Aden Rage Mwenyekiti mpya Simba

hongera mzee mwenzangu, ila kazi tuliyokupa wanasimba uifanye kwa moyo wako wote, bado tunakumbuka uliyofanya ukiwa FAT..... usituangushe
 
Wamempa Rage ulaji!? jamaa kweli anapenda soka lakini anahusudu sana kuiba huyu...na pia maneno mengi mno hata siri huvujisha.....
 
Hongera sana Rage- tunaomba fuata nyayo za mzee Dalali,amejitahidi sana kutengeneza timu.
mpenzi wa simba no 1/
 

Ufisadi wake ni zao la CCM kwani yeye ni CCm damu. Nakumbuka siku ya hukumu ya kesi yake alienda kortini amevalua T-shirt yenye maandishi; 'CCM NO. 1' nguo ambayo aliondoka nayo kwenda Lupango siku hiyo. Alidhani CCM ingemuokoa!
Gazeti moja (sikumbuki lipi) lilitoa katuni ikimuonyesha hakimu akishindilia nyundo juu ya kichwa cha Rage aliyevaa Tshirt hiyo!
 
Jamaa kaanza vizuri, karipoti leo leo kazini, kakuta jengo halina umeme miaka 15!!, kaunganisha leo leo, umeme unawaka!.
Hala hala tuu isiwe nguvu ya soda.
Kaka Rage, huo ni mwanzo mzuri, najua wataka kurudi Tabora ili kuingia mjengoni, CCM hawatakusimamisha kwa sababu wao Yanga na rangi zao ndio uthibitisho!, jiunge Chadema wao hawana ushabiki maandazi, wao ni maslahi tuu ya taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…