Aden Rage aitwa "Bingwa wa Kudanganya" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aden Rage aitwa "Bingwa wa Kudanganya"

Discussion in 'Sports' started by Tisha-TOTO, Sep 13, 2012.

 1. Tisha-TOTO

  Tisha-TOTO JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 1,173
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Leading story ukurasa wa mwisho wa michezo wa gazeti la leo la Nipashe imemchanachana Aden Rage vibaya sana!!

  Jisomee mwenyewe hapa chini............
  ===================================================
  [h=2]Rage bingwa wa kudanganya[/h]


  Na Mwandishi wetu  13th September 2012

  Kauli kwamba Simba itajadili kujitoa kwenye Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara na kwenda kushiriki katika Ligi Kuu ya Zanzibar iliyotolewa na mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage juzi na kwamba ameitisha mkutano mkuu wa dharura jana, zimethibitisha kwamba kiongozi huyo anakurupuka katika anayoyasema na pia anawadanganya wanachama wa klabu hiyo.

  Rage alitoa madai hayo wakati akielezea kutoridhishwa na maamuzi ya Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambaye naye ni mjumbe, ya kumuidhinisha beki wa zamani wa Simba, Kelvin Yondani kuichezea Yanga.

  Katiba ya Simba inaeleza kuwa ili kuwepo na Mkutano Mkuu wa dharura ni theluthi mbili ya wanachama wa klabu hiyo wawe wamejiorodhesha majina yao kwenda kwa mwenyekiti na itakapothibitishwa uhalali wao mkutano huo utaitishwa ndani ya siku 45 na si ghafla kama alivyosema Rage juzi kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

  Kauli aliyoitoa kwamba Simba inataka kufanya mkutano huo kwa nia ya kujadili kushiriki ama kutoshiriki ligi ya Bara na pengine kuhamia katika ligi kuu ya Zanzibar hilo ni jambo jingine lililodhihirisha kauli za kukurupuka za kiongozi huyo ambazo hazistahili kutolewa na kiongozi wa klabu ambaye ni lazima ajadiliane na wenzake kabla ya kutoa taarifa kwa kuwa Simba si mali yake binafsi.

  Kutoshiriki ligi kuu ya Bara kunamanisha kwamba Simba itahitaji kulipa fidia ya mabilioni ya fedha kwa kukiuka mkataba wa udhamini binafsi kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yao ya Kilimanjaro Premium Lager, ambayo imezidhamini Simba na Yanga kwa mkataba wa zaidi ya Sh. bilioni 5 kwa miaka mitano.

  Timu haiwezi kuhama ligi kama mpangaji anavyohama kutoka nyumba moja kwenda nyingine.
  Simba italazimika kuonyesha kuwa ina maskani yake yake visiwani Zanzibar kwenye maeneo kama Bububu, Rahaleo, Pemba, Mkunazini na kwingineko, na wala siyo kwenye makao yao ya sasa yaliyopo Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

  Baada ya kukamilisha hilo, Simba italazimika kusaka usajili ili kuhalalisha uwepo wake kisheria Zanzibar na katika Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) ambako kabla ya yote, itaangaliwa kama hakuna klabu ya soka yenye jina linalofanana na lao (Simba).

  Super Falcon, kwa mfano, ikichukizwa na mwenendo wa Ligi Kuu ya Zanzibar, haiwezi kuhamia kirahisi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara bali italazimika kusaka usajili na baadaye kuanzia ligi za chini za TFF.
  Wakivuka kigingi cha usajili, Simba watalazimika kuanza kucheza ligi za chini hadi ije kufuzu kucheza Ligi Kuu ya Zanzibar, ambako udhamini wa pombe (kama kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager) haukubaliki.

  Wachezaji wa Simba waliosajiliwa kwa fedha nyingi na wanaolipwa mishahara minono nao watadai fidia kwa kuwa hawakujiunga na timu hiyo ili kucheza ligi za chini.

