiliano utakesha
Najiuliza tabu yote hii kwa wakazi wa Mbezi na Kimara kwanini? Pale Mawasiliano usafiri wa sehemu zingine upo vizuri kasoro huu wa Kimara mpaka Mbezi.Hata zile daladala chache wamezigawa sijui namba 2 Kimara-Mbezi namba 1 Goba.Uongozi haulioni hili kwa wakazi wa Kimara Mbezi?
 
Back
Top Bottom