  Rage pia alizungumza na vyombo vya habari akiwa mkoani Dodoma na kusema anataka Yanga irejeshe fedha walizozitoa katika kumsajili Mbuyu Twite (Dola za Marekani 39,000) bila ya kuishirikisha Kamati ya Utendaji ya klabu yake ambayo yenyewe ilisisitiza kwamba haikuwa na nia ya kurudishiwa fedha bali walihitaji huduma ya mchezaji huyo.

  Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) aliwahi kutangaza kwamba ataileta klabu ya Birmingham City ya Uingereza lakini ziara ya timu hiyo iliyeyuka na baadaye alitamka kuingia mkataba na kampuni moja ya Uturuki kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa klabu hiyo ambao bado utekelezaji wake uko shakani.

  Inakumbukwa kwamba Rage alisema ujenzi wa uwanja huo utagharimu Sh. bilioni 74, lakini bila ya kusema fedha nyingi kiasi hicho zitapatikana wapi. Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam ulijengwa kwa Sh. bilioni 56 zilizopatikana kwa kiasi kikubwa kutokana na msaada wa serikali ya China.

  Rage aliudanganya mkutano mkuu wa wanachama wa Simba Agosti 5 mwaka huu kwamba mshambuliaji wao Emmanuel Okwi amefuzu kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Salzburg nchini Austria na kwamba Simba inatarajia kupata dola 600,000 (sawa na Sh. milioni 930), jambo ambalo halikuwa kweli baada ya Okwi kuiambia NIPASHE siku chache baadaye kwamba hakuwahi hata kujaribiwa na klabu hiyo kwavile alifika huko (Austria) akiwa anaumwa.

  Mwenyekiti huyo pia alidai kwamba Yondani aliidhinishwa kuichezea Yanga baada ya wajumbe kupiga kura, jambo ambalo limekanushwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji, Alex Mgongolwa, ambaye alisema hakuna kitu kama hicho katika kanuni na kwamba maamuzi yaliyofanywa yalizingatia kanuni, ibara ya 44(3) ya Kanuni za Uhamisho wa Wachezaji za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na pia ibara ya 18(3) ya kanuni za uhamisho wa wachezaji za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

  Inakumbukwa kwamba Rage aliwahi kusema kwamba amemsajili mshambuliaji Kenneth Asamoah kutoka katika klabu ya Asante Kotoko ya Ghana na kwamba Yanga waliojidanganya kwamba wamemsajili Mghana huyo kutoka katika klabu ya FK Jagodina ya Serbia wamepotea "chaka".
  Hata hivyo, baada ya Asamoah kutua Dar es Salaam na kuvishwa jezi ya Yanga yenye jina la Rage, mwenyekiti huyo wa Simba alisema alikuwa akitania tu watani zao.

  Alisema pia wanaanzisha Simba TV lakini cha kushangaza televisheni yenyewe ilipangwa kuwa ndani ya televisheni nyingine na licha ya kuzindua vipindi vyao, hadi leo imekuwa kimya.

  Wakati anachaguliwa kuiongoza Simba Mei 10, 2010, Rage alisema kwamba anataka kuona wachezaji wanaweka kambi kwenye jengo la klabu yao, wanakuwa na gym yao ya mazoezi, na kuahidi kufanya ukarabati wa jengo ndani ya siku 100 lakini kufikia sasa miaka miwili na miezi minne imepita (zaidi ya siku 850) jambo hilo halijatekelezwa na badala yake jengo la kwanza la klabu hiyo linaendelea kuchakaa wakati lingeweza kuwa ni kitega uchumi kikubwa. Kikubwa alichofanya ni kupaka rangi na kushughulikia tatizo la umeme.

  Wakati tunaenda mitamboni jana jioni, Kamati ya Utendaji ya Simba ilikuwa imekutana kwenye hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam kujadili ajenda ya kujitoa ama kushiriki Ligi Kuu ya Bara.


   
 2. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,012
  Likes Received: 1,144
  Trophy Points: 280
  ...duhi kweli Aden katisha...
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Rage amechanganyikiwa, ukuta wa timu yake unavuja kama tenga la mapapai, forwardline kimeo.
  Msisahau kwamba rage ni mccm, ni kawaida yao kukurupuka na kudanganya.
   
 4. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  I don't like Rage as politician and as sportsman either.He is full of himself,lier and worse enough ni M.W.I.ZI tu
   
 5. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,524
  Likes Received: 10,441
  Trophy Points: 280
  Rage anawachezesha bolingo wanasimba,ameshawajulia pakuwashika..
   
 6. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hivi Simba hawajui huyu Msomali na hamnazo, kazi ulimbukeni tu na kujidai anajua kila kitu.
   
 7. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,098
  Likes Received: 1,484
  Trophy Points: 280
  namsifu mwandishi aliyeandika hii story maana jamaa pia ni bingwa wa kuhonga waandishi ili wamwandike vizuri gazeti la mwanaspoti liliwahi kuhoji juu ya ahadi zake baada ya siku 100 akatishia kulishitaki na kudai fidia ya fedha kitu ambacho hakikufanyika kwa kifupi simba wasitegemee kujenga uwanja chini ya rage ataondoka akiwaacha na madeni baada ya kuwaibia pesa nyingi tangia aje simba amekuwa akiuza wachezaji waliosajiliwa wakati yeye hajaingia madarakani lakini yeye bado ameshindwa kufanya usajili wa maana
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,268
  Trophy Points: 280
  Ukiwauliza Wananchama wa Simba ni kwa nini wanamchakuwa mtu Tapeli kama huyu watakwambia eti anajuwa fitna za mpira!! wajinga ndio waliwao Simba na Yanga zimejaa wanachama mazuzu mazuzu tu.
   
 9. M

  Masuke JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mbona mwandishi mwenyewe kadanganya anasema kikao kilifanyika hotel ya movenpick wakati hakuna hotel yenye jina hilo nchini Tanzania, hayo mengine aliyoandika tutaaminije?
   
 10. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  maharage bwana , ni matamu SANA, ila yavimbisha tumbo mnooo !
   
 11. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,135
  Likes Received: 2,159
  Trophy Points: 280
  Siasa hadi kwenye Soka.... Simba Vueni Gamba mvae Gwanda...

  Nimekumbuka wimbo wa Diamond Unanidanganya danganya
   
 12. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,346
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Na Mwandishi watu!

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 14. T

  Tanzania1960 JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe unaye weka hii picha kila mara unajifurahisha kweli kweli ,ngoja hiyo tarehe 3/10 hutaonekana humu kwa sababu zitakua goli nne tuu za halali .this is a promise.nyie mlifanya kitu fulani kushirikiana na timu yenu ile ya lamba lamba kutuadhiri sasa zamu zenu.hongera timu nzima ya yanga sasa tuko na umoja.:a s 465::a s 465:
   
 15. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  utawajua tu wahanga wa rageliasis
   
 16. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  I like Rage. Tena Kocha angekuwa Julio halafu Mwenyekiti Rage wange team-up zaidi kuchangamsha ulimwengu wa soka la TZ kwa vijembe, n.k. (na waandishi wangepata story nyingi tu za kusisimua za kutangaza/kuandika)
   
 17. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,983
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Msanii tu huyo msomali.
   
 18. Tisha-TOTO

  Tisha-TOTO JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2012
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 1,173
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Hata ingekuwa 100 - 0 bado haiwezi kuzifuta hizi records hapa chini!

   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tuwekee na mashindano ya Kimataifa Yanga imeishia wapi na wapi na Simba imeishia wapi.
   
 20. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  umeonyeshwa recodi apo umebaki kubwabwaja tu kama upo mkutano wa ccm, umekosa sera huna hadhi ya kimataifa hata uganda utambuliki,. Kuna kombe gani la kuku linandaliwa la kuku tupeleke simba akachukue
   
Loading